Asante sana Chief.
Naungana na wewe kusisitiza kuwa ni vyema sasa serikali ianze kulitazama hili jambo katika jicho la tofauti kuwanasua vijana waliozama katika janga hili.
Unaweza ukaandika uzi wa kushauri kuhusu hiyo sheria kali.
Mimi maoni yangu ni haya, hayabadiliki. Kama haujayapenda basi tumshukuru Mungu. Ndio demokrasia hiyo.
Na by the way, hiyo "sheria kali"
unayoitaka mbona ipo? Haujasoma sheria za nchi? imesaidia nini?
Utawafunga watoto wadogo jela...
Mbinu nilizozitumia nimezitaja kama kweli umenisoma vema mkuu.
Na nimetoa ushauri jinsi ya kufanya. Ushauri kwa wazazi, jamii na serikali.
Tukijikite katika hayo, ni ya muhimu zaidi.
Mheshimiwa amenielewa, na yeye ndiye mwenye mamlaka katika serikali naamini anajua cha kufanya.
Wewe endelea kutukana na kutoa laana, sisi tunasonga mbele katika kulisaidia taifa.
Ni kweli. Hata mimi nililelewa na baba na mama lakini haikusaidia sana.
Kuna mambo mengi zaidi ambayo wazazi wote kwa pamoja wanapaswa kuyatilia mkazo katika malezi ya mtoto.
Kuna watoto wamelelewa na mama tu lakini hawana changamoto yoyote ya aina hii.
Umakini unahitajika zaidi, na kudra za...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.