Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,063
Umeme ni idara pekee duniani inayofanya kazi kwa HASARA. Ndiyo maana karibu kila sehemu duniani, Serikali za nchi hizo huwa zinasaidia kulipia gharama baadhi ili kupunguza makali yake.
Gharama kubwa ziko kwenye UGAWAJI wa umeme. Ndiyo maana hawa wote akina NSSF, DOWANS, SONGA nk wako kwenye kuzalisha tu na kusambaza wanataka TANESCO wafanye na wao walipwe kwa kuzalisha tu. Ukweli ni kuwa gharama za kuzalisha, milele si kubwa ki hivyo ila USAMBAZAJI gharama zake sinatisha hasa kwa nchi ambayo miji iko mbalimbali sana kama Tanzania.
Wenzetu wa Ulaya kwa mfano ni rahisi sana maana nchi zao si kubwa sana na miji ipo karibu karibu mno.
Nina imani hata kwenye KUGAWA kama kungelikuwa na FAIDA, basi kuanzia enzi ya Mkapa, wangelibadili sheria ili na wao wasambaze na kuvuna hayo mahela. Ila utawasikia kuwa TAnesco pekee ndiyo watauza UMEME ila makampuni mengine yanaweza kuzalisha umeme na kuuza kwa TANESCO. Na hapo ndipo utaona wazalishaji Uchwara weeengi wakija kwan nguvu zote maana hapo kuna ulaji wa uhakika bila kuhangaika na Wateja, wezi wa umeme, nyaya za kusambaza umeme na nguzo zake na wezi wa vyuma/nguzo, wizi wa mafuta ya Transformer, long distance katika kusambaza umeme nk nk.
Umeona kwenye MAJI wanalilia hata siku moja? Sababu ni kwamba, maji KUSAMBAZA ni rahisi kidogo ila KUZALISHA ni kasheshe maana inabidi kweli kujiandaa na si blaa blaa. Na maji watu wana visima ila umeme, mhh GENERATOR? Huwezi hata kusema ukachote UMEME kwa ajili ya kiwanda. Itabaki unasubiri tu kwenye mgawo.
Kuna miradi NSSF wanaweza kujiingza na wakapata faida ila siyo kuzalima Umeme, Maji, Usafiri wa Reli ......
Wamenikatia umeme sasa hivi. Laptop ikiishiwa charge, nimedoda.

Wakuu, nadhani mpango wa NSSF kununua Kiwira haukuanzishwa na Mh. Zitto, mbona hatuwasakami hao hao NSSF wanaotaka kuwekeza kwenye mradi wa kujenga bomba la gesi toka Mtwara kwenda Mombasa na Mwanza?, mradi wa kujenga UDOM, magorofa ya Mchikichini, daraja la Kigamboni etc, etc, etc...
Mimi si msemaji wa mh. Zitto isipokuwa naamini kabisa yeye binafsi amekuwa mshabiki wa suala hili kutokana na performance ya NSSF kwenye miradi yao mingine waliyokwisha fanya.
Pia imani yake inaweza kuwa inachangiwa na uwezo wa kifedha wa NSSF ukilinganisha na wawekezaji wengine ambao malengo yao makubwa ni kuchota pesa za mradi badala ya kuwekeza pesa. Mfano mzuri ni hiyo kampuni iliyoshindwa hapo Kiwira iliyokuwa ikimilikiwa na comradi Nkapa....
Mwisho nawaombeni tumuache kijana afanye kazi...ingawaje kumkosoa ni vizuri lakini ingekuwa vizuri zaidi kumkosoa pale alipo haribu na sio kumfuatilia kwa kila jambo. Kwanza kumbukeni huyu ni member mwezetu hapa jamvini, tusimfanye achukie na mwisho ajitoe jamvini...:washing: