RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe

RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
60,053
Reaction score
135,358
Wanabodi

Huu mtindo wa viongozi wetu wenye dhamana kutoa kauli za hovyo hovyo, kauli za udhalilishaji na za kimipasho mipasho zinazidi kushika kasi, japo najua wanamuiga nani kwa utoaji wa kauli hizi, nawauliza, hivi hawamuoni Makamo wa rais Mhe. Mama Samia Suhuhu Hassan, kwani yeye hana mdomo?. Ua hawamuoni Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa, kwani yeye hana mdomo?

Mbona viongozi hawa hawatumii lugha za kuudhi?.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuwashangaa viongozi wa taifa letu kwa kukiri kuwa kila awamu, ina mazuri yake na mabaya yake, akawashangaa viongozi badala ya kuiga mazuri, wao wanaiga mabaya!.

Hivyo viongozi wetu nao pia ni binadamu, wana strengths zao, na weaknesses zao, yaani wana mazuri yao na mabaya yao, hivyo nyie viongozi, msiige kila kitu cha viongozi wakuu wenu, igeni mazuri yao tuu, na mabaya yao waachieni wenyewe!.

Nyie mnaiga tuu yote yakiwemo mabaya!. Miongoni mwa baadhi ya mabaya ya awamu hii, ni kauli za hovyo hovyo za baadhi ya viongozi ambazo badala ya kuleta upendo kujenga umoja na mshikamano, zinachochea chuki, kuleta utengano na mifarakano!. Hata Mungu hapendi kauli ambazo sio za kuhamasisha upendo na mshikamano, na viongozi wote wanaotoa kauli hizi, watahukumiwa na mahakama ya karma!.

Mimeisikia hii kauli ya hii ya RC Makonda



Kiukweli kauli hii sio kauli nzuri. RC Makonda, Makonda ni Mkuu wa Mkoa wetu wa Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam ni metropolitan society, lina watu wa aina zote na vyama vyote dini zote, hali zote. Ni Jiji la wote.

Mhe. Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, chama ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Mkuu wa Mkoa, Makonda amemuita Mhe. Mbowe ni mwanasiasa uchwala aliyefilisika!. Hii sii kauli nzuri kutolewa na Makonda ni kama kumtukana Mhe. Mbowe!.

Mhe. Zitto ni kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Makonda amemuita Mhe. Zitto ni mganga wa kienyeji na mshirikina!. Hizo ni lugha za matukano, ni lugha za kuudhi!.

Kwa wanaopenda makala fupi, tuishie hapa
kwa wale wakata issues tuendelee
Nani Zaidi Kati Ya Mwananchi, Kiongozi wa Watu na Kiongozi Mtu?.
Kwa vile hili ni bandiko elimishi kwa kiongozi wetu wa jiji letu, sio vibaya nikitoa elimu kidogo ya nani ni zaidi kati ya mwananchi, kiongozi wa watu na kiongozi mtu.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977, watu muhimu kabisa kwenye taifa letu ni wananchi, "we the people", wananchi ndio wenye katiba, katiba ni mali ya wananchi, wananchi ndio wenye nchi, Tanzania ni mali ya wananchi wa JMT, sio mali ya viongozi. Wananchi ndio wanawaajiri viongozi kupitia kura zao wawatumikie na ndio wanaowalipa mishahara yao. Hivyo wananchi ndio watu muhimu number moja kuheshimiwa.

Baada ya wananchi, wa pili kwa umuhimu ni viongozi wa watu, hawa ni viongozi waliochaguliwa na wananchi kupitia kwenye sanduku la kura zao, kuanzia rais wa JMT, wabunge, madiwani, na wenyeviti wa mitaa, ni viongozi wa watu, waliochaguliwa na watu kama wawakilishi wao kwa niaba yao, hivyo hawa ni watu wa kuheshimiwa sana kwasababu wamechaguliwa na watu, sauti ya watu ni sauti ya Mungu!, (vox pupuli is vox Dei), hivyo viongozi wote wa kuchaguliwa kupitia sanduku la kura, ni viongozi waliowekwa na Mungu!, sio wa kubezwa hata kidogo!, Mungu asijekukasirika akakupiga kibao!.

Kundi la tatu ni viongozi watu, hawa ni viongozi wanaoteuliwa, kumsaidia rais wa JMT, hivyo ni wasaidizi wa rais, miongoni mwao wamo viongozi wa watu kama wabunge na viongozi wa kuteuliwa kama ma RC, ma DC na watendaji wengine ambao sio chaguo la wananchi.

Wateule wote wa rais, ukiondoa wale wenye kinga ya kikatiba, Majaji, na CAG, wengine wote wako hapo walipo kwa hisani tuu ya rais, at presidents pleasures. Hakuna mwananchi anamchagua RC au DC, na ikitokea tuu rais akaamka vibaya, unajikuta huna kazi!.

Kwa siku za hivi karibuni imetokea baadhi ya wateule wa rais kujiinua sana dhidi ya viongozi wa wananchi. DC au RC anajiona yeye ni bora zaidi kuliko Mbunge, kisa tuu ana mamlaka makubwa kuliko Mbunge, RC na DC ni watendaji wa kuteuliwa, kamwe hawawezi kuwa wakubwa kuliko wawakilishi wa wananchi!.

Hili la ma RC na ma DC kujiinua sana, nimewahi kulitolea somo.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika - JamiiForums

Hivyo ni muhimu sana kwa viongozi watendaji na wateule wa rais kuwaheshimu sana viongozi wa watu, kwasababu wao wako kwa hisani tuu ya mteule, lakini viongozi wa watu wako kwa mujibu wa katiba. Rais Magufuli anaweza kumfukuza kazi Makonda wakati wowote, any time, lakini hawezi kumfukuza kazi mawakilishi wa wananchi!, hata sheria inayoruhusu Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa Mtaa kupoteza uongozi kwa kuvuliwa uanachama wa chama cha siasa iko kinyume cha katiba! its a bad law!.

Kitendo cha RC Makonda kutumia lugha kama hizi kwa viongozi wawakilishi wa wananchi au viongozi wa watu na viongozi wakuu wa vyama vya wananchi wako, sio jambo la kupendeza, hata kama ni kweli Mhe. Mbowe ni mwanasiasa uchwala aliyefilisilika, mwache na wafilisika wake!, Kutangaza kwamba mgonjwa fulani wa Corona ni ndugu na Mbowe, huko ni kutoa nje siri za mgonjwa!, unless Mbowe mwenyewe au mgonjwa mwenyewe atangaze ni ndugu na Mbowe, kinyume cha hapo ni kinyume cha maadili kwa kuingilia haki za mgonjwa na the right to privacy ya Mhe. Mbowe!.

Kuhusu Zitto, hata kama huwa mnakutana na Zitto kwa waganga wa kienyeji na ma sangoma washirikina, au hao waganga na washirikina pia wanaripoti kwa RC kuwa leo wamemuhudumia nani na nani, hizo ni siri za wananchi wako, huko ni kuingilia the right to privacy ya wananchi wako. Hata kama unazijua siri hizo, lakini hupaswi kuzisema hadharani tena kwa lugha ya kejeli au kubeza mila zetu za asili, maana kiukweli zimesaidia wengi, na kwa vile hata wewe ni mtoto wa pekee kwa wazazi wako, ongea haswa na mama yako, ili ujue jinsi alivyohangaika kukupata, alikwenda wapi na wapi, na alifanya nini na nini hadi ukapatikana!. Wanaojua wapo!, wakiibuka na kuyasema ni kuwadhalilisha, tena mambo mengine ya mama zetu katika kutafuta watoto, naomba tusiyaseme kabisa kwa heshima za mama zetu!.

Mtu huwezi kuibuka na kuropoka tuu Zitto mshirikina!, these are very serious allegations zinaposemwa na the executives kama RC, Zitto akikuibukia na kukuita u proove itakuwaje?. Makonda uliza kilichotokea Mwanza 1976!, mtu akinyooshwa tuu kidole kuwa ni mshirikina!, hafiki kesho yake, watu wa kazi wanamfanyia kazi usiku huo huo, asubuhi ni taarifa za mauaji ya kutisha!.

Viongozi wa executives tutofautishe uongozi wa umma na ukada wa vyama, mtu wa kuyasema haya ni kina Polepole na timu yake, mtu kama Polepole hata akisema lolote kama kufananisha wapinzani na Corona, itachukuliwa lightly kuwa ni politics lakini sio wewe RC Makonda japo ni kada wa Chama cha Mapinduzi, lakini as RC, wewe sio kiongozi wa chama ni kiongozi wa wote, hivyo kutumia kauli za mipasho ya kikada dhidi ya viongozi wa vyama vya wananchi wako, sio jambo jema!.

Nautoa ushauri huu very genuinely kwa RC Makonda, japo ni bosi wetu na Mkuu wetu wa Mkoa, hivyo Ki Darisalaam, Makonda ndio kama rais wetu, lakini sisi tunaomshauri haya, japo we are nobody, lakini wengine wetu, tumemzidi umri, hivyo Makonda ni mdogo wetu kiumri, kwa lugha za mtaani huyu ni Dogo, ikitokea wewe ni kaka mkubwa, unamuona dogo ana haribu, na huyo dogo unampenda, hutamuacha tuu aendelee kuharibu, asije akaharibikiwa mbeleni, utampa ushauri wa bure.

Tena na hata hapo alipofika, kwa vile yeye Makonda anahesabu ni kazi ya Mungu tuu pekee ndiye aliyemfikisha hapo, anaweza asijue kuwa kuna kauli huumba!, unaweza kukuta kauli kama hii, iangalie ilitolewa lini na baada ya siku ngapi tangu kauli hii kutolewa Makonda aliukwaa u RC.
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums
imechangia kumfikisha Makonda hapo alipo, tena bado tuna matarajio makubwa sana na Makonda huko mbeleni.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... - JamiiForums

Mhe. Paul Makonda, sisi wananchi wako wa Jiji la Dar es Salaam, tunakupenda sana na tunakukubali sana kwa uchapakazi wako kama Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, tuna kuheshimu sana kama rais wetu wa mkoa, tunakuomba na wewe ujiheshimu, heshimu watu wote wa jiji lako na vyama vyao, na viongozi wao, ili na wewe uheshimiwe na wote wa vyama vyote na viongozi wote! Sasa asijiharibie chances zako za mbeleni kwa kauli za hovyo hovyo kama hizi.

Kaka yako
Paskali
Rejea za jinsi Makonda Anavyokubalika.
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... - JamiiForums

Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni - JamiiForums

Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! . - JamiiForums

Madawa ya Kulevya: Kumbe Makonda Alizuiwa Kutaja Majina!. Anaamini Uwazi, Atunge By-Law Ataje Majina - JamiiForums

Mayalla Paschal bado unaamini kuwa Paulo Makonda bado ni Presidential material? - JamiiForums

Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanamwaminije Gwajima kuliko Rais wao?!. - JamiiForums

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... - JamiiForums

Je, Tanzania tunahitaji viongozi gani?. wajinga wachapakazi, au mangi meza wenye vyeti?. - JamiiForums

Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!. - JamiiForums

Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
 
Huo ndio mnara wa babeli watu wananena kwa lugha zao.nMadaraka yamekuwa machungu wanasiasa wanamtafuta mchawi.

Na huo ndio mwanzo lakini ule mwisho bado so usiogope Pascal. Wanasiasa wetu wataongea mambo ya kushangaza zaidi ya hayo unayoyaita matukano.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mimi sjawai kumpenda Makonda, na ni mwananchi wa Dsm tafadhali badilisha andiko lako andika kuwa wewe pamoja na wale wanawake alio wakusanya ofisini kwake kwa madai kuwa wametekelezwa na waume zao ndo mnampenda ila sisi wananchi wa Dsm wenye akili zetu timamu hatuwezi kumpenda mwanaizaya kama makonda.

sifileo. Pascal Mayalla,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom