Recent content by Doslamari

  1. D

    DOKEZO TANROADS mkoa wa Arusha wekeni matuta pale shule ya msingi Kimandafu na njia ya ng'ombe au mnasubiri maafa makubwa yatokee

    Shule ya Msingi Kimandafu ipo kati ya Maroroni na Kikatiti. Ukitokea Maroroni, eneo hilo ni mteremko wenye kivuko cha watoto chenye alama za pundamilia, lakini madereva wengi hawazingatii. Leo asubuhi, mwanafunzi alinusurika kugongwa na gari ndogo iliyokuwa ikitokea Maroroni. Pale eneo la...
  2. D

    Hii nchi imegawanywa kuanzia kipindi cha Magu, Samia anaendeleza dhambi hiyo kuhusu ujenzi wa miundo mbinu

    Ndugu zangu watanzania wenzangu nchi hii si moja, hakuna usawa ktk ujenzi wa miundo mbinu. Mwezi wa 8 nilisafiri kutokea Arusha kwenda Dodoma kupitia Kiteto. Kiteto ni wilaya ndani ya mkoa wa Manyara. Ukitokea Arusha unapitia mji wa Orkesumet ambao ni makao makuu ya wilaya ya Simanjiro. Hilo...
  3. D

    Hizi bei za nyama kupandishwa kiholela nani wa kuwasaidia Wananchi? Sasa hivi kilo TZS 12,000/ Bodi ya nyama kazi yake nini?

    Siku hizi kuna umoja wa kila sekta, pale Arusha kuna umoja wa wauza nyama, wanakubaliana kupanga bei wanavyotaka na ole wako uuse chini ya hiyo bei. Sasa hivi kila butcher Arusha kilo moja ni TZS 12,000/. Hakuna mamlaka au chombo cha kudhibiti huu upandishaji holela? Mlinzi wa mwananchi ni...
  4. D

    Wairaqw(Wambulu) mmepuuzwa na Rais Samia: Iweje mpaka leo mko kwenye barabara za vumbi?

    Kosa la hawa ndugu zetu wambulu ni nini kwa serikali hii ya CCM? Mji wa Mbulu ndio origin ya wairaqw(Wambulu). Mwaka 2022 ulianzishwa ujenzi wa barabara ya lami Km 25 tu kutoka Mbulu mjini na kuishia kijiji kinaitwa Garbabi, ila kwa masikitiko mkandarasi ameondoka serikali imeiteleleza huo...
  5. D

    TCRA Polisi wako wapi watu wanaibiwa kupitia hii mikopo mtandaoni? Jerry Silaa msaidie Rais

    Kuna wimbi kubwa sana la matapeli likitumia majina ya watu maarufu km Mohamed Dewji(MO), Tulia Ackson, Jokate Mwegelo n.k. Hawa watu ni matapeli na wana mtandao mkubwa, unakuta kwenye comments wanashukuru kuwa wamepata mikopo kumbe ulaghai ili uiingie mkenge. Namna ya kukuingiza mkenge...
  6. D

    Serikali kinashindikana nini kujenga upya na njia 4 kutoka uwanja wa ndege Arusha kwenda mjini?

    Barabara kutoka pale bypass ya East Africa ni ya zamani sana, ni nyembamba, imejaa mashimo, viraka, ukiipata ni sawa tu na njia ya kwenda Kiteto. Barabara hiyo inatumiwa na watalii hasa wazungu, uwanja wa ndege Arusha una miruko(flights) zaidi ya 150 kwa siku, ni aibu kwa nchi. Kwanini...
  7. D

    TANESCO lini watakuwa na akili? Unalipa kuunganishiwa tangia jana mpk sahz hakuna ht uthibitisho wa malipo

    Nilijisajili kuunganishiwa umeme ikiwa ni kuletewa nguzo 2. Nikatumiwa control number ya malipo baada ya kufanya survey kuwa nitume Tsh 697,000/=. Mpaka muda huu ujumbe ni ule wa mwanzo tu kuwa malipo yako yanashughulikiwa na utapokea ujumbe mfupi kuthibitisha malipo yako. Siku ya 2 hakuna...
  8. D

    Zile barabara 8 zilizosainiwa tarehe 16.06.2023 kwa mbwembwe ziko wapi?

    Tarehe 16.06.2023 zilisainiwa barabara 8 zaidi ya Km 2200 nchi nzima, ila mpaka leo hii hakuna ht moja iliyoanza kujengwa. Ile ilikuwa ghilba? Walikuwa wanamdanganya nani, kwa faida ya nani. Tunaona Rais yuko bize na Kizimkazi, ni Rais yupi anafuatilia utekelezaji wa ujenzi wa ile mikataba...
  9. D

    Kwa haya anayoyafanya Samia kijijini Kizimkazi hayana tofauti na aliyokuwa akifanya Magufuli Chato

    Kwanza yeye ni Rais wa JMT kila mara yuko Zanzibar kuzindua miradi. Kijiji kidogo hicho mapesa yote ndani ya miaka 3 hela ililipelekwa pale ni nyingi sana. Hii ni kwanza ni aibu na kashfa kwa Rais wa nchi nzima. Tabia hii alianza Magufuli, kabla ya hapo huu ubaguzi usio na haya haukuwepo...
  10. D

    Ahsante Rais kuwarudisha Palamagamba Kabudi na William Lukuvi: Luhaga Mpina ana la kujifunza

    Ahsante Rais wetu kumteua Kabudi, Kabudi ni miongoni mwa binadamu wenye akili sana, watanzania wenye akili kubwa ni pamoja na Sospeter Muhongo, Kitila Mkumbo, Palagamamba Kabudi, William Lukuvi. Hawana makuu ni watulivu, utapenda wakichangia. Hongera Rais tumefurahi wananchi wako.
  11. D

    Ahsante ahsante Rais wetu, ahsante Doroth Gwajima; tunajivunia serikali yetu

    Jana nilitoa taarifa ya ukatili kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Kitefu mkoa wa Arusha. Najivunia serikali yangu mmechukua hatua, mbarrikiwe. Ila huyu mwalimu mkuu mumchunguze anatafuta aliyetoa taarifa. Hongera Max, hongera waziri, hongera mh. Rais wetu, haki itendeke
  12. D

    DOKEZO Waziri Gwajima chukua hatua kwa ukatili huu aliofanywa mtoto shule ya Msingi Kitefu, Halmashauri ya Meru

    Shule ya msingi Kitefu iko Halmashauri ya Wilaya Meru mkoa wa Arusha. Kuna mtoto amefanyiwa ukatili na anadaiwa ni baba yake kwa kumchoma na nyaya za umeme, huyu bwana alikuwepo leo shuleni baada ya kuitwa na Mwalimu Mkuu Mdee. Kinachokatisha tamaa ni kwamba badala ya huyu bwana kujutia kitendo...
  13. D

    KERO Waziri Biteko, kwanini nguzo moja ya umeme ilipiwe Tsh 515,000/ wakati ni mali ya shirika? Huu unyanyasaji mpaka lini?

    Wakati unataka kuunganishiwa huduma ya umeme kama nyumba iko mbali kila nguzo moja ni sh. 515,000/, nguzo ni mali ya shirika, mwananchi ni mteja wa huduma ya umeme kwanini alipie nguzo? Huu ni uonevu mkubwa sana. Kwanini mwananchi anunue kitu ambacho si mali yake? Mlitegemea bila nguzo...
  14. D

    Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko huu mgao wa umeme Arusha ni wa nini?

    Sahivi kila siku kuanzia saa 12 jioni umeme unakatwa huku Arusha wilayani Arumeru, kurudi saa 5 usiku, huu ni mgao? Kwanini msitangaze? Huu mgao upo na maeneo mengine ya nchi? Shida Biteko baada ya kuwa naibu waziri mkuu naona muda mwingi yuko kwenye uzinduzi wa shughuli mbalimbali...
  15. D

    Haya matamasha ya kikabila ni janga la Taifa: sasa hivi Wanyakyusa wako ITV

    Hivi vinavyoitwa matamasha ya kikabila yanayojitokeza kwa kasi siku hizi havina afya ktk kujenga umoja wa kitaifa. Kuna ajenda gani imejificha humu? Walianza wasukuma, halafu wanaigana utafikiri sifa kumbe ni janga. Karne hii watu mnatukuza ukabila? Mnaunda vikundi vinavyohamasisha ubaguzi...
Back
Top Bottom