Muda unazidi kwenda saa sita hii na mpaka sasa sijafanikiwa kupata chochote. Mimi na mama yao tunaweza vumilia huku nikipambana ila kwa watoto ni mateso makubwa sana, nimetoka nyumbani hakuna kitu chochote yaani pako empty. Eeeh Mungu tenda miujiza yako nipate riziki nipate nguvu ya kuendelea...
Nafight sana though sometimes mambo yanakuwa hayaendi kama hivi kichwa knapata moto mkuu wanangu bado wadogo. Can you imagine bro mpak kula inakuwa mtihani. Mpaka nafikia hatua ya kuanzisha uzi ili nipate msaada. Nafight mkuu. Shukran sana
Mkuu maisha popote na mwanaume ni kupambana bado sijakata tamaa mkuu nitakutafuta mkuu ili niipate hiyo connection. Wacha kwa leo mkuu nipambanie ugali wa watoto mkuu. Shukran sana
Mkuu haina haja ya kusema samahani nashukuru kwa hili pia nilishafanya tuition japo haikiwa na mafanikio, mazingira niliyopo muamko wa elimu ni mdogo sana nilipata watoto watatu ambao nilikuwa ninawafundisha na ukizingatia masomo niliyochukuwa si yenye uhitaji sana wa tuition kwa ngazi ya o level.
Mpaka nimefikia hatua hii ya kuandika uzi huu ni kwamba nimekwama sina jinsi siwezi kukopa kwani sina uhakika wa kulipa pesa nahitaji wanangu na mama yao wapate kula. Kazi kupata ni ngumu na vibarua vimekuwa mtihani. Kwa atakaewsza nisaidia naomba tuwasiliane Pm. I really need your help.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.