nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Wakuu,
Pamoja na mijadala kadhaa inayoendelea hapa JF kuwa na hoja zilizo nzuri kwa maslahi ya taifa letu, upo uwezekano mkubwa kwamba, maadam mchokozi na watu wake nao wanajua Kiswahili, pengine wako nasi mtandaoni wakifuatilia kila kinachoandikwa kwa sababu zao za kiintelijensia.
Hivyo tunapoendelea kujadili, si vibaya kutahadhari tusijikute tumesaidia kumweleza adui kila udhaifu tulionao. Badala yake, tunaweza kujikita katika kuanika kile anachoendelea kufanya katika eneo letu na kile anachokusudia kufanya baadaye.
Wazee wa kule kanda ya ziwa Nyanza wana msemo; Zamani chui alikuwa hajui kukamata shingo la mawindo yake, alijifunza baada ya kusikia mawindo ya kinongona kwamba; tunachomoka maana anakamata mikia, siku akikamata shingoni, tumekwisha
Jamani ni kitu gani tunachojadili humu kitasaidia Wamalawi Kiitelijensia? Wengine hata hatuko Bongo tunaongelea
Maoni yetu kweli itahatarisha Usalama wa Taifa letu? Kweli tumeanza kuwa na maisha ya kiuwalakini? sasa hata jani
likitugusa tunaruka tunadhani ni NYOKA? tumekuwa DHAIFU kiasi hicho?
How Shocking... Hembu tueleze UDHAIFU gani humu Jamii Forums tutamueleza MMALAWI atumalize taifa la watu
MILIONI 40? na wao MIL 7? OH wana NUCLEAR BOMB?
TAFADHALI USITUNYIME UHURU WA KUCHANGIA HUMU KWENYE JAMII FORUMS; THE ONLY PLACE ANGALAU TUNAONGEA
KWA UHURU WETU...