Rose Nungu (Munalove), akubali kupeleka msiba nyumbani kwa baba wa Patrick

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
IMG_20180705_182704.jpg

Kwa ufupi
Jana Julai 4, 2018 Muna kupitia ukusara wa mtandao wa kijamii wa Instagram liandika baba wa mtoto ni Casto Dickson

Dar es Salaam. Kufuatia sintofahamu kuhusu nani ni baba halisi wa mtoto wa Muna, Patrick na wapi msiba upelekwe hatimaye Muna amekubali msiba upelekwe kwa baba wa mtoto huyo, Peter Zacharia Komu, maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Jana Julai 4, 2018 Muna kupitia ukusara wa mtandao wa kijamii wa Instagram liandika baba wa mtoto ni Casto Dickson, huku akisisitiza msiba utafanyika nyumbani kwake Mbezi, huku akimtaka Peter aache kuongea maneno kwani anasiri nzito moyoni.

Akizungumza kwa njia ya simu na MCL Digital leo Alhamisi Juni 5, 2018 Muna amesema alipitiwa na shetani hadi kufikia hatua ya kusema msiba ufanyikie nyumbani kwake Mbezi na kuandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa Peter siyo baba wa Patrick.

"Najua nimekosea ndio maana posti yangu nimeifuta niliyoiandika jana kuwa mtoto sio wa Peter, shetani alinipitia, hivyo msiba utakuwa Mwananyamala kwa Peter na sio Mbezi kama nilivyosema hapo mwanzo,"amesema Muna.

Hata hivyo, MCL Digital imezungumza na dada yake Muna, Eve na kusema ni kweli Muna amekubali msiba uwe nyumbani kwa Peter, sababu ndiyo baba halali wa Patrick.

"Tunamshukuru Mungu tena sana, kweli Muna amekubali msiba uwe Mwananyamala kwa mume wake, na hivi wako ubalozini wanafanya mchakato wa kuuleta mwili kesho Tanzania.” Amesema.

“Amezungumza na mama na kumuomba msamaha kuwa shetani alimpitia hivyo asamehewe, yaani siku ya leo mama ameonekana kuchangamka kuliko hali aliyokuwa nayo jana,”amesema Eve.

Patrick alifariki dunia Julai 3, 2018 Nairobi, Kenya alikukuwa akipatiwa matibabu ya kichwa, yaliyosababisha uvimbe kichwani.

Mwili wake unatarajia kuletwa Tanzania kesho Julai 6, 2018 na maziko yatakuwa Jumamosi.

Habari zaidi, soma=> Sakata la Mtoto wa Muna Linaumiza Sana Moyo
 
View attachment 803207
Kwa ufupi
Jana Julai 4, 2018 Muna kupitia ukusara wa mtandao wa kijamii wa Instagram liandika baba wa mtoto ni Casto Dickson

By Rhobi Chacha, Mwananchi rchacha@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Kufuatia sintofahamu kuhusu nani ni baba halisi wa mtoto wa Muna, Patrick na wapi msiba upelekwe hatimaye Muna amekubali msiba upelekwe kwa baba wa mtoto huyo, Peter Zacharia Komu, maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Jana Julai 4, 2018 Muna kupitia ukusara wa mtandao wa kijamii wa Instagram liandika baba wa mtoto ni Casto Dickson, huku akisisitiza msiba utafanyika nyumbani kwake Mbezi, huku akimtaka Peter aache kuongea maneno kwani anasiri nzito moyoni.

Akizungumza kwa njia ya simu na MCL Digital leo Alhamisi Juni 5, 2018 Muna amesema alipitiwa na shetani hadi kufikia hatua ya kusema msiba ufanyikie nyumbani kwake Mbezi na kuandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa Peter siyo baba wa Patrick.

"Najua nimekosea ndio maana posti yangu nimeifuta niliyoiandika jana kuwa mtoto sio wa Peter, shetani alinipitia, hivyo msiba utakuwa Mwananyamala kwa Peter na sio Mbezi kama nilivyosema hapo mwanzo,"amesema Muna.

Hata hivyo, MCL Digital imezungumza na dada yake Muna, Eve na kusema ni kweli Muna amekubali msiba uwe nyumbani kwa Peter, sababu ndiyo baba halali wa Patrick.

"Tunamshukuru Mungu tena sana, kweli Muna amekubali msiba uwe Mwananyamala kwa mume wake, na hivi wako ubalozini wanafanya mchakato wa kuuleta mwili kesho Tanzania.” Amesema.

“Amezungumza na mama na kumuomba msamaha kuwa shetani alimpitia hivyo asamehewe, yaani siku ya leo mama ameonekana kuchangamka kuliko hali aliyokuwa nayo jana,”amesema Eve.

Patrick alifariki dunia Julai 3, 2018 Nairobi, Kenya alikukuwa akipatiwa matibabu ya kichwa, yaliyosababisha uvimbe kichwani.

Mwili wake unatarajia kuletwa Tanzania kesho Julai 6, 2018 na maziko yatakuwa Jumamosi.

Habari zaidi, soma=> Sakata la Mtoto wa Muna Linaumiza Sana Moyo
Mama naye kama kalaaniwa vile.
R.i.p kwa dogo.
 
Ana bahati nzuri sana huyu Muna lasivyo huyo mtoto angezikwa mwezi ujao maana baba wa mtoto asingekubali ujinga huo....wa kutapeliwa...
Bora amechukua ushauri wa DEMBA
Sijui huyo Casto ana jisikia Vipi huko daaaa
Nilikuwa najiuliza na kuumiza kichwa kila siku....

Huyu Casto kabeba laana gani.!??

Now I know.
 
Back
Top Bottom