Zitto kufunguliwa mashtaka endapo...

Huyu jamaa anaitwa Zitto ni mtu ambaye nilikuwa na mkubali sana kutoka na siasa zake, ila baada ya kugundua kuwa huyu jamaa ni Mnafiki na Mchumia tumbo Ahaaaaa! nimeingiwa nyongo na huyu kiasi kwamba sura yake huwa naiyona kama jinamizi vile. Hafai kabisa. Mwanzoni niliona km wanamuonea kumbeeee
 
Hawana lolote hao akina soud umaarufu wanaoutaka Mzanzibari gani asiekua na Imani na Nchi yake
Anasaka tonge na umaarufu tuu huyo Soud na mwenzake
 
Viongozi wengi wa Zanzibar huwa wana uelewa mdogo sn ktk mambo mhimu.

Hata Dr. Shein CCM bara isingeingilia tiyar Maalim alikuwa kashamgalagaza chaliii!!

Sijui Nyerere alihujumu Syllabus yao toka Primary to Univ.?
 
Huyu jamaa anaitwa Zitto ni mtu ambaye nilikuwa na mkubali sana kutoka na siasa zake, ila baada ya kugundua kuwa huyu jamaa ni Mnafiki na Mchumia tumbo Ahaaaaa! nimeingiwa nyongo na huyu kiasi kwamba sura yake huwa naiyona kama jinamizi vile. Hafai kabisa. Mwanzoni niliona km wanamuonea kumbeeee

Toa maelezo juu ya unafiki wake....weka na viambata
 



Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini.

Msimamo huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa Zanzibar kubakia madarakani wakati serikali yake imefikia ukomo wake Novemba 2, mwaka huu.

Soud alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Kifungu cha 28 (1)(a), Rais Shein ni Rais halali wa Zanzibar na atabakia madarakani hadi atakapochaguliwa rais mpya kwenye uchaguzi wa marudio.

Alisema kuwa Dk. Shein alichaguliwa na wananchi wa Zanzibar na haikuwa haki kwa Zitto kumhusisha na makosa ya uhaini kwa kuendelea kubaki madarakani kwani yuko kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. ?Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14 na asipofanya hivyo tutamfungulia mashitaka.? alisema Soud pia Mwenyekiti wa Chama cha AFP.

Katika sakata hilo, Juma Ali Khatib, alisema tayari ameanza kutafuta namna ya kuwasiliana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Zitto kwa kumhusisha na makosa ya uhaini Rais wa Zanzibar.

Alisema iwapo Bunge litashindwa kumchukulia hatua za kinidhamu Zitto, yeye atalazimika kufungua kesi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kupinga kauli ya Zitto.

Khatib alisema Zanzibar ni nchi na Rais wa Zanzibar lazima apewe heshima yake kwa sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani ni matakwa ya Kikatiba.

?Kumdhalilisha Rais wa nchi ni sawa na kutudhalilisha wananchi wake, rais anashauriwa na vyombo vingi vya sheria hivyo hawezi kuvunja Katiba,??alisema Khatib
Viongozi hao si wa kwanza kujitokeza kumtetea Rais wa Zanzibar kwani walitanguliwa na aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, Simai Mohamed Said, tangu Zitto alipotoa kauli kuwa Zanzibar haina rais na kuendelea kubakia madarakani Rais Shein ni sawa na kufanya uhalifu wa uhaini.

Katika mkutano wake na wandishi wa habari hivi karibuni, Zitto alisema kwa sasa Zanzibar haina serikali na mtu yoyote anayejiita rais wa Zanzibar kikatiba amepindua nchi na katika hali ya kawaida anapaswa kushitakiwa kwa uhaini.



CHANZO: NIPASHE



Hawakusoma kifungu cha chini yake kinasema nini katiba ibara hiyo. Kinasema "miaka mitano kuanzia siku ya kula kiapo". Ina maana rais atakuwa madarakani mpaka atakapoapishwa "ndani ya huo muda wa miaka mitano" na si nje yake maana ikiwa nje then hicho kifungu hakina maana kwa sababu rais anayamaliza muda wake anaweza pia kukaa bila kwa muda zaidi ya huo bila kuapishwa. Kilichotakiwa ni kuona utaratibu wa au kubadili hicho kifungu cha katiba ili aendelee kukaa nje ya muda wa miaka 5 au ufanyike utaratibu mwingine wa mpito. Hivi ndivyo nionavyo mimi.
 
Na wasi wasi wengi tunachangia kwa utashi na matamanio ya nafsi zetu pasi na kujua kwa uhakika kile unachosema.
Wengi wana shout khs Mr.Zitto bila hujjah zenye mashiko na wengi wanatumika kalima "MNAFIKI"
Labda twambieni

1) unafiki ni nini na ni nani mnafiki?

2) unafiki wa Zitto uko wapi?

3) Leteni ushahidi yakinifu unao mtia Zitto ktk unafiki huku ukichunga asitoke ktk maana ulizo zitaja hapo juu za Nifaaq (unafiki).

KUNA WATU WANAONGEA ILI WAONEKANE NAO WAMEONGEA NA UTAKAPO WAULIZA KWA NINI UNAONGEA HIVI HUKOSA JAWABU NA BADALA YAKE HUTUKANA.

MTU MWENYE BUSARA HASEMI KILA ANACHO KIONA NA ENDAPO ATASEMA BASI HUSEMA LILILO LA HAKI NA KWELI EVEN THOUGH YULE ANAYE MSEMEA NI ADUI WAKE NA HAPASWI KUONYESHA UADUI WAKATI HUO.

HII NI SIFA YA MTU MWENYE BUSARA NA MUADILIFU WAKUU.
 
Na wasi wasi wengi tunachangia kwa utashi na matamanio ya nafsi zetu pasi na kujua kwa uhakika kile unachosema.
Wengi wana shout khs Mr.Zitto bila hujjah zenye mashiko na wengi wanatumika kalima "MNAFIKI"
Labda twambieni

1) unafiki ni nini na ni nani mnafiki?

2) unafiki wa Zitto uko wapi?

3) Leteni ushahidi yakinifu unao mtia Zitto ktk unafiki huku ukichunga asitoke ktk maana ulizo zitaja hapo juu za Nifaaq (unafiki).

KUNA WATU WANAONGEA ILI WAONEKANE NAO WAMEONGEA NA UTAKAPO WAULIZA KWA NINI UNAONGEA HIVI HUKOSA JAWABU NA BADALA YAKE HUTUKANA.

MTU MWENYE BUSARA HASEMI KILA ANACHO KIONA NA ENDAPO ATASEMA BASI HUSEMA LILILO LA HAKI NA KWELI EVEN THOUGH YULE ANAYE MSEMEA NI ADUI WAKE NA HAPASWI KUONYESHA UADUI WAKATI HUO.

HII NI SIFA YA MTU MWENYE BUSARA NA MUADILIFU WAKUU.

CDM wote wamekula yamini ya kumuita zitto mnafiki.....no reason for justification.

Mwingine waliyekula yamini kumuita hivyo ni Dr. Slaa
 
Kwamujibu wakatiba ya zanzibar ibara ya 28 ibara ndogo ya pili raisi ataacha madaraka yake mbaada ya kumaliza miaka mitano tangu....... ukishuka kifungu cha pili kinasema pale alipokula kiapo cha uaminifu na kiaPo cha kuwa raisi.
ibara ndogo ya tatu inasema itakuwa marufuku kwa raisi kuvuka kipindi kimoja cha miaka mitano kila kimoja.
Nendeni mahakamani enyi vibaraka wa haini mkapigwe nyundo. Mnakuwa viongozi wa chama hamjui hata katiba yenu
 
Ccm inafanya uhaini pale inapo ing'ang'ania Zanzibar ni uhaini kuwa raisi kinyume cha taratibu
 
hahahahahaha we mgeni wa siasa za bongo nn! hapo kuna wale wabaya wake wanatamani achafuke hivyohivyo, si unakumbuka ile vitA yao haijaisha.
 
Zitto ni mnafiki tu. Kama anamaanisha anachokisema basi angetoka nje Dr. Sheni alipoingia bungeni. Kubaki kwake kulimaanisha anamuunga mkono na anakubali kinachoendelea ZNZ.
Acha wivu wa kike, kila mtu anatumia njia yake ktk kufikisha ujumbe wake, zitto hakusimama shein alipoingia kuonesha hamtambui, au ulitaka amtii mfalme mbowe ndo uone sio mnafiki, hovyo kweli wewe
 
Chadema mps are feelng ov only one kamanda in the war field duuu propaganda zmeanza mapema tarehe za bunge kuanza bado jaman
 
Back
Top Bottom