gimmick vs must have feature kwenye simu yako ya mkononi.

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,062
Reaction score
43,487
ni kawaida kwa simu mpya kutoka watu kuongelea specs kama processor na ram za hio simu, huku wakiviona hivyo vitu kama ugunduzi mkubwa. manufacture wa simu wamekuwa wakituziba macho kwa kutuekea specs kubwa ili wasitekeleze jukumu lao la kufanya research na kutuekea vitu vitakavyo optimize software kufanya kazi kwenye specs ndogo.

-gimmick ni trick ambazo manufacture wa simu wanazitumia ili wewe mteja uone simu zao ni nzuri wakati hio trick hata haina faida kwako zaidi ya kuwaringishia marafiki. mfano wa gimmick ni kama air gesture ya samsung haina maana kwenye real life na wala haiongezi productivity.

-must have feature hivi ni vitu vipo kwenye simu kiasi kwamba ukivikosa unahisi kama simu haijakamilika. ili kuweka mada interesting nitataja/utataja vitu ambavyo vimegunduliwa kuanzia mwaka 2010 hadi leo tuache vitu vya zamani.

vitu vya lazima kwenye simu

1. kioo cha hd.
sikumbuki ilikua ni samsung au lg alioanzisha kioo cha kwanza cha hd ila kuna umuhimu mkubwa kuwa na kioo cha hd kwenye simu. kwa simu yenye kioo ukubwa wa inch 5 kushuka chini hd (720p) inatosha kabisa kufanya kioo kuwa kizuri. pixel zikizidi hapo inakuwa ni gimmick tu.

2. camera nzuri.
mwaka 2012 ulikuwa ni wa mapinduzi ya camera baada ya nokia kutoa simu ya pureview baada ya hapo tukaona makampuni kama samsung akija na isocell camera, motorola akaja na clearpixel, htc akija na ultrapixel na wengineo wakija na innovation tofauti. hivyo ni muhimu simu kuwa na camera nzuri.

3.network ya 4g
japo tanzania ipo maeneo machache ila ni must have nayo.. advantage ya 4g lte ni kuwa speed yake ipo constant, haishuki na kupanda kama ya 3g hivyo ukiambiwa ni 5mbps basi ujue ni 5mbps kweli hivyo inafanya simu iwe reliable kwenye kuangalia video online na task nyengine kubwa za internet.

4. multiple window na chat head
sasa hv simu zinafanya task nyingi hivyo zinahitaji kuonesha task zaidi ya moja kwenye kioo. chukulia mfano upo internet unafanya kitu cha muhimu halafu ghafla mtu kakutext inabidi utoke internet/minimize halafu ukamjibu text then urudi. ila kwa multiwindow au chat head kama fb messanger utaweza kuchat na kumjibu fasta tu. hichi kitu kimeanzia win rt/w8 na kimekuja hadi kwenye simu sasa hv samsung na lg wana hii feature

5. uwezo wa kulocate simu yako iloibiwa.
manufacture wengi wa simu wanadharau hiki kipengele. apple wanajitahidi wameweza kuifanya iphone ya ios7 kuwa ngumu kuiba kwa kueka simu iwe rahisi kuipata pale ikiibiwa.

6.led light
kile kitaa kinachowaka mbele ya simu ni muhimu sana kwangu. kinajulisha kama kuna notification au bettry ipo low au battery ipo full au simu inaingia chaji bila hata kutoa lock.

7. battery nzuri.
kila mtu anatamani simu inayokaa na chaji atleast siku moja kwa matumizi ya poweruser lakini hakuna manufacture aliefanikiwa hivyo hapa hakuna anaepewa credit hata mmoja.

gimmick features
hizi zipo nyingi sana nitataja chache tu hapa chini.
1. air gesture ya samsung
2. curved smartphone (simu zinazopinda)
3.vioo vya 2k na full hd
4.speaker kali (wakati mda wote una earphone)

je unafkiri vitu gani muhimu na vipi havina maana kwenye simu ya kisasa?
 
Sijawahi kujua non removable battery ndo inafaida gani kwenye simu.

All in all as long as my Lumia ikiwa na battery ya zaid ya 3500 nahisi ntaiona kali kuliko zote, hayo ya gimmick features sio muhimu kwangu. Just a battery life.
 
Vitu ambovyo ni gimmicks
1: Kwangu mimi nfc na infrared ni gimmicks, bluetooth inatosha kabisa kureplace hivi vitu.
2: Pia ukubwa wa screen display ni gimmick, sasa hivi makampuni ya simu yanatengeneza simu zenye screen kubwa sana mpaka imefikia wakati mtu anashindwa kutofautisha kati ya tablet na simu ya kawaida, hata ubebaji wake ni kero, shukuruni kwa kampuni ya Apple Inc kwa kuweza kututofautishia kati ya simu ya kawaida na tablet
3: Non removable battery, ukiwa na simu ambayo ni none removable battery inakunyima uhuru wa kubadili battery nyingine pindi charge inapoisha, kama ndo unasafiri charge imeisha ndo basi

Vitu muhimu
1: Kioo kugumu kichokwangulika kirahisi, shukurani kwa Corning Inc kwa gorilla glass
 
non removable ni battery zisizotoka. manufacture wanazieka kupunguza cost ili wapate faida kubwa. pia inafanya wateja wasinunua battery fake kueka kwenye simu original.
 
ningekua ulaya nfc ningeieka kwenye must have feature sababu haihitaji kupair kama bluetooth inatumika kwenye malipo kama credit card vile. just unagusisha kwenye counter hela inakatwa.
 
Na hizi S Pen unaziweka kwenye kundi gani?
 
inategemea na kaZi unazofanyia. kazi nyingi za productivity kama za kiofisi s pen ni must have ila kwa kazi za play kama games ni gimmick.
 
ningekua ulaya nfc ningeieka kwenye must have feature sababu haihitaji kupair kama bluetooth inatumika kwenye malipo kama credit card vile. just unagusisha kwenye counter hela inakatwa.
mkuu chief hii NFC hata kenya wanataka kuianzisha kulipia bidhaa.
 
yah lakini ili nfc iwe na maana inabidi kuwe na vimachine vyake vingi kadri iwezekanavyo. vikiwa vichache watu wataona ni gimmick tu.

vodafone_australia-smartpass-dsc_7103.jpg
 
non removable ni battery zisizotoka. manufacture wanazieka kupunguza cost ili wapate faida kubwa. pia inafanya wateja wasinunua battery fake kueka kwenye simu original.

na mie ninae badili battery pale ninapoona imeanza kuchoka nafanyaje? au ndo kununua simu mpya?
 
kilugha rahisi zilitakiwa ziitwe harder to remove battery na sio non removable. unaweza kuzitoa na ukabadilisha lakini ni ngumu kuzitoa. itabidi uchukue screw driver ufungue simu nyuma ndio uweze kuitoa battery.
 
okay mkuu, thanks aisee
 
Back
Top Bottom