George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 148
Wakuu,
Pamoja na mijadala kadhaa inayoendelea hapa JF kuwa na hoja zilizo nzuri kwa maslahi ya taifa letu, upo uwezekano mkubwa kwamba, maadam mchokozi na watu wake nao wanajua Kiswahili, pengine wako nasi mtandaoni wakifuatilia kila kinachoandikwa kwa sababu zao za kiintelijensia.
Hivyo tunapoendelea kujadili, si vibaya kutahadhari tusijikute tumesaidia kumweleza adui kila udhaifu tulionao. Badala yake, tunaweza kujikita katika kuanika kile anachoendelea kufanya katika eneo letu na kile anachokusudia kufanya baadaye.
Wazee wa kule kanda ya ziwa Nyanza wana msemo; Zamani chui alikuwa hajui kukamata shingo la mawindo yake, alijifunza baada ya kusikia mawindo ya kinong'ona kwamba; ‘tunachomoka maana anakamata mikia, siku akikamata shingoni, tumekwisha'