Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Nilitegemea baada ya summary itafuatia Recommendation na Conclusion! Nimetafuta recommendation na conclusion nimevikosa.Hii ngoma imekuwa ndefu sana nipeni fursa kuweka SUMMARY,
- Wenye busara wamemshauri Zitto pamoja na nia yake nzuri ya kutaka kuwa rais aendelee kusoma alama za nyakati ili wakati ukifika aingie ulingoni akiwa na nafasi nzuri kushinda/ kuchaguliwa na chama chake
- Pro CCM members wamefurahia sana uamuzi huu wa Zitto, hii imewapa mashaka makubwa sana Pro CDM members kwamba kwa nini akina Ritz, Topical, Geniusbrain nk wamfurahie Zitto katika nia yake ya kugombea against chama chao? Kuna ujumbe mzito sana behind this scene...
- Wengine wameegemea kwenye age ain't nothing but a number kwamba ujana au uzee sio ishu sana kwani kuna vijana tumewaona ni wahuni kama Adam Malima na pia kuna wazee wengine hawana busara kama Wassira. Cha muhimu ni kuwa na sifa na uwezo wa kukabiliana na matatizo yaliyopo hapa nchini na sio changamoto kwa kuwa changamoto hata zisipotatuliwa hakuna wa kulaumiwa but matatizo kama ajira kwa vijana na umaskini lazima yamalizwe na rais ajaye, Na Zitto amesema anayajua vizuri sana