Zitto, Mnyika wafichua upotoshaji bajeti ya Mkulo; Spika Makinda akiri, amtaka Mkulo arekebishe

mmmh hadi nimeogopa yani nifunguka kifikra kwamba mkulo katutupia changa la macho..mmh kweli JF inahitaji pongezi za kipekee..Dr slaa Tangaza mandamano nchi nzima kuipinga bajeti hii..
 
Hapo kwenye nyekundu unajipaisha pasipo sababu!
Back to the topic....

Ninaunga hoja hii serikali ni ya kitapeli, imecheza na takwimu kupiga rangi uwongo

Bajeti tegemezi tena yenye madeni makubwa.

Kifupi uchumi wa nchi unazidi kudidimia na umasikini kuongezeka. Siwezi shangaa Tanzania Ikawa ni nchi masikini zaidi dunia kwa mwaka ujao wa fedha.

Hahahahaha!!! Hapo kwenye nyekundu, safi sana!
 
chadema always inaifundisha gvt... budget ya vituk! baada ya chadema kusema watapunguza kodi ya mafuta kwa forty percent mkulo na eti atatelemsha kwa hiyo hiyo 40%... Je utekeleaji wake wataweza?
 
dah! Hawa magamba ni noma hadi kwenye vitu vya msingi wanaleta usanii!
Haya makosa ya makusudi kwenye bajeti yanaweza kuleta historia mpya kabisa nchini! Ni mtikisiko mkubwa! Hapa ndio watamjua Zitto na wana cdm vizuri.mtikisiko mkubwa huu
 
Safi saana Chadema, nadhani magamba always huwa wanatudanganya ndo maana hatujafanya lolote la maana kwa miaka 50 ya uhuru wetu
 
1. Nadhani Zitto anajua kuwa nishati hapa Tanzania hujengwa kutokana na misaada na mikopo kutoka nje.Hata TANESCO hutafuta funds na mikopo kutoka nje ya serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali,mfano ule wa kusambaza umeme kilomita 667 toka Iringa mpaka shinyanga ambao umekuwa funded na European Investment Bank,shs bilioni 150...je ulikuwa kwenye bajeti yoyote?

2.Kulipa deni la taifa ni moja kati ya matumizi ya maendeleo,ina facilitate uwezo wa kupata mikopo.

3. Kuhusu posho, ni wajibu wetu watanzania, hasa wafanyakazi wa serikali kuamua au kujitolea kutokuzipokea au kuomba kupunguziwa kwa asilimia hamsini..... hapatakalika!

4. Jumatano nakuchallenge Zitto, usome bajeti itakayoonyesha vyanzo mbadala vya kodi na makato ya matumizi, ili elimu iwe bure!...cos you promised this in your campaigns na ilani ya CDM, kama haita-include free education huo utakuwa ni uhuni tu! Ninayo video ya Mnyika akielezea what you will do in your first year kwenye utawala kama mngepata ridhaa.
Mkuu,

Hata William Malechela ameanza kusoma alama za nyakati anasoma upepo ulivyo. Subiri uone hao unaowatetea majibu watayoyatoa. Kwanza kabisa watasema siasa hizo!
 
Mkuu,

Hata William Malechela ameanza kusoma alama za nyakati anasoma upepo ulivyo. Subiri uone hao unaowatetea majibu watayoyatoa. Kwanza kabisa watasema siasa hizo!
Hii bajeti ni mbuzi,wala siwezi kuitetea!

Ila kuna mambo watu wanajitafutia umaarufu, bila kufikiria.

Hii bajeti hata ukiongeza trilioni mbili (shilingi), hakutakuwa na maendeleo ya maana, huwezi kuchukua shilingi ukaigeuza dola au euro kirahisi, serikali huwa haiendi bureau de change.

Inabidi tuvikabe vyanzo vya forex.....Lazima tujue tunategemea kuwa na dola au Euro ngapi kwa mwaka na tutazitumiaje......haya mambo ya shillings hayana maana.
 
Doh! Mmenifungua Macho! Wanachakachua hata bajeti! Makubwa! Asante sana, nadhani saa ya ukombozi i karibu sana sasa! Mungu awabariki azidi kuwapa upeo huu mkubwa wa kuona, ili kumkomboa mtanzania.

Kamwe huwezi kutenganisha ccm na usanii. Muhimu ni kuwaeleza wananchi kuhusu huo uhuni.
 
3.kuhusu posho,ni wajibu wetu watanzania,hasa wafanyakazi wa serikali kuamua au kujitolea kutokuzipokea au kuomba kupunguziwa kwa asilimia hamsini.....hapatakalika!

Kobello, tuongee vitu vyenye uhalisia. Posho anazoongelea Zitto hazimgusi mtanzania kama unavyotaka tuamini.

Bilioni 19 za maandazi na chapati za mwaka jana zilikuwa za 'state banquet' semina elekezi n.k. Kuna mfanyakazi wa kawaida hajawahi kupata posho hata siku moja.Karani anapata posho kwa lipi, hahudhurii semina, vikao au safari ya aina yoyote.

Posho ni kama za wabunge, mawaziri. Usitake kukwepa ukweli kwa kubadili maneno ili ionekane posho ni kwa watanzania wote, si kweli ni asilimia ndogo sana lakini ina bajeti kubwa sana.

Mwalimu kule mkuranga hajapata mshahara, kobello anatuaminisha kuwa naye ni miongoni mwa Watz wanopata posho!!!!!!!!!!!!
 
1. Nadhani Zitto anajua kuwa nishati hapa Tanzania hujengwa kutokana na misaada na mikopo kutoka nje.Hata TANESCO hutafuta funds na mikopo kutoka nje ya serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali,mfano ule wa kusambaza umeme kilomita 667 toka Iringa mpaka shinyanga ambao umekuwa funded na European Investment Bank,shs bilioni 150...je ulikuwa kwenye bajeti yoyote?

2.Kulipa deni la taifa ni moja kati ya matumizi ya maendeleo,ina facilitate uwezo wa kupata mikopo.

3. Kuhusu posho, ni wajibu wetu watanzania, hasa wafanyakazi wa serikali kuamua au kujitolea kutokuzipokea au kuomba kupunguziwa kwa asilimia hamsini..... hapatakalika!

4. Jumatano nakuchallenge Zitto, usome bajeti itakayoonyesha vyanzo mbadala vya kodi na makato ya matumizi, ili elimu iwe bure!...cos you promised this in your campaigns na ilani ya CDM, kama haita-include free education huo utakuwa ni uhuni tu! Ninayo video ya Mnyika akielezea what you will do in your first year kwenye utawala kama mngepata ridhaa.
Kobello, Kobello

Please be candid to your country. It doesnt pay to support where you are suppose to critize or have a different idea. This reminds me of the saying; if two people agree in everything one of them is not thinking.

You seem to be supporting each and everything done by the govt.

Haya mkuu, nadhani huitendei haki serikali yetu. Nilitarajia utapingana na mleta thread badala yake tunaleta ujanja wa kujaribu kututoa kwenye topic.
Hongera
 
2. Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa. Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.
Hakuna ubaya kwa kulipa madeni, ila ingekuwa ni vizuri waziri akweka bayana kuwa katika bejeti hii serikali imamua kulipa madeni ili angalu kujenga imani kwa wakopeshaji.

Halafu serikali iwe wakweli kwa kutuambia kitaalamu kuwa matumizi ya 11.6 bilioni mwaka huu hayana thamani sawa na 11.6 billioni za mwaka jana kutokana na depreciation ya shilling.

Serikali imeamua kupunguza ukubwa wa bejti yake kisirisiri; tutakoma ubishi mwaka huu
 
Serikali hii inahitaji tuzo kwa usanii, haipendezi hata kidogo kuuongopea umma wa watanzania, yaani umeandika 300000 wewe unatamko 50000? Kiukweli hawana msaada kwetu, hongereni CDM nyie onyesheni njia sisi tutafuata hatutawaacha peke yenu
 
Hii bajeti ni mbuzi,wala siwezi kuitetea!

Ila kuna mambo watu wanajitafutia umaarufu, bila kufikiria.

Hii bajeti hata ukiongeza trilioni mbili (shilingi), hakutakuwa na maendeleo ya maana, huwezi kuchukua shilingi ukaigeuza dola au euro kirahisi, serikali huwa haiendi bureau de change.

Inabidi tuvikabe vyanzo vya forex.....Lazima tujue tunategemea kuwa na dola au Euro ngapi kwa mwaka na tutazitumiaje......haya mambo ya shillings hayana maana.
At least tumekutana ila mkuu tatizo ulilotaja si msingi wa mtatizo ya bajeti bali namna tunavyosimamia na kudhibiti matumizi.ulichotaja ni zao tu. Hata mipango ya kukusanya mapato haijajikita kwenye vyanzo vikuu na muhimu sana kama madini, utalii.

Nilichokoza jana kuwa bajeti yetu ina kurasa 126 na pale kenya ni 32 sababu si wingi wa karatasi tu bali mbwembwe za kisiasa za kutoa matumaini.

Kama content ni ya maana nafikiri isingekuwa hoja. Hivi kuna umuhimu wa kuanza kupongeza ushindi wa Rais, PM, speaker na upupu mwingi while juzi tu wamepongezana? That was not relevant. Akina Zitto wamekesha tu tayari wamegundua makosa kibao while wao wameiandaa muda mrefu tu.
 
Kobello, tuongee vitu vyenye uhalisia. Posho anazoongelea Zitto hazimgusi mtanzania kama unavyotaka tuamini.

Bilioni 19 za maandazi na chapati za mwaka jana zilikuwa za 'state banquet' semina elekezi n.k. Kuna mfanyakazi wa kawaida hajawahi kupata posho hata siku moja.Karani anapata posho kwa lipi, hahudhurii semina, vikao au safari ya aina yoyote.

Posho ni kama za wabunge, mawaziri. Usitake kukwepa ukweli kwa kubadili maneno ili ionekane posho ni kwa watanzania wote, si kweli ni asilimia ndogo sana lakini ina bajeti kubwa sana.

Mwalimu kule mkuranga hajapata mshahara, kobello anatuaminisha kuwa naye ni miongoni mwa Watz wanopata posho!!!!!!!!!!!!
Nitakupa mfano mdogo tu.Hebu angalia posho za serikali za mitaa,

Nataja wafanyakazi wa serikali, nina rafiki yupo IT Wizara moja na mwaka 2010 amekula posho si chini ya shs milioni15, na huyo ni ofisa wa kawaida tu wizarani.

Mawaziri na wabunge nao pia, lakini kuna wafanyakazi wa ngazi za kati, wanakula posho, na magari yao yanalipiwa mafuta kila mwezi wakati CEO wangu hapa US anaendesha gari lake kuja kazini na hana secretary wala tarishi.

Don't act like you don't know!
 
1. Nadhani Zitto anajua kuwa nishati hapa Tanzania hujengwa kutokana na misaada na mikopo kutoka nje.Hata TANESCO hutafuta funds na mikopo kutoka nje ya serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali, mfano ule wa kusambaza umeme kilomita 667 toka Iringa mpaka shinyanga ambao umekuwa funded na European Investment Bank,shs bilioni 150...je ulikuwa kwenye bajeti yoyote?

@Kobello hapo kwenye red; unaweza kutueleza kwa nini nishati Tanzania inajengwa kutokana na misaada na mikopo toka nje? Wanaotupa misaada wanapata nini in return?

Unajua serikali ilitoa stimulus package kiasi gani na kwa nani? Kuna uwezekano hii amount ya stimulus package ingetatuwa tatizo la nishati kwa kiasi kikubwa?
 
Loooh! nimefumbuka macho,

Kumbe uchakachuaji hata kwenye bajeti. Hii ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi na watu wake, nawapongeza sana CHADEMA na Mungu aendelee kusimamia harakati zenu za ukombozi, pia ili kuleta uwazi ktk bajeti zijazo ni lazima kuwe na pre-budget discussions kwa wadau wote ili kukidhi haja za wenye nchi na sio kuleta uwongo kwnye masuala ya msingi.
 
Akina zitto wamekesha tu tayari wamegundua makosa kibao while wao wameiandaa muda mrefu tu.
Tehe teh teh.... Utawezaje kuwa mwenyekiti wa PRSC na usijue bajeti itakuwa kiasi gani,mimi nilishaiona gazetini tangu early may!! na wataalam wengi walishamwambia haitoshi,au wewe ulikuwa hujui?

Ndio maana unanikashifu na kuwapa vichwa watu wanaohitaji kura yako...same old stories brother!
 
Back
Top Bottom