Recent content by mutashambala

  1. M

    Nahitaji kukodi Suzuki Carry

    Samahani nilikuwa na maana ya kazi inayozidi uwezo wa gari.
  2. M

    Nahitaji kukodi Suzuki Carry

    Si vema kukodisha gari kwa mkataba wa kazi inayozidi uwezo wa kazi. Gari inaweza kuhitaji kubadilisha injini baada ya kazi hiyo.
  3. M

    Nahitaji kukodi Suzuki Carry

    Nguvu ya injini ya kirikuu ni cc 660. Kama unataka kubeba watu kumi bila kumuingiza hasara mwenye gari, tafuta noah kama barabara ni zuri. Kama barabara ni mbaya, tafuta toyota hilux.
  4. M

    Nahitaji kukodi Suzuki Carry

    Sawa inabebeshwa lakini matokeo yake injini yake inachoka mapema. Kwa kazi ya kubeba watu wa Mbeya ambao wameshiba, inatakiwa asibebe zaidi ya watu 5.
  5. M

    Nahitaji kukodi Suzuki Carry

    Je itakuwa inabeba watu wangapi? Bado najiuliza kwa nini ukodi pick up kwa ajili ya kubeba watu. Mimi ninayo lakini nahitaji majibu ya maswali hayo kabla ya kuamua kukukodisha.
  6. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Uzi huu ni kwa ajili ya waliiomba certificate na diploma
  7. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Sasa nimejua tatizo lako. Baada ya kufungua, ulitakiwa uwe unachungulia. Kwa sifa ulizonazo, utakuwa ulichaguliwa NACTE wakasubiri uthibitishe kwenye profile yako haukuthibitisha, hivyo nafasi yako watapewa waliiomba safari ya pili. Nashauri utumie namba za simu ulizopewa, uwapigie NACTE.
  8. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Naona kama haueleweki vizuri. Ni bora kuwa wazi ili wanaojua wakufahamishe. Nilikuuliza kama uliomba NACTE kwa kutumia CAS ukasema ndiyo ulitumia. Wakati huo unaomba msaada jinsi ya kutumia. Sasa ulitumiaji kuomba wakati hujui.
  9. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Wote walioomba kwa kutumia CAS, kila mtu kwa sasa anaelewa hatma yake. Kama hauelewi, maana yake ni kwamba haujui jinsi ya kuitumia. Itabidi usubiri mwaka kesho.
  10. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Kwani wakati wa kuomba hukutumia Central Admission System?
  11. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Kama uliishaconfirm, profile yako haina kazi tena wala huhitaji kuifungua tena.
  12. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Taarifa kwa wote mliokwishaconfirm ni kwamba hamna tena haja ya kuingia kwenye profile zenu maana kazi yake imekwisha. Sasa mnatakiwa kuwa mnachungulia e-mail ili kuona kama joining instructions zimetumwa. Wale mliochagua mara ya pili, endeleeni kuchungulia profile zenu.
  13. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Hapo nimemuelewa. Kama aliishaconfirm ikaandika yes, sasa kwenye profile anatafuta nini tena? Kazi yake kwenye CAS imeisha sasa awe anachungulia kwenye email yake maana atatumiwa joining instructions ya chuo alichochaguliwa.
  14. M

    Ni lini post za Vyuo vya Afya zitatoka kwa mwaka 2015?

    Hapo hakuna makosa mkuu. Ulitakiwa kufanya uchaguzi upya kwa kuzingatia vyuo vya private ambavyo bado vina nafasi.
Back
Top Bottom