Kwa hiyo kosa hapa ni Mh. Mbowe na Mwigulu kuwaona wako pamoja kwenye Train ila ingekuwa kwenye Ndege fresh tu au vipi? Lakini pia SGR ni usafiri wa umma unaweza ukakata tiketi ukajikuta jirani yako ni Ex wako
Iwapo utanihakikishia kuwa hao maaskofu wengine walipewa mwaliko wa kuwepo na wakagoma kuja nitakuelewa point yako vinginevyo nachukulia kama ni maoni yako tu!
Una uhakika hao maaskofu wengine walialikwa??? Kumbuka pia shughuli ilikuwa ya KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo Askofu Malasusa ndio Mkuu wake. Hivyo hakuwa pale kama Mkuu wa Kanisa KKKT
Upo sahihi Mkuu! Inawezekana alikuwa anamaanisha hao wanaotoka Kayumba wapo wengi UDSM bila kujali wanasomea Fani gani! Lakini ukweli ni kwamba kwa zile fani ambazo zina ushindani mkubwa kuzipata na asilimia kubwa na wanaochaguliwa kusoma fani hizo wanatoka Private schools
Hakuna haja ya kupita dirishani Mkuu! Kama umedownload tiketi yenye QR code kwenye simu yako unaenda kuiscan tu pale kwenye geti la kuingilia unatinga ndani ya mchuma!
Deni tunalodaiwa ni Tsh. 8,695,000/= Ili turuhusiwe kuitoa maiti mochwari. Tumelia sana lakini wanataka tutafute 3,000,000/= kama advance kwa sasa ili watupatie mwili kwenda kuzika.
Wametuambia pia tuache kadi ya NIDA ya baba wa mtoto (marehemu). Balance itakayobaki tumeambiwa tutalipa...
Naheshimu maoni yako lakini naona ugumu katika utekelezaji wake. Huyu inaonekana ni rahisi kufuta deni kwa kuwa alikuwa hajalipa. Vipi kwa ambaye anakuwa kishalipa na hadaiwi chochote ikatokea bahati mbaya akafariki, na huyo unapendekeza nndugu zake warejeshewe hela waliyolipa au wampotezee? Ila...
Nadhani anachodaiwa sio gharama za 'kukomboa maiti' kama unavyodai ila ni gharama za matibabu alizopata akiwa anatibiwa. Kama unaona hastahili kudaiwa basi ata wagonjwa wanaokuwa wamelipa gharama za matibabu na ikatokea wakafariki basi nao ungependekeza wawe wanarudishiwa pesa wanazolipa...
Hisa za TBL gani ambazo rafiki yako anakosa mteja? Watu Juzi tu tumekula gawio la maana la TBL. Kama rafiki yako bado anatafuta mteja wa hisa zake za TBL naomba uniunganishe nae tufanye biashara.
Yaani maelezo yote haya unayoelezea malalamiko kibao na bado umeshidwa ata kutaja jina la hiyo shule (English medium) ambayo wamekataa kuwahamisha wanao!!! Sasa unaomba msaada upi wakati unashiriki kumficha mtuhumiwa wako? Mie naona hii ni story kama story nyingine tu ila story hii imekosa mtu...
Nadhani kabla haujasema NECTA imedanganya ungejaribu kujumlisha idadi ya hao waliofail kuona kama inafanana na idadi iliyotangazwa na NECTA au hapana. Vinginevyo na utakuwa ni mpiga kelele tu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.