Kama mlikuwa mnafuatilia toka mwanzo, huyu Naibu Meya toka TLP alikuwa haeleweki toka mwanzo. Mara hakubaliani na kuchaguliwa kwa sababu hakushiriki uchaguzi, mara, anaendelea na nafasi yake! Inawezekana mwenyewe hakuwa na msimamo wowote, au alikuwa anayumbishwa na mwenyekiti wake LYATONGA!
Bado naamini michango mbalimbali inayotolewa hapa itasaidia KUWASAMBARATISHA hawa Dowans feki. Je, kwa kutaja hao wakurugenzi wa kufikirika, watakuwa na ubavu wa kwenda kuisajili hukumu hii Mahakama Kuu ili walipwe?
Baada ya kutajiwa makampuni yenye hisa na wakurugenzi wake, maswali yamekuwa mengi kuliko majibu. Nadhani sasa wakati umefika wa kusema bayana 'enough is enough'. Zile salamu za Arusha zikiingia jijini, hakuna kitakacholipwa. Wanashabikia kulipa kwa sababu wanajua malipo hayo yanapotelea hapa...
Tatizo, Great Thinkers wa Arusha wamejifungia vyumbani la laptop zao, wanaoumia ni walalahoi wa Ngarenaro! Matokeo yake, hata habari za on field haziji sawa sawa.
Tuache usanii, tufanye tunachohubiri!
Mimi ningetarajia kuona great thinkers wanajadili uwezo wa kuchambua mambo, badala ya uwezo wa kuongea kiingereza. Nina wasiwasi, hata aliyeanzisha mada hii, akikaa na porter toka wingereza ambaye hakusoma hata sekondari atamuona bonge la mtaalamu kuliko yeye mwenye shahada!
Kiingereza ni...
Habari za mtu kuoa au kutooa ni mawazo ya kijima kabisa. Mbona hata hapa jamvini wapo members wengi tu hawajaoa na wanaendelea kulijenga taifa kama kawaida?
Nilipigiwa sana kelele za kuoa nilipokuwa under 40, lakini sasa, hata hao wamekata tamaa na kuheshimu maamuzi yangu.
Kila kitu kina pande mbili. Mkikaa hapa kuongelea upande mmoja, kamwe hamtafikia conclusion ya maana.
Yako mengi tu ambayo bwana Mengi ameyafanya, haihitaji kuorodhesha hapa. Lakini pia, yapo mapungufu ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuboresha sura ya mjasiria mali huyu mbele ya jamii:-...
Drifter
Naungana na wewe kwa asilimia 100. Tunatazamia great thinkers kuchambua hoja kwa uzito wake, sio nani kasema.
Ukiangalia kauli hizo mbili, bila kujali nani kasema na anajikomba kwa nani, ni dhahiri kwamba mtoa maoni wa kwanza EL alikuwa sahihi. Mji wa Arusha si wa madiwani na...
Mazingira tuliyokuzwa kati ya miaka ya '60 mpaka '90 ilionekana dhambi kutaja Tanganyika. Wengi wetu tukahusisha Tanganyika na ushamba! Mahali kulikosahaulika tukakuita Tanganyika. Kumbe hiyo ilikuwa sumu maalumu ya kuhakikisha kwamba mwisho wa siku tutakuwa radhi kujikana wenyewe.
Ni wazi...
Tukio hili linanikumbusha mtu mmoja aliyekuwa anaitwa sipendi rajabu. Mwaka 1981 alitutembelea shuleni kwetu pale tanga akiwa na kabrasha kubwa lenye mihuri ya kila aina. Alichotuambia kilituacha na maswali mpaka leo:-
alisema yeye ni mzaliwa wa musoma, amekuwa akitembea kuunga mkono azimio la...
Acid
Ni kweli kabisa wana jamvi wanatakiwa kujadili mambo kwa kina na mapana, badala ya kuishia kushabikia Mrema kuondoka. Tusije ishia kufanana na hadithi ya kijiji kimoja chenye hospitali ya misheni. Naambiwa kwamba wakati nchi inakaribia kupata uhuru, watu wa kijiji kile waliambiwa kwamba...
Naungana na wote wanaosema TCRA wanatakiwa kutoa maelezo zaidi, pamoja na umuhimu wa kuwahusisha polisi. Tatizo hapa ni ukweli kwamba namba hii inaonekana ni ya nje. Hakuna nchi yenye code +3 wala +35. Lakini Finland code yake ni +358. Swali hapa ni kujua kama kweli SMS hizi zinatumwa toka...
Tangu siku ya kwanza nilipoingia form I, Chemistry, Physics na Biology nilikuwa nikisoma nikiwa Labaratory. Huwa najiuliza, hivi nikialikwa nikatoe mada ya Chemistry kwenye shule hizi nitafanyaje? Sana sana najua nitaishia kuitwa mbabaishaji, kwa sababu nitashindwa 'kubabaisha' kwa kukosa...
Bado ninakuwa na wasiwasi na hiyo mitego ya TAKUKURU. Nadhani ni viherehere wasiokuwa na nia ya kweli kuwakamata watuhumiwa. Mbona zile kesi nzito za Moshi, Tabora.... zimeishia hewani?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.