Lakini kumbuka kwamba sisi Africa tunaweza kuishi bila kwenda au kuchukua kitu chochote cha Amerika tukaishi. Lakini Wao Amerika hawawezi kuishi bila kuja Africa au kujisogeza karibu na madini yetu wakaishi kwa furaha. They need us more than we need them. Angalia mfano wa Rais wa Burkinafaso...
Wengi walisahau kuuliza na kuelewa zile zinazoitwa AWAMU. Ilivyoitwa tu awamu ya 6 wenye kubisha hapo wangebisha ili ibaki kuitwa awamu ya 5. Ikishabadirika tu kutoka awamu ya 5 kwenda awamu ya 6, Mgombea kipindi cha PILI hawezi kuwa na wagombea wengine kwenye ulingo maana anamalizia awamu yake...
Sio mbaya kama ajira za watanzania zinapatikana . shida nayoiona ni kwasababu gani sasa tusichimbe Chuma ili tuache kuagiza chuma maana kazi ya ujenzi wa SGR bado inahitajika reli iende mpaka Burundi, DRC na kwingine Africa na Mashariki. Kiwanda kianze na wanufaika walipe kodi basi sote...
Umenikumbusha case za Mh.Trump kule Amerika alizokuwa nazo kabla ya uchaguzi lakini hakukata tamaa bali alienda nao hivyo hivyo na kwasasa ndie Rais wa nchi.
Kwa mwenye uwezo wa kuona beyond the Box, hii kesi baada ya uchaguzi kupita ni kama haitakuwepo. Shida ni Mh.Lissu anakazana atoke kabla ya uchaguzi na wanajua kwamba yeye Lissu hataki uchaguzi ufanyike bila reforms na aliahidi kukinukisha na hilo hawalitaki litokee.
MKuu hii hoja yako haiwezi kuwa sawa. Nakumbuka kama machine moja wapo ya zile Tisa isingewashwa, tungekuwa kwenye mgao wa umeme wa hatari. Fanya uchunguzi tena utwambie kama kweli hatupati umeme wowote kutoka Bwawa la Nyerere
Kwa hatua Tanzania ilipofikia, sitamani kuhamia au kuzamia Merikani au Ulaya. tutabanana hapa hapa maana maendeleo sasa tunayaona vizuri (visible Devt)
Wana JF, nilikua najaribu kuwaza, hivi kama Tz inazalisha umeme lakini hauna manufaa kuupeleka Kasikazini kwasababu ni mbali na kuamua kununua wa Ethopia, Je umeme tunaotaka kuwauzia majirani zetu kama Zambia, Malawi, Kenya na wengine utafikaje huko?
Nisaidieni kupata majibu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.