Jina Dr. Magufuli latawala kila mahali uchaguzi mkuu wa Kenya. Tanzania tunapata ujumbe gani?

Inatupa ujumbe kwamba huwezi jua shida wanazopitia jirani mpaka uende kuhamia kwao...... mfano gadaffi kila mtu alimuadmire ila mbona walibya walimpindua??? Kwame nkurumah anakubalika kila taifa hapa afrika ila mbona wananchi wake walimpindua????

Nachojua wakenya wanataka mabadiliko ila kusema magufuli ni rais bora nop ni mapema sana ingawa kwa marais waliopo hapa east africa hta kma mie ni mpinzani naafiki amewazidi sana kwa mbali kwenye uchapakazi ukiachana na kagame
Hakuna binadamu mkamilifu hata mmoja yule hapa duniani...hayupo.nashukuru hata kwa kutambua uchapakazi wa Dr Magufuli. Basi hilo ndilo linalombeba huko Kenya wanata viongozi wanaonyesha njia na utendaji unaonekana kwa wanainchi bila kuogopa sura wala jina la mtu.
 
Mpiga dir ,cheti feki,mtumish hewa huwez kuwa na aman

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi kuhusu mtumishi mwaminifu na asiye na shida na hivyo vyeti vyenu, lakini Rais wake kazuia hata promotion iliyokwishatolewa kwake, ikafutwa kwa kisingizio cha uhakiki? Au mamia elfu ya watumishi ambao nyongeza ya mshahara imekuwa hadithi?
 
Hakuna shida...tatizo lako ni nini kwa hapo! Serikali itatekeleza tu lakini si kama unavyotaka wewe!!
 
Tuwekee japo video au audio tusikie basi. Lumumba shida kweli..
Mambo ya Thomaso hayo!! JF si itajaa video Sasa kama kila habari tukiweka hizo clip!
 
Kiukweli Rais Jpm anafanya kazi vizuri japo kunawasioona mambo anayoyafanya ila ipo siku watamkumbuka kwa uzalendo wake ktk taifa hili hongera sana Jpm kwa kazi nzuri unazotufanyia wtz hadi mataifa jirani wanakusifia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mgombea huko Kenya anaposimama na kumwaga Sera zake na jinsi atakavyo wahudumia wakenya atakapochaguliwa baada ya uchaguzi ni lazima ajifananishe na Rais wa Tanzania Dr Magufuli Katika suala nzima la uwajibikaji bila kumuogopa yoyote.

Kila mikutano ya hadhara jina la Dr Magufuli limekuwa likitumika Katika kijinadi kwa wagombea.

Hii inatoa ishara gani kwa nchi za Africa Mashariki?
Magu nichaguo la Mungu
 
Kwa hiyo kila mgombea huko Kenya anajinadi kwa kuwaahidi wananchi kwamba akichaguliwa hataheshimu Katiba kwa kuilinda na kuitetea? Kwamba akichaguliwa atapiga marufuku mikutano ya kisiasa? Kwamba akichaguliwa atawakamata wapinzani bila kujali nafasi zao na kuwasweka ndani? Kwamba akichaguliwa wakuu wa mikoa na Wilaya watawakamata wabunge wa upinzani na kuwasweka ndani kwa saa 48? Kwamba Rais wa wanasheria wa Kenya hawatabaki salama na kuwa huru kutoa mawazo yao?

Wewe [B]tramadol[/B], unawajuwa kweli Wakenya?

Unajua kweli Katiba yao inasemaje?
Kila mikutano ya hadhara jina la Dr Magufuli limekuwa likitumika Katika kijinadi kwa wagombea.
Kwamba akichaguliwa atakuwa dikteta uchwara? Umekula maharage ya wapi wewe [B]tramadol[/B]? Unajua Wakenya walivyopigania uhuru walio nao? Unajua walivyoweza kukataa kuwa na Rais mungumtu? Yaani ungependa Wakenya waige huu utawala wa kindugu na kikabila wa kwetu? Kweli unajua walikotokea Wakenya mpaka wakafikia hapo walipo? Labda kama wewe ni mtoto mdogo kiasi hukujua walipataje Katiba mpya iliyowawezesha kumuondoa dikteta wao uchwara madarakani!
Hii inatoa ishara gani kwa nchi za Africa Mashariki?
Huyo atakayejinadi kwa hayo niliyoyaorodhesha hatashinda uchaguzi nchini Kenya. Kisiasa Kenya si wenzetu, sisi tuendelee tu na dikteta wetu uchwara tukiwaiga akina Museveni, Kagame, Kabila na Nkurunzinza.

Hakuna shida...tatizo lako ni nini kwa hapo! Serikali itatekeleza tu lakini si kama unavyotaka wewe!!
Sina hakika kama uwezo WA kuelewa nilichoandika hauna au unafanya makusudi.
 
Magufuli ni mtu mchapakazi, mwenye Maono na vitendo zaidi. Lakini hapendi tu Kukosolewa japo anapenda Kuwakosoa wakosoaji wake. Akirekebisha hapo tu yuko pw
 
Kwa hiyo kila mgombea huko Kenya anajinadi kwa kuwaahidi wananchi kwamba akichaguliwa hataheshimu Katiba kwa kuilinda na kuitetea? Kwamba akichaguliwa atapiga marufuku mikutano ya kisiasa? Kwamba akichaguliwa atawakamata wapinzani bila kujali nafasi zao na kuwasweka ndani? Kwamba akichaguliwa wakuu wa mikoa na Wilaya watawakamata wabunge wa upinzani na kuwasweka ndani kwa saa 48? Kwamba Rais wa wanasheria wa Kenya hawatabaki salama na kuwa huru kutoa mawazo yao?

Wewe [B]tramadol[/B], unawajuwa kweli Wakenya?

Unajua kweli Katiba yao inasemaje?

Kwamba akichaguliwa atakuwa dikteta uchwara? Umekula maharage ya wapi wewe [B]tramadol[/B]? Unajua Wakenya walivyopigania uhuru walio nao? Unajua walivyoweza kukataa kuwa na Rais mungumtu? Yaani ungependa Wakenya waige huu utawala wa kindugu na kikabila wa kwetu? Kweli unajua walikotokea Wakenya mpaka wakafikia hapo walipo? Labda kama wewe ni mtoto mdogo kiasi hukujua walipataje Katiba mpya iliyowawezesha kumuondoa dikteta wao uchwara madarakani!

Huyo atakayejinadi kwa hayo niliyoyaorodhesha hatashinda uchaguzi nchini Kenya. Kisiasa Kenya si wenzetu, sisi tuendelee tu na dikteta wetu uchwara tukiwaiga akina Museveni, Kagame, Kabila na Nkurunzinza.

Nimefanya kazi Kenya miji ya Nakuru,Kakamega,Nairobi na Mombasa.

Kenya wao walichokichukua kwa Dr Magufuli ni namna anavyofanya kazi hasa ktk kutatua matatizo ya wanainchi na ndiyo sifa inayombeba huko nje ya nchi.

Hayo sisi tunayoyaita ukandamizaji wao hawayajui kwasababu hayawagusi ila wewe na Mimi tuliopo hapa ndiyo tunaweza kuyazungumzia.

Kutokana na utumishi uliotuka wa Dr Magufuli ktk kushughulika na hayo matatizo ndiyo maana kila mmoja anaona ni kiongozi mwenye ujasiri na anayeweza kusema jambo na likawa na imeonekana wazi.

Na zaidi Dr Magufuli amekuwa field yeye mwenyewe na kutoa maagizo na kuchukua hatua Kali kwa watumishi husika.
 
Back
Top Bottom