Zitto: Tumemtoa Mghwira ili kuondoa dhana kwamba ACT ni "CCM B", asema utaratibu ufatwe kwenye teuzi

kwa asilimia kubwa vyama vinavyoshirikiana huwa tayari vimekubaliana kabla ya kushika dola. Halafu nchi nyingine mambo ya coalition government uwekwa kwenye katiba za nchi. Tuna mfano mzuri pia hapa nyumbani kwa upande wa Zanzibar kutokana na mazingira ya Zenj.

Halafu Chancellor Angela Mekhail wa Ujerumani kwa nini alimchagua mpinzani? Katiba ya Ujerumani unasemaje juu ya hilo?

Kwa mujibu wa ideal democracy, vyama vya siasa vinatakiwa kuwa independent and competitive period.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Zitto ameongea vizuri,

Suala la utamaduni Na bla bla halina maana
Akiri tu kweli kuwa Chama kimeumia, maana yalipoanza ya Kitila Baraka Sana walimtetea, haya mama huyoo amechupa na u arasii
 
Boss Evans-Arsenal Nawaza kimya kimya, ni Intelligence imeona hili au amesoma Upepo.

My Take: WaTanzania wa leo, sio WaTanzania wa Miaka ile ya vita ya Kagera au MajiMaji. WaTanzania wa leo wameamka sana, hasa Mijini. Bado vijijini.

Mbunge wa kigoma Mh zitto zuberi kabwe ambaye pia ni kiongozi wa ACT wazalendo amesema kwamba wameamua kumuweka pembeni mwenyekiti wao wa zamani Mama Anna Mgirwa ili kutoa dhana kwamba ACT ni CCM B Akihojiwa na mwandishi wa habari amesema hayo

"Sasa tunaweka kanuni ambazo mtu akichaguliwa na uongozi wa juu unaoongozwa na Chama kingine tofauti na ACT basi tufanye kwanza mazungumzo kabla ya mtu kukubali tu bila kutoa taarifa" alisema Mh Zitto Kabwe.

Pia akaongeza kwa kusema kwamba Kwa sasa wameshachagua kaimu mwenyekiti wao wa Chama na anaendelea na majukumu kama kawaida.
 
Lakini Mh Rais baada ya kumuapisha alisema msimamo wake wa kuto kushirikisha wapinzani upo pale pale.
Sasa kwa maana ambayo siyo rasmi ni kwamba ACT ni wana Ccm. Zitto usituhadae.
 
Mbunge wa kigoma Mh zitto zuberi kabwe ambaye pia ni kiongozi wa ACT wazalendo amesema kwamba wameamua kumuweka pembeni mwenyekiti wao wa zamani Mama Anna Mgirwa ili kutoa dhana kwamba ACT ni CCM B Akihojiwa na mwandishi wa habari amesema hayo

"Sasa tunaweka kanuni ambazo mtu akichaguliwa na uongozi wa juu unaoongozwa na Chama kingine tofauti na ACT basi tufanye kwanza mazungumzo kabla ya mtu kukubali tu bila kutoa taarifa" alisema Mh Zitto Kabwe.

Pia akaongeza kwa kusema kwamba Kwa sasa wameshachagua kaimu mwenyekiti wao wa Chama na anaendelea na majukumu kama kawaida.

Wote Anna na Zitto wanyamaze wasidhanie kuwa WAtanzania ni Manyumbu kama Zitto alivyotufanyia. Mambo yako wazi kabisa, hakuna asiyejua kuwa Zitto ni CCM B kwa hali na mali. Isitoshe Zitto na Anna wanajijua kuwa wako kazini, na kwa hili wamefanya kazi nzuri sana wanastahili kupewa shahada ya ushindi wa kutukuka na CCM. Sasa mjadala wa nini? Zitto asimseme Anna kuwa mnafiki pengine cha kumshutumu ni kuwa faster than him. Hapa wakuwavulia kofia ya ushindi ni Chadema, tena Dr Slaa kwa kuwajua mapema na kuwatokomezea huko mbali. Very sad, ila nataka hasa Anna, ajue kuwa usaliti huo aliotufanyia watanzania, ni boriti kubwa sana kwenye maisha yake, hatafanya lolote hata apewa nafasi gani. Poleni sana wananchi wa Kilimanjaro, lakini ninayofuraha kuwa nafasi hiyo haikwenda kwa the so called, 'walewale' kama walivyozoea wenyewe, sasa Rais kama kweli unania na watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi, basi toka pia nje ya wanasiasa, maana yawakina Bashite yamekutosha, bado unadeni la kumpeleka mahali pake, serikalini sio mahali pa kujifunzua ushenzi
 
ZZK amejieleza vizuri kama kiongozi wa chama. Nnachokiona kwa baadhi ya wachangiaji kama wana chuki na ZZK.
Nafasi ya Anna Mghwira ikimtokea yoyote yule kukataa si rahisi ,we ukatae uteuzi wa Rais thubutu. Ila kwa hili nampongeza JPM ameonesha kuamini watu wa kariba tofauti ya chama chake. Hivyo hata mbele ya safari akija Rais mwngne anaweza akapitia mlango huo huo kuchukua watu imara kufanya nao kazi kutoka chama chochote maadam wanafaa maana maendeleo hayana chama ni yetu sote wananchi.
 
Hizi teuzi za Raisi ndani ya Act, hazileti afya kwenye siasa za upinzani Nchi hii.sanasana Magu anazidi kujiwekea wigo wakisiasa.karata anazo Changa sasa Zitachezwa 2020. Kumbuka ndani ya ccm kuna panga lilipita kuna waliofyekwa kwakufukuzwa, uwanachama, kuna wakutumbuliwa vyeo,kuna Idadi kubwa yawajumbe wamepunguzwa kwenye vikao vya maamzi.kundi hili rote linamnyima usingizi.hesabu zake ameanza na Act maana likiangukia huko hatopata zogo lakuakata ngebe, mbele ya wapiga kura walio kata tamaa.kwa upande wa Chadema anajua wataenda wa chache kwa sababu kwanza karibu nafasi zaungozi zimejaa, rakini pia siasa zamapambano wengi hawaziwezi. Tusishangilie sana adui yuko macho, hakuna mwaka ulio kua wabahati kwa upinzani kama 2015. Watu wakiendelea kushikana uchawi utashangaa 2020 hii hapa Mtungi anaweka mpila kati,kadi zote 2, yellow na Red, anazichana Siku y afainal, muamzi anakaa nje ya uwanja, anasubilia dk90 kuona Mshindi bila kujali fujo na faulo zilizo tokea uwanjani.
 
ZZK saa yoyote atateuliwa kwenye nafasi za uongozi! Mzee anaendelea kummulika kama alivyowamulika Kitila na Anna Mgwira!! ACT itabaki inaning'inia kama tambara, na wanachama wake sio wataenda wapi maana watabaki wakiwa kwa sababu familia haina baba wala mama! Too sad..... Chezea kila kitu lakini sio "pesa" aisee. Hata mimi kwa hali ya sasa, nikiitwa napokea cheo na unafiki wangu, maana hakuna namna tena!!
Tuitangaze tu rasmi kwamba hii ni nchi ya wanafiki au unasemaje msnajo?

Unafiki unaigharimu sana nchi hii. Unafiki top bottom, bottom up.

Iko siku Mungu ataleta hukumu kali kwa nchi hii zaidi ya hii ya "kutumbuliwa" na "kulia lia tunaibiwa" wakati ni "Viongozi" wetu ndio walisaini hati(mikataba) za kuridhia tuibiwe.
 
Mbunge wa kigoma Mh zitto zuberi kabwe ambaye pia ni kiongozi wa ACT wazalendo amesema kwamba wameamua kumuweka pembeni mwenyekiti wao wa zamani Mama Anna Mgirwa ili kutoa dhana kwamba ACT ni CCM B Akihojiwa na mwandishi wa habari amesema hayo

"Sasa tunaweka kanuni ambazo mtu akichaguliwa na uongozi wa juu unaoongozwa na Chama kingine tofauti na ACT basi tufanye kwanza mazungumzo kabla ya mtu kukubali tu bila kutoa taarifa" alisema Mh Zitto Kabwe.

Pia akaongeza kwa kusema kwamba Kwa sasa wameshachagua kaimu mwenyekiti wao wa Chama na anaendelea na majukumu kama kawaida.

Chama gani, chama hata kura laki moja hakikufikia! Janja tu kumuondoa ni gheresha, hawa ni wasaliti wa nguvu za mabadiliko.
upload_2017-6-9_6-1-25.jpeg
 
Anatuchezea akili tu hyu jamaa sio wa kumuacha, kumpa sana sapoti ya media sio nzuri ni mlafi & kigeugeu kisimpite
Hana jipya sahv tuachane naye, point za kuokoteza zisizo na mashiko ndo alicho bakiza
 
Mama alishaondoka mwenyewe, mengine ni siasa za kitoto tu, kukubali uteuzi na kupokea Ilani ya CCM ni kukubali kuondoka ACT, waachana ne siasa za kitoto.
 
Kama chama kilimuamini mtu anayeweza kununulika kirahisi hivi,hata bada ya kumtoa, tutajuaje kwamba chama si CCM B?

Kama mlivyojua kuwa CHADEMA siyo CCM C baada ya kupokea masazo ya CCM A na kuyafanya bidhaa adimu na ghali zaidi kwenu.Kwa nini wakifanya wengine kwa manufaa ya wote mnshangaa mkifanya ninyi kwa manufaa yenu mnaona sawa?
 
ndio maana me na chadema yangu tu.maana kipindi zito anaenguliwa M4C. watu walimlaumu mbowe kumbe zito ccm b.leo imeonekana na ninavyojua ubunge atakosa safari hii
Hapo ndiyo kutokuelewa kwenu kunapojitokeza. Hivi Lowasa na Sumaye wametoka lini CCM na kuja CDM? Kama issue ni vyama na si watu basi ninawasiwasi na fikra zenu baadhi ya watu maana vyama ni watu na hao watu ulionao huko ndiyo waliozesha chama cha Mapinduzi. Vinginevyo mnasukjmwa na ukanila wenu na ukanda tuuuuu. CCM ni chama safi kuliko chochote kwa sasa.
 
Kama mlivyojua kuwa CHADEMA siyo CCM C baada ya kupokea masazo ya CCM A na kuyafanya bidhaa adimu na ghali zaidi kwenu.Kwa nini wakifanya wengine kwa manufaa ya wote mnshangaa mkifanya ninyi kwa manufaa yenu mnaona sawa?
Wapi nimejua CHADEMA siyo CCM C?

Unapoandika "mkifanya nyinyi" unamaanisa "nyinyi" kina nani na kwa nini unaniweka mimi kundi hilo?
 
Back
Top Bottom