Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tuyaenzi kwa 4R za Rais Samia?, JMT Tuitendee Haki Zanzibar?, Tuwatendee Haki Wazanzibari? Mshindi Halali Apewe?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu, kumpongeza Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dr, Husein Mwinyi, kwa Zanzibar kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku waliopindua wakiyaenzi na kuyaita Mapinduzi Matukufu, huku waliopinduliwa wakisema Mapinduzi yale hayana utukufu wowote kwasababu yaliandamana na umwagaji wa damu.

Kufuatia uwepo wa kambi hizi mbili, nashauri, katika kuyaenzi Mapinduzi, tuitumie falsafa ya Rais Samia, ya 4R kutibu makovu ya Mapinduzi, na kuponya vidonda ambavyo ni vibichi vya yatokanayo na Mapinduzi hayo. Hivyo haya ni maswali kwenye pongezi zangu za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, jee tuyaenzi kwa 4R za Rais Samia?, Serikali ya JMT tuitendee haki Zanzibar kwa kuitambua rasmi katiba yao, hivyo lazima tuirekebishe katiba yetu iitambue GNU?, Tuwatendee Haki Wazanzibari kwa kuwaruhusu kuingia mikataba Zanzibar iwe kama Dubai? Turuhusu Mshindi Halali wa Uchaguzi wa Zanzibar 2025. Atangazwe?, Apewe?.

Nawaasa Wazanzibari kuielewa na kuizingatia falsafa ya 4R iliyoasisiwa na kutumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuyafikia mafanikio na kuwa Zanzibar moja kwa maendeleo endelevu.

Falsafa hiyo ya 4R inahusu mambo manne ya msingi ya kuzingatiwa ambayo ni Maridhiano , Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi mpya (Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding).

Zanzibar ni nchi ya mapinduzi, hivyo kuna aliyepindua, anayetamalaki kwa shangwe, nderemo, vifijo na shamra shamra zote kusherehehekea miaka 60 ya Mapinduzi, lakini pia yupo aliyepinduliwa, huyu amenyamaza kimya akiumia chini kwa chini na ndani kwa ndani kila akikumbuka kilichotokea na yatokanayo na mapinduzi hayo.

Zanzibar kunahitajika kuundwa tume ya Mapatano na Maridhiano (Reconciliation) kuwaponya walioumizwa na Mapinduzi yale, ili kujenga Zanzibar moja yenye kusameheana, kuleta umoja na amani na maelewano kwa wote Zanzibar kwa kuhuisha moyo wa kitaifa na kuinganisha nguvu ya pamoja katika kuleta maendeleo endelevu kwa visiwa hivyo vya Karafuu.

Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kumfanyia application ya zile 4R za Rais Samia kwa kuwasamehe, wapinduliwa wote akiwemo Sultan mpinduliwa, kuwajengea mazingira wezeshi wawe huru kurejea Zanzibar, ili kushiriki katika ujenzi wa Zanzibar moja yenye uhuru, umoja, upendo, amani, na mshikamano.

Hili likifanyika, Rais Samia na rais Mwinyi, watabarikiwa sana for kwa kuponya machungu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na Zanzibar itabarikiwa sana!.

Japo SUK imeleta mshikamano, lakini bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo Changamoto za muungano ambazo zamani zilikuwa zikiitwa kero za muungano, kule Pemba wanaziita makero.

Hapa R ya pili ya Ustahimilivu (Resilience) itumike kutatua changamoto hizo za muungano na kuzigeuza fursa. Wapindua wasinyanyue mabega juu kujiona wao ndio wao, na wapinduliwa wasijisikie wanyonge. Wote wawe wastahimilivu kama katika kuleta maendeleo kwani katika dunia ya sasa changamoto haziepukiki kwani ni dunia ya sayansi na teknolojia na lazima tukabiliane na kila changamoto kwa Ustahimilivu.

Mfano mzuri wa ustahimilivu ni japo mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 yako kinyume na katiba ya JMT, madam yote yamefanywa kwa ajili ya Zanzibar, safari hii serikali ya JMT imestahimili, ilichofanya ni kwa Katiba ya JMT kutofanyiwa mabadiliko kuyatambua mabadiliko ya katiba ya Zanzibar, lakini protokali zote zinayatambua.

Kwa upande wa Mabadiliko (Reforms) kiukweli Rais Mwinyi, kupitia falsafa yake ya Uchumi wa Buluu, ameibadili Zanzibar kutokuwa watumwa wa historia ya Mapinduzi bali kuirejesha kuwa nchi ya maendeleo makubwa eneo hili la Afrika Mashariki. Zanzibar ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na Televisheni ya Rangi mwaka 1971, Rais Mwinyi anafanya Reforms nyingi zinazoipaisha Zanzibar kitaifa na kimataifa.

Nikimalizia na dhana ya Ujenzi mpya (Rebuilding) Rais Mwinyi anafanya mengi makubwa kwenye kuijenga upya Zanzibar umuhimu wa kujifanyia tathimini kwa kuangalia mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi na Kiyonga mbele katika kusukuma maendeleo

Rais Samia ilichokifanya huku Tanzania Bara, Rais Mwinyi akifanye Zanzibar, katika hali ya maelewano,usalama,na maendeleo endelevu kufuatia siasa za uhasama zilizorithiwa kutokana historia ya vyama vingi na mapungufu mbalimbali ndani ya vyama vya upinzani pamoja na serikali. Raisi Samia Suluhu Hassan ameamua kujenga nchi yenye watanzania wanaoishi kwa kusameheana, kuvumiliana, kuleta mabadiliko na kujenga nchi kwa pamoja.Mpango mkakati huu wa R4 za Rais Samia zimesaidia sana huku bara.

Uongozi imara wa Raisi Samia Suluhu Hassan umefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani, makundi mbalimbali, asasi za kiraia na matunda ya upatanishi yanaonekana katika jamii ya Watanznaia. Viongozi wakuu wote wa vyama vya upinzani wameoneshwa kufurahia na kuunga mkono juhudi hizi za Raisi Samia kwenye sera zake pamoja na nia yake ya kuikwamua Tanzania ilipokuwa imekwama tunakwenda kuwa sheria mpya ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi na Uwanja sawa wa kufanya siasa.

Kinachofanyika Bara, kifanyike Zanzibar, Rais Mwinyi akae na wapinzani Zanzibar, wafanye mapitio ya maridhiano, ili uchaguzi wa Zanzibar wa 2025 uwe ni uchaguzi huru na wa haki na mshindi halali atangazwe, n ahata ikitokea,.. atangazwe tuu.

Mwisho ni ombi kwa Rais Samia, ili hizi 4R zilete manufaa ya kweli, lazima tufanye mabadiliko madogo ya katiba ya JMT, tuwatendee haki Zanzibar kwa madadiliko ya katiba yao ya 2010, yatambuliwe na katiba ya Tanzania. Kama Tanzania tumeweza kuingia mkataba wa DPW na Dubai ambayo sio nchi na ina hadhi saw ana Zanzibar ndani ya JMT, tuitendee haki Zanzibar kuweza kuingia mikataba bila udhamini wa JMT, Zanzibar iwe Dubai ya Afrika Mashariki, yale magari watu wanayafuata Japan na Dubai, wayafuate Zanzibar.

Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania

Hongera Zanzibar kwa Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Paskali.
 
Hayo mabadiliko itakuwa vigumu sana kufanyika, kwa sababu hata hizo 4R za Samia kiuhalisia zimeshakufa, ndio maana hata ile habari ya maridhiano kwasasa imebaki historia.

Naamini hata Zanzibar pia, CCM wanaweza kutudanganya kwa kila aina ya maneno mazuri, lakini kamwe, hawatakaa waiweke rehani nafasi ya kuunda serikali waliyonayo, never.

Hawa jamaa wako tayari kucheza michezo yote, kama ule wa Rasimu ya Warioba na kupoteza pesa nyingi za walipa kodi wasijali, lakini usijaribu kuonesha dalili za kuleta uwanja sawa wa kufanya siasa ukadhani watakutazama tu, that will never ever happen.

Hasa nikukumbuka siku ile Mkapa alipopanda ndege kwenda Zanzibar kumwambia Jecha apindue meza, naona bado tuna safari ndefu sana.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Wanabodi,

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu, kumpongeza Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dr, Husein Mwinyi, kwa Zanzibar kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku waliopindua wakiyaenzi na kuyaita Mapinduzi Matukufu, huku waliopinduliwa wakisema Mapinduzi yale hayana utukufu wowote kwasababu yaliandamana na umwagaji wa damu.

Kufuatia uwepo wa kambi hizi mbili, nashauri, katika kuyaenzi Mapinduzi, tuitumie falsafa ya Rais Samia, ya 4R kutibu makovu ya Mapinduzi, na kuponya vidonda ambavyo ni vibichi vya yatokanayo na Mapinduzi hayo. Hivyo haya ni maswali kwenye pongezi zangu za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, jee tuyaenzi kwa 4R za Rais Samia?, Serikali ya JMT tuitendee haki Zanzibar kwa kuitambua rasmi katiba yao, hivyo lazima tuirekebishe katiba yetu iitambue GNU?, Tuwatendee Haki Wazanzibari kwa kuwaruhusu kuingia mikataba Zanzibar iwe kama Dubai? Turuhusu Mshindi Halali wa Uchaguzi wa Zanzibar 2025. Atangazwe?, Apewe?.

Nawaasa Wazanzibari kuielewa na kuizingatia falsafa ya 4R iliyoasisiwa na kutumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuyafikia mafanikio na kuwa Zanzibar moja kwa maendeleo endelevu.

Falsafa hiyo ya 4R inahusu mambo manne ya msingi ya kuzingatiwa ambayo ni Maridhiano , Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi mpya (Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding).

Zanzibar ni nchi ya mapinduzi, hivyo kuna aliyepindua, anayetamalaki kwa shangwe, nderemo, vifijo na shamra shamra zote kusherehehekea miaka 60 ya Mapinduzi, lakini pia yupo aliyepinduliwa, huyu amenyamaza kimya akiumia chini kwa chini na ndani kwa ndani kila akikumbuka kilichotokea na yatokanayo na mapinduzi hayo.

Zanzibar kunahitajika kuundwa tume ya Mapatano na Maridhiano (Reconciliation) kuwaponya walioumizwa na Mapinduzi yale, ili kujenga Zanzibar moja yenye kusameheana, kuleta umoja na amani na maelewano kwa wote Zanzibar kwa kuhuisha moyo wa kitaifa na kuinganisha nguvu ya pamoja katika kuleta maendeleo endelevu kwa visiwa hivyo vya Karafuu.

Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kumfanyia application ya zile 4R za Rais Samia kwa kuwasamehe, wapinduliwa wote akiwemo Sultan mpinduliwa, kuwajengea mazingira wezeshi wawe huru kurejea Zanzibar, ili kushiriki katika ujenzi wa Zanzibar moja yenye uhuru, umoja, upendo, amani, na mshikamano.

Hili likifanyika, Rais Samia na rais Mwinyi, watabarikiwa sana for kwa kuponya machungu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na Zanzibar itabarikiwa sana!.

Japo SUK imeleta mshikamano, lakini bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo Changamoto za muungano ambazo zamani zilikuwa zikiitwa kero za muungano, kule Pemba wanaziita makero.

Hapa R ya pili ya Ustahimilivu (Resilience) itumike kutatua changamoto hizo za muungano na kuzigeuza fursa. Wapindua wasinyanyue mabega juu kujiona wao ndio wao, na wapinduliwa wasijisikie wanyonge. Wote wawe wastahimilivu kama katika kuleta maendeleo kwani katika dunia ya sasa changamoto haziepukiki kwani ni dunia ya sayansi na teknolojia na lazima tukabiliane na kila changamoto kwa Ustahimilivu.

Mfano mzuri wa ustahimilivu ni japo mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 yako kinyume na katiba ya JMT, madam yote yamefanywa kwa ajili ya Zanzibar, safari hii serikali ya JMT imestahimili, ilichofanya ni kwa Katiba ya JMT kutofanyiwa mabadiliko kuyatambua mabadiliko ya katiba ya Zanzibar, lakini protokali zote zinayatambua.

Kwa upande wa Mabadiliko (Reforms) kiukweli Rais Mwinyi, kupitia falsafa yake ya Uchumi wa Buluu, ameibadili Zanzibar kutokuwa watumwa wa historia ya Mapinduzi bali kuirejesha kuwa nchi ya maendeleo makubwa eneo hili la Afrika Mashariki. Zanzibar ndio ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na Televisheni ya Rangi mwaka 1971, Rais Mwinyi anafanya Reforms nyingi zinazoipaisha Zanzibar kitaifa na kimataifa.

Nikimalizia na dhana ya Ujenzi mpya (Rebuilding) Rais Mwinyi anafanya mengi makubwa kwenye kuijenga upya Zanzibar umuhimu wa kujifanyia tathimini kwa kuangalia mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi na Kiyonga mbele katika kusukuma maendeleo

Rais Samia ilichokifanya huku Tanzania Bara, Rais Mwinyi akifanye Zanzibar, katika hali ya maelewano,usalama,na maendeleo endelevu kufuatia siasa za uhasama zilizorithiwa kutokana historia ya vyama vingi na mapungufu mbalimbali ndani ya vyama vya upinzani pamoja na serikali. Raisi Samia Suluhu Hassan ameamua kujenga nchi yenye watanzania wanaoishi kwa kusameheana, kuvumiliana, kuleta mabadiliko na kujenga nchi kwa pamoja.Mpango mkakati huu wa R4 za Rais Samia zimesaidia sana huku bara.

Uongozi imara wa Raisi Samia Suluhu Hassan umefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani, makundi mbalimbali, asasi za kiraia na matunda ya upatanishi yanaonekana katika jamii ya Watanznaia. Viongozi wakuu wote wa vyama vya upinzani wameoneshwa kufurahia na kuunga mkono juhudi hizi za Raisi Samia kwenye sera zake pamoja na nia yake ya kuikwamua Tanzania ilipokuwa imekwama tunakwenda kuwa sheria mpya ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi na Uwanja sawa wa kufanya siasa.

Kinachofanyika Bara, kifanyike Zanzibar, Rais Mwinyi akae na wapinzani Zanzibar, wafanye mapitio ya maridhiano, ili uchaguzi wa Zanzibar wa 2025 uwe ni uchaguzi huru na wa haki na mshindi halali atangazwe, n ahata ikitokea,.. atangazwe tuu.

Mwisho ni ombi kwa Rais Samia, ili hizi 4R zilete manufaa ya kweli, lazima tufanye mabadiliko madogo ya katiba ya JMT, tuwatendee haki Zanzibar kwa madadiliko ya katiba yao ya 2010, yatambuliwe na katiba ya Tanzania. Kama Tanzania tumeweza kuingia mkataba wa DPW na Dubai ambayo sio nchi na ina hadhi saw ana Zanzibar ndani ya JMT, tuitendee haki Zanzibar kuweza kuingia mikataba bila udhamini wa JMT, Zanzibar iwe Dubai ya Afrika Mashariki, yale magari watu wanayafuata Japan na Dubai, wayafuate Zanzibar.

Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania

Hongera Zanzibar kwa Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Paskali.
Umenena! Asante mkuu🙏🙏🙏
 
Turuhusu Mshindi Halali wa Uchaguzi wa Zanzibar 2025. Atangazwe?, Apewe?.
Kumbe washindi halali huwa hawapewi ushindi ?.....kweli hii nchi ina demokrasia bandia (fake democracy).....

Tunachezea pesa kwa uchaguzi wa kihuni huku tukiwa na changamoto kibao zinazohitaji pesa, matumizi mabaya ya akili ndio haya.
 
Back
Top Bottom