Recent content by lebabu11

  1. L

    Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

    Kumbukumbu ya fikra, matendo na sera haizikwi na marehemu, na hiyo ndiyo iliyoshindanishwa.
  2. L

    Ujamaa ni sababu mojawapo kubwa ya umasikini na uharibifu wa nchi nyingi za Afrika

    Wizi ni tabia mbaya na haikubaliki popote. Hata hivyo, nafikiri maendeleo yanakosekana kwa sababu ya ujnga zaidi. Mwizi hujimilikisha visivyo vyake na kuwa tajiri, kwa hiyo waafrika ni wajinga wanaoruhusu wageni (wezi) kuiba raslimali zao.
  3. L

    Yanayoendelea ndani ya uongozi wa CCM na serikali yanatafakarisha

    Siku zote chama kinatakiwa kuwa na wananchi ili wakiunge mkono. Kwa kuwashawishi wananchi, chama chaweza kubadilisha team yake serikalini kutokana na hoja za wananchi. Hata hivyo, kwa sababu ya siasa za uchawa wa kutafuta teuzi, chama tawala, watumishi wa serikali na vyombo vya dola huimba...
  4. L

    Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

    Songas mkataba unaisha lini? Kuna maandlizi yoyote ya serikali kupokea miundombinu na mitambo?
  5. L

    Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

    Uchumi wa nchi za Afrika, ukiondoa Afrika Kusini na zile za Kiarabu (kaskazini) umeshikwa na magabacholi kwa asilimia kubwa. Serikali na taasisi za kidola hufikiria na kuelekeza nguvu nyingi kulinda viongozi huku wakisahau umiliki wa uchumi na teknolojia. Rushwa kubwa hutokea kwenye sekta za...
  6. L

    Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

    Kuna tofauti kubwa sana kati ya nadharia na vitendo kwa nchi masikini kwa sababu ya ukosefu wa maarifa ya kuunganisha.
  7. L

    Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

    Kunapokuwa na vacuum uchafu unaweza kuingia. Ni muhimu kutoa taarifa sahihi kwa wakati sahihi kunapokuwa na jambo lisiloeleweka, hasa linalohusu usalama wa raia (uhai/maisha). Kama walipotosha baada ya taarifa sahihi kutolewa hapo kuna uzito, vinginevyo wapewe onyo na maelekezo ya kutulia...
  8. L

    Hii ndio hali ya Bumbuli ambayo Mbunge wake ni Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi

    Ukisoma vizuri, kwa kutulia utaona nimeandika kwamba mbunge hupeleka taarifa ili serikali ikatatue, hata barabara nimetaja.
  9. L

    Hii ndio hali ya Bumbuli ambayo Mbunge wake ni Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi

    Maendeleo ya eneo lolote hufanywa na wakazi husika kutokana na fikra na vitendo vyao katika shughuli za kiuchumi (mbunge ni mwananchi anayewakilisha maoni na kero zao bungeni, ili serikali ipate taarifa ikatatue, hasa kwa zile huduma muhimu kama elimu, afya, barabara, maji, ....). Hata hivyo...
  10. L

    IMF: Tanzania ni moja ya nchi 10 vinara zenye uchumi mkubwa zaidi Barani Afrika kwa mwaka 2024

    Uchumi waweza kuwa mkubwa ukiwa mikononi mwa wageni. Hii ni changamoto pia ambayo ni kazi ya TISS kufanya uchunguzi na kushauri vitendo vya marekebisho kwenye Sera na uendeshaji wa siku kwa siku wa serikali na dola (uchumi waweza kuwa mkubwa kinadharia kwa wananchi).
  11. L

    TAKUKURU Wala rushwa Serikalini ni wengi lakini wao wanahangaika na Mawakala

    Hii ipo kiwizi wizi na ni kazi ya polisi zaidi, labda takukuru walifanya baada ya kuambiwa polisi wamekula rushwa na kutochukua hatua (maelezo haysjitoshelezi) .
  12. L

    Mbunge Mohamed Issa: Wanaotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar wawe na Passport

    Huyo anatakiwa aelimishwe tu kwamba Wazanzibari wanaitegemea Tanganyika kuliko watanganyika wanavyoitegemea Zanzibar. Pili, siyo rahisi kurudi nyuma tena kwenye uwepo wa nchi mbili, Tanzania ni ya wote kuanzia bara hadi visiwani (fikra kama zake hazina nafasi tena katika zama hizi). Yeye...
  13. L

    Mbowe, wenye akili wamekuelewa. Hawa wasiokuelewa tuwaite nani?

    Hoja zenye mantiki lazima tuzikubali bila kujali katoa nani. Hii itakuwa kwa maslahi mapana ya ujenzi wa jamii na taifa kwa ujumla. Vyama viache Siasa za kipumbavu na hoja za kijuha hazisaidii kizazi hiki na kinadidimiza fikra na ni uangamivu kwa vizazi vijavyo. Siasa lazima zijengwe katika...
  14. L

    Benki ya Dunia yasitisha kufadhili mradi wa REGROW. Mradi huo unahusishwa na ukiukaji wa Haki za Binadamu nchini Tanzania

    Makadirio hafifu ndiyo uthibitisho wa kutojali au kutothamini utu wa wakazi hao. Vinginevyo ithibitishwe kwamba waliofanya makadirio hayo ni wajinga, hivyo wafundishwe au waondoshwe katika utekelezaji wa zoezi hilo au mengine yafananayo.
  15. L

    Idadi ya Wanawake Wanaomiliki Ardhi Nchini Imeongezeka Kutoka Asilimia 25 Hadi Asilimia 41

    Mwanamke hajawahi kuzuiwa kununua ardhi na kupata umiliki wa kisheria. Changamoto ipo kwenye urithi wa ardhi kimila. Wazee wa mila walikuwa na akili za kulinda jamii kuliko Sisi wa kizazi hiki (wao walitumia akili za kuzaliwa yaani common sense), wakati sisi tunakariri yanayofundishwa, zaidi...
Back
Top Bottom