Zitto: Tumemtoa Mghwira ili kuondoa dhana kwamba ACT ni "CCM B", asema utaratibu ufatwe kwenye teuzi



Mbunge wa Kigoma Mh Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa ACT wazalendo amesema kwamba wameamua kumuweka pembeni mwenyekiti wao wa zamani Mama Anna Mghirwa ili kutoa dhana kwamba ACT ni CCM B.

"Sasa tunaweka kanuni ambazo mtu akichaguliwa na uongozi wa juu unaoongozwa na Chama kingine tofauti na ACT basi tufanye kwanza mazungumzo kabla ya mtu kukubali tu bila kutoa taarifa" alisema Mh Zitto Kabwe.

Pia akaongeza kwa kusema kwamba kwa sasa wameshachagua kaimu mwenyekiti wao wa Chama na anaendelea na majukumu kama kawaida.

Haitofautiani sana na ile dhana ya kofia mbili kule ccm
NB
ACT haina tofauti sana na jumuiya ya wazazi, UWT, UVCCM na nyingonezo zote baba ni mmoja
 
Tamaa mbaya sana, namshauri rais magufuli ampe zitto uwaziri wa nishati na madini tuone kama atakataa
 
Zito kanifurahisha, yuko UK anawaombea kura Labour mitaa ya Julius Nyerere, huku kwake mmmmh!
 
Uteuzi kabla ya kutangazwa ni siri na lickage yoyote means nullify, sasa majadiliano na mteuliwa yatafanyika lini! Zitto duh! Najuta kukufahamu.
 
Kati ya wanasiasa ambao wanaipandikiza kansa demokrasia nchini mwetu Zzk ni number 1
 
bora katiba ibadirishwe viwepo vyama viwili tu kama marekani kama tukienderea kuwa hivi tuta subiri sana na ccm kuondoka madarakani itabaki stori tu vikiwepo vyama viwili maendereo yatakuja haraka
Marekani Vipo vyama zaidi ya viwili mkuu..Na katiba yao haijaweka ukomo Wa vyama ila uimara Wa hivyo viwili ndo unafanya vipokezane vijiti
 
ZZK haya ni malipo ya usaliti! pole sana.Tunapoelekea wananchi wengi watashtuka na kukuachia lichama lako likufie.
 
Zitto asipoangalia atakiingiza kwenye mgogoro chama chake kama ule wa Lipumba na cuf
 
Tuitangaze tu rasmi kwamba hii ni nchi ya wanafiki au unasemaje msnajo?

Unafiki unaigharimu sana nchi hii. Unafiki top bottom, bottom up.

Iko siku Mungu ataleta hukumu kali kwa nchi hii zaidi ya hii ya "kutumbuliwa" na "kulia lia tunaibiwa" wakati ni "Viongozi" wetu ndio walisaini hati(mikataba) za kuridhia tuibiwe.


Mkuu ukitaka kujua hii nchi ipo chali mazima, angalia wasomi wetu walivyotulia! Kimya chao sio kwamba hawana la kusema, la hasha, wanasubiri uteuzi wa bwana mkubwa! Ni aibu, wasomi badala ya kutumia taaluma zao, wanataka kuwa wanasiasa! Kitila na mbwembwe zake zote sasa ivi ametulizwa anakula madhabahun, shida zake kwishney!! Hii ndp TZ, ma-dr pale UDSM kila siku wanasikilizia nani atachukuliwa, wameamua kuachana na kufanya research wanasubiri uteuzi!
 
ndio maana me na chadema yangu tu.maana kipindi zito anaenguliwa M4C. watu walimlaumu mbowe kumbe zito ccm b.leo imeonekana na ninavyojua ubunge atakosa safari hii
Yaani maelezo yote aliyotoa still unamlaumu!!?
Kweli umeonyesha kwa jinsi gani umemezezwa chuki na yule unayemuamini.

Tukikutaka ulete huo ushahidi wa ccmb, unaweza leta au mpaka ukamuombe yule alikuambia kuwa Zitto ni ccmb akupatie.

Anyway,
Tumekuelewa.
 
Back
Top Bottom