Ni kweli hakuna cha uspecial wowote, mbona awali saili zake zilikuwa zinapitia utumishi, sema tu ni mabadiliko haya yaliyokuja ya kusema taasisis zijiendeshe zenyewe ikiwemo na suala la kuajiri zenyewe, nje ya hapo hakuna cha u special wowote hapo , usitake kudanganya watu.
Huu ulimwengu bana mambo ni mengi sana unaweza ukachanganyikiwa ukisikiliza rumours za watu, usaili wa mwisho umefanyika J5 , usaili ulikuwa na idadi kubwa sana ya wasailiwa mfano tax management officer II oral ni 847, leo hii hata wiki haijaisha una ambiwa watu wameshaitwa kazini, any way sisi...
Aisee nimeshangaa sana sasa si bora wange wa screen mapema na kuwaambia kuwa hawana vigezo kuliko watu wametupa nauli zao halafu mitihani wamefaulu baada ya kufaulu unawaambia irrelevant
Ni sahihi sana tunamshukuru sana Mungu kwa ajili yake Mama Samia, maana hali ilikuwa tete, nikikumbuka mwaka 2021 nafasi 6 za customs officer TRA , Interview candidates 15,000 hali ilikuwa mbaya sana , ila angalau kwa miaka miwili hii ya Mama vijana tumetoka sana kitaa.
Mfwende sawa dogo hongera na karibu sana kwenye utumishi wa uma , tunasema safari moja huanzisha nyingine Mungu daima ni mwema sana kwa watu wake, hakuna anayemtumainia akamwacha bila baraka zake, hio ni ahadi yake amesema hivyo katika Neno lake. Hivyo inapaswa ukamshukuru kwa Neema zake hizo...
Kama hamkutangaziwa siku ile mliofanya written basi ni ngumu sana kupata majibu hapa, swala la msingi ni kuwa na subira tu na kwa Imani siyo mbaya ukaanza maandalizi ya Oral.
Jitahidi tu kujikumbusha yale uliyosoma chuoni pia changanya na mambo ya Economics, pia ujue taratibu za kusajili biashara na sheria mbalimbali zinazotumika kusajili biashara, sifa za biashara zinazostahili kusajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania nk.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.