Recent content by raiamwematz24

  1. R

    Ujumbe wa sauti wa vijana wa hamasa (CCM) unaochezwa kwenye vituo vya SGR usitishwe; unagawa abiria kiitikadi

    Kampeni zimeisha na tayari Serikali imepatikana. Huu si muda wa ofisi za umma kuendelea kutumika kufanya propaganda, kama vile kucheza sauti zenye jumbe za kiitikadi kana kwamba bado tupo katika kipindi cha kampeni ambacho tumezoea mambo hayo kufanyika, licha ya kwamba hayapaswi kufanyika hivyo...
  2. R

    KERO Barabara za Mitaa Wilaya ya Ubungo zimegeuka Machinjio ya vyombo vya moto, fedha za Matengenezo ziko wapi?

    Barabara nyingi za mitaa katika Wilaya ya Ubungo zimegeuka machinjio ya vyombo vya usafiri na chanzo kikuu cha hasara kwa wananchi, huku mamlaka husika zikionekana kushindwa kutoa suluhisho la kudumu. Katika Kata za Kimara, Makoka na Saranga, mashimo makubwa, matope na mifereji mibovu vimekuwa...
  3. R

    KERO Responded Maghorofa ya Shekilango NHC - Dar yananuka sababu ya kukosa maji

    Wakazi wa Shekilango jiji Dar es Salaam tunashida kubwa sana ya uhaba wa maji, hatuna huduma tangu mwezi wa Desemba 2025. Watayafungua wao, wakipenda kufungua na bili za maji kama kawaida yaaani tunaumia sana. Imagine unaishi maghorofa ya NHC hapo Shekilango halafu hamna maji, just imagine how...
  4. R

    PostGE2025 Serikali itarejeshaje Imani ya Wananchi, Jumuiya ya Kimataifa baada ya Uchaguzi wa Oktoba 29, 2025?

    Vurugu zilizotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 29, 2025 zimeacha alama nzito ikiwa pamoja na kuchafua diplomasia na uhusiano wa kimataifa. Vurugu hizo zilizotokana na maandaano katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Njombe...
  5. R

    KERO Kibamba - Dar es Salaam wengi bado tunalazimika kununua maji ya chumvi

    Kibamba wengi bado tunalazimika kununua maji ya chumvi Licha ya Serikali kukiri kuwa Tanzania si masikini wa vyanzo vya maji, bado kero ya maji imeendelea kukithiri hasa kwa miji mikubwa kama Dar es Salaam. Kero hiyo imedhihirika tena mwisho mwa mwaka 2025, kwa jiji la Dar es Salaam kukumbwa...
  6. R

    KERO Dar: Jiji lenye vyanzo vingi vya maji ikiwemo Bahari lakini kila kukicha Wananchi “wana kiu ya maji”

    Dar es Salaam ni jiji lililo na mito inayotiririsha maji kuelekea baharini, lakini kwa muda mrefu kumekuwa na uhaba wa maji. Kwa muda mrefu jiji hilo limekuwa likitegemea maji ya mto Ruvu unaopita mkoani Pwani. Wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba akiwa mto Ruvu alidai tatizo la maji...
  7. R

    PostGE2025 Jinsi Vyombo vya Usalama vilivyogeuza Ulinzi kuwa chanzo cha hofu

    Tangu yalipofanyika maandamano na baadaye vurugu wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 na baada ya hapo, kumekuwa na hofu kubwa kwa wananchi kutokana na kuongezwa kwa ulinzi wa polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Maandamano yaliyokabiliwa kwa nguvu na polisi na JWTZ yalisababisha...
  8. R

    Uchawa umepunguza imani ya Wananchi kwa Serikali

    Demokrasia inahitaji sauti huru na uwajibikaji wa viongozi lakini pale ambapo kundi la vijana linageuka kuwa mashabiki badala ya walinzi, misingi hiyo taifa na misingi imara ya demokrasia huanguka taratibu. “Viongozi wanajua wakifanya kosa, watatetewa. Wapinzani wakisema ukweli, watashambuliwa...
Back
Top Bottom