DAWASCO acheni uzembe hapa bunju watu hawana maji licha ya kufungiwa mabomba kwa mbwembwe. Ukiuliza unaambiwa pressure ndogo haitoshi maji hayawezi kufika huko sasa mlifunga ya nini mje mchukue mabomba yenu.
Wadau naombeni ushauri nataka kununua Brevis 250i au Mark x 250G. Naomba kujua kwa wenye uzoefu ni ipi bora kwa matumizi ya kawaida na siku moja moja safari za mapumziko mkoani.
Kwa hili la Bashite linaweka doa ambalo litadumu daima kwenye historia ya nchi hii kuhusu HAKI. Inawezekana vipi wengine kutumbuliwa ndani ya saa 24 wakati wengine wanaachwa tu? Bado tunasafari ndefu sana.
Mh. Mkulu kukimbilia au kutishia kuwafukuza wawekezaji au kutaifisha mali zao si suluhisho la matatizo ya nchi yetu bali ni kuzidi kuumiza uchumi na kuudidimiza kabisa. Ifike mahali hata kama Serikali zilizopita zilifanya makosa na wewe ukiwa mmojawapo ambapo ulikuwa huko kwa miaka 20...
Pia Sheria inaruhusu kama mwajiri hawahitaji awalipe mafao yao yote kwa miaka hiyo waliyokuwa nje ya kazi plus mishahara ya miezi 12 (mwaka mmoja). Hivyo mwajiri anazo option mbili aidha kuwapokea au kulipa malpo hayo.
Ni aibu sana kuwa na nchi inayowaza vyanzo vile vilen tangu Uhuru. Madai yao eti bia si hitaji la msingi hivyo hata ukikosa huwezi pata madhara ndiyo maana kila mwaka kodi juu. Ifike mahali Serikali iwaze angalau hatua moja mbele si kila siku pale pale.
Waziri wa Viwanda unasubiri nini ofisini usitumbue majibu kwenye taasisi zilizopo chini yako. Hasa sisi tuliopo taasisi za utafiti kuna majipu yanayotoa usaha. Mfano CARMATES, TIRDO, nk
Jana nilimsikia kweli ni mabadiliko mazuri sana ndani ya muda mfupi. Na hapo amegusa tu bandari na TRA je kwingineko kama madini, maliasili, makampuni ya simu nk nk nk??? Huenda tukafikia uchumi wa kati ndani ya muda mfupi ujao. Tumpe support ngosha atafanya mambo.
Mwarobaini wa mambo kama haya yalikuwa yapatiwe ufumbuzi kwenye katiba ya Warioba ambayo ingeondoa hivi vyeo vya kupeana kama njugu. Ifike mahali tuwe wastaarabu jamani na kutumia busara zaidi kuliko mabavu. Je mmetoa picha gani kwa wananchi mlioenda kusikiliza shida zao badala yake mnaishia...
Dr Francis yeye misifa ya hovyo na kujitia ujuaji kumbe hakuna kitu. Alijisifu sana kuwa kwenye bodi ya TPA angalau Magufuli amemtumbulia mbali. Anapaswa kunyofolewa tena kwenye bodi ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi.
Kweli hawa jamaa wako fair kuliko maelezo, mimi ndugu yangu aipata kazi hatukuamini kabisa. Kweli namshukuru Mungu sana hawa ni ukombozi kwa watoto wa watu wadogo ambao hapo awali walikuwa hawachomozi kwenye ajira. Anaye walaumu hawa jamaa ni kumuelimisha tu ajirekebishe na asikate tamaa siku...
Wadau kwa hatua hii ya JPM ni wazi kuwa huenda tukawa na Tanzania mpya siku za usoni kama haitakuwa ni nguvu ya soda. Aidha kwa hatua mbili tatu alizochukua hadi sasa ni wazi kuna alama za matumaini siku za mbeleni kama tutampa support. Mimi kama mdau ningeomba wale wenye data kuhusiana na...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.