Recent content by OCC Doctors

  1. OCC Doctors

    Kuyeyuka na kupotea kwa Mimba

    Kifuko cha ujauzito baada ya mimba kutunga (gestational sac) ni muundo uliojaa maji unaozunguka kiinitete (embryo) wakati wa wiki chache za ukuaji wa kiinitete. Tatizo la Kuyeyuka kwa mimba 'Blighted ovum' hutokea pale ambapo kifuko cha ujauzito (gestational sac) kinakua bila kiinitete...
  2. OCC Doctors

    Sababu inayopelekea Mbegu za uzazi kuchanganyika na damu

    Sababu zinazopelekea mwanaume kutoa mbegu ambazo zimechanganyika na damu (hematospermia). Sababu inayojulikana zaidi ni kutokana na uchunguzi wa tezi dume (Prostate biopsy) ambapo inahusisha kuondolewa kwa sampuli ndogo za tishu ili kuchunguza saratani ya tezi dumu. Sababu zisizo za kawaida ni...
  3. OCC Doctors

    Rangi ya Choo kubwa na utambuzi wake kiafya

    Kinyesi cha kawaida huwa na rangi ya hudhurungi (brownish) kutokana na kuwepo kwa kemikali ya 'stercobilinogen' kwenye utumbo. Kinyesi cha watoto wachanga huonekana kahawia-njano au kijani-njano. Kinyesi Kisicho na rangi (Pale coloured stool) ni kwa sababu ya kukosekana kwa 'stercobilinogen'...
  4. OCC Doctors

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya

    Ngedere hufugwa, ikiwa utamfuga mtu basi tambua yatakayokukuta baadae, lakini ikiwa utaishi na kumuweka kama binaadamu basi kuna faida baadae. Kumbuka ungedere unaujenga wewe na ubinaadamu pia unaujenga wewe, mwanamke ni mtu wa hisia ni lazima ucheze vizuri na hisia zake.
  5. OCC Doctors

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya

    Inatagemea ulimkuta nayo au aliyapata kwako, ikiwa ulimkuta nayo basi ataendelea kujiweka hivyo kwasababu hayo ndio yaliyokuvutia wewe, lakini kama hukumkuta nayo kamwe hawezi kujiweka hivyo kwasababu hayo sio haiba yako.
  6. OCC Doctors

    Vipuli vya Sikio la kati

    Ooh sawa sawa. Ahsante sana.
  7. OCC Doctors

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya

    Kucha feki ni kwa ajili ya kukuvutia wewe mume wake, Kupoteza hamu ya tendo la ndoa, ni shida ya kitabibu inayofahamika kitaalam kama (Hypoactive sexual desire disorder (HSDD), pia hufahamika kama kupoteza hisia ya tendo (Loss of libido) ndio janga kubwa linalo wakumba wanawake walio wengi...
  8. OCC Doctors

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya

    Usiende nayo haraka, mpe wazo la vikao kisha apendekeze yeye usikie mtazamo wake.
  9. OCC Doctors

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya

    Ni kwasababu hamkai na kuongea ndio maana wamekamatwa akili na mambo mengine. Huko kwenye vikoba wanakaa na kuongea wanapata nafasi ya kutoa vifundo vyao. Na huko ndiko unapomalizwa
  10. OCC Doctors

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya

    Ni ngumu kugombana na mtu ambaye ameshakueleza madhaifu yake, unaweza kumuadhibu mtu lakini kumbe ni hali ya kutopata nafasi kujieleza vizuri. Mtu anapojieleza unaweza kupata takwimu yake ya kufikiri na akili yake inapoelekea na hapo sasa unapata njia ya uishi nae vipi na kwa mrengo upi.
  11. OCC Doctors

    Vipuli vya Sikio la kati

    Kwanini mada hizo zinapendwa?
  12. OCC Doctors

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya

    Wengi wanataka kulinda ndoa zao, lakini hawajui njia halisi ya kufanya. Hili hapa Suluhisho la kisaikolojia na Afya ya akili katika mahusiano: Msisubiri magomvi ndio muweke vikao vya ndoa, kila ndoa ina misukosuko na migogoro ambayo ni mikubwa, midogo au ya wastani. Vikao vya Mke na Mume...
  13. OCC Doctors

    Vipuli vya Sikio la kati

    Sikio la binaadamu limegawika sehemu kuu tatu, sehemu ya nje, sehemu ya kati na sehemu ya ndani. Uzi huu unahusu mchakato wa kusafirisha mitetemo ya hewa sehemu ya kati ya sikio kwenda sehemu ya ndani ya sikio.
  14. OCC Doctors

    Vipuli vya Sikio la kati

    Kwenye sikio la kati kuna vipuli vitatu (ossicles) ambavyo hupitisha mitetemo ya hewa kutoka sikio la nje hadi sikio la ndani ili kuchakatwa kama sauti. Kipuli cha kwanza ni 'Malleus' mfupa mdogo wa umbo la nyundo husambaza mitetemo ya sauti hadi kwenye kipuli cha pili kiitwacho 'Incus', ni...
Back
Top Bottom