Tatizo liko wapi? Sehemu yenyewe Mburahati😁😁Unategemea nini?Watoto hao hawasikii la mwalimu wala la mzazi. Mbona hao wachache walifaulu? Acheni zenu bwana. Walipwe tena kwa wakati. Wakaguzi wako wapi? Timu ya wilaya ya elimu iko wapi? Waratibu wako wapi? Kamati ya shule iko wapi? Nani kaona...😂😂😂
Hongera sana kwa angalizo hilo la kamari na vinywaji vya kemikali. Tatizo la nchi hii ni aina ya siasa tuliyonayo. Siasa yetu ina mushkeli wa kiuchumi. Ukweli unabaki kuwa kuna maslahi ya kisiasa hivyo suala la afya ya wanywaji halitaangaliwa. Vyombo vinavyosimamia vyakula na tbs vipo hao...
Rais Samia katulia tuli. Unajua anasoma hoja zenu? Pengine wala hapendi sana kusifiwa sifiwa ila basi tu. Anaona hata nani anajigonga gonga. Shauri zenu. Utashangaa unamsifuuu yeye anakuchora...mie sipo!!!😅😅😅
.
Suala la Bashiru ni suala la msingi kuwa wakulima na wanyonge wote waungane kutoa sauti zao. Suala la Bashiru alikuwa nani halina mashiko. Kama alikuwa kibaraka au mwizi au mbaya sio hoja. Hoja yake ya sasa haina ubaya na ina msingi. Wanaobeza hawaelewi maana ya hoja au ndio hawana hoja...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.