Zitto, imetosha sasa

Umeme ni idara pekee duniani inayofanya kazi kwa HASARA. Ndiyo maana karibu kila sehemu duniani, Serikali za nchi hizo huwa zinasaidia kulipia gharama baadhi ili kupunguza makali yake.

Gharama kubwa ziko kwenye UGAWAJI wa umeme. Ndiyo maana hawa wote akina NSSF, DOWANS, SONGA nk wako kwenye kuzalisha tu na kusambaza wanataka TANESCO wafanye na wao walipwe kwa kuzalisha tu. Ukweli ni kuwa gharama za kuzalisha, milele si kubwa ki hivyo ila USAMBAZAJI gharama zake sinatisha hasa kwa nchi ambayo miji iko mbalimbali sana kama Tanzania.

Wenzetu wa Ulaya kwa mfano ni rahisi sana maana nchi zao si kubwa sana na miji ipo karibu karibu mno.

Nina imani hata kwenye KUGAWA kama kungelikuwa na FAIDA, basi kuanzia enzi ya Mkapa, wangelibadili sheria ili na wao wasambaze na kuvuna hayo mahela. Ila utawasikia kuwa TAnesco pekee ndiyo watauza UMEME ila makampuni mengine yanaweza kuzalisha umeme na kuuza kwa TANESCO. Na hapo ndipo utaona wazalishaji Uchwara weeengi wakija kwan nguvu zote maana hapo kuna ulaji wa uhakika bila kuhangaika na Wateja, wezi wa umeme, nyaya za kusambaza umeme na nguzo zake na wezi wa vyuma/nguzo, wizi wa mafuta ya Transformer, long distance katika kusambaza umeme nk nk.

Umeona kwenye MAJI wanalilia hata siku moja? Sababu ni kwamba, maji KUSAMBAZA ni rahisi kidogo ila KUZALISHA ni kasheshe maana inabidi kweli kujiandaa na si blaa blaa. Na maji watu wana visima ila umeme, mhh GENERATOR? Huwezi hata kusema ukachote UMEME kwa ajili ya kiwanda. Itabaki unasubiri tu kwenye mgawo.

Kuna miradi NSSF wanaweza kujiingza na wakapata faida ila siyo kuzalima Umeme, Maji, Usafiri wa Reli ......

Wamenikatia umeme sasa hivi. Laptop ikiishiwa charge, nimedoda.
Wakuu, nadhani mpango wa NSSF kununua Kiwira haukuanzishwa na Mh. Zitto, mbona hatuwasakami hao hao NSSF wanaotaka kuwekeza kwenye mradi wa kujenga bomba la gesi toka Mtwara kwenda Mombasa na Mwanza?, mradi wa kujenga UDOM, magorofa ya Mchikichini, daraja la Kigamboni etc, etc, etc...

Mimi si msemaji wa mh. Zitto isipokuwa naamini kabisa yeye binafsi amekuwa mshabiki wa suala hili kutokana na performance ya NSSF kwenye miradi yao mingine waliyokwisha fanya.

Pia imani yake inaweza kuwa inachangiwa na uwezo wa kifedha wa NSSF ukilinganisha na wawekezaji wengine ambao malengo yao makubwa ni kuchota pesa za mradi badala ya kuwekeza pesa. Mfano mzuri ni hiyo kampuni iliyoshindwa hapo Kiwira iliyokuwa ikimilikiwa na comradi Nkapa....

Mwisho nawaombeni tumuache kijana afanye kazi...ingawaje kumkosoa ni vizuri lakini ingekuwa vizuri zaidi kumkosoa pale alipo haribu na sio kumfuatilia kwa kila jambo. Kwanza kumbukeni huyu ni member mwezetu hapa jamvini, tusimfanye achukie na mwisho ajitoe jamvini...:washing:
 
Najua hii ilipoanzia!

Ule mchezo wa kulipua jengo la Uwekezaji Nairobi na kufahamisha umma kuhusu mifuko mingine kutaka kutumika. Sasa naona mmeanza kuona NSSF inaelekea kupata faida kubwa na hivyo sifa kwa utawala wake mnaanza kushambulia watu wanaotazama mema ya nchi. Siasa wekeni kando na kamwe cha juu hamtapata kwa kuwa NSSF hatutoi rushwa.

Narudia sisi ni zero corruption zone na Hosseah anajua. Zitto achana na hawa

Una hakika? Unajua kuwa Manji alikopa kwenu akakarabati jengo kwa mkopo wenu halafu akawauzia tena kwa bei mbaya?Hii sio corruption? Halafu nani kakwambia Hosea ndio barometer ya kupimia corruption nchini? Huyu si alisema Richmond haina tatizo? Karibu JF uelimike......
 
Bila nguvu ya umma hata sioni tutatokaje kwenye hili janga la ufisadi ambalo limetanda serikalini na bungeni. Ndo maana wananchi wakiandamana kidogo tu mafisadi wanapatwa na matumbo ya kuhara
 
Mh. mzito yuko sawa kwa maana ya kuondoa tatizo sugu la umeme tz. na nssf ni sawa kupewa mradi wa kiwira lkn iwe kitu cha kweli. kama kiwira ina mgogoro waende steagler gouge watupe umeme wa uhakika. wakati uganda wanajitayarisha kuchimba mafuta sisi tunashindana jinsi ya kuiba rasilimali za taifa. aibu kwa Watanganyika. hebu tujadili vitu vya maana. hawa tunawaita mafisadi watafika mwisho na siku si nyingi. Mh. Zitto ameingia choo ya kike ATATOKAJE?
 
"ukishakkula nyama ya binadamu basi ili uache kuila yahitaji ujasiri" sasa sishangai yanayofanywa na Zitto,kwani huko alikoamua kuwa lazima kumshinde kutoka.Hapa hakuna maslahi ya Taifa
 
Umeme ni idara pekee duniani inayofanya kazi kwa HASARA. Ndiyo maana karibu kila sehemu duniani, Serikali za nchi hizo huwa zinasaidia kulipia gharama baadhi ili kupunguza makali yake.


Kuna miradi NSSF wanaweza kujiingza na wakapata faida ila siyo kuzalima Umeme, Maji, Usafiri wa Reli ......

Wamenikatia umeme sasa hivi. Laptop ikiishiwa charge, nimedoda.

Pole sana Mkuu,

Subiri kidogo Kiwira ianze kazi....:juggle:
 
Naelewa kuwa NSSF wana jukumu kubwa sana la kuhifadhi jamii ya kitanzania. Tanesco hawana vyanzo vingine vya nishati zaidi ya Maji ya mwenyezi Mungu akitunyima kilio. Kwann tusiwape TANESCO chanzo kingine ambacho ni Kiwira?!!! Tatizo, baada ya Tanesco kulifanya shamba la bibi na kulirundikia lundo la madeni kutokana na wanasiasa wetu kula bila kunawa, wameanza kulinyemelea shirika lingine la umma NSSF. NSSF imetuna wanajaribu mbinu za kula,ili wanachama wa mfuko huo baadaye wasipate lolote kwa ajili ya fedha zao halali kwani litakuwa taabani.
 
Wakuu, nadhani mpango wa NSSF kununua Kiwira haukuanzishwa na Mh. Zitto, mbona hatuwasakami hao hao NSSF wanaotaka kuwekeza kwenye mradi wa kujenga bomba la gesi toka Mtwara kwenda Mombasa na Mwanza?, mradi wa kujenga UDOM, magorofa ya Mchikichini, daraja la Kigamboni etc, etc, etc...

Mimi si msemaji wa mh. Zitto isipokuwa naamini kabisa yeye binafsi amekuwa mshabiki wa suala hili kutokana na performance ya NSSF kwenye miradi yao mingine waliyokwisha fanya.

Pia imani yake inaweza kuwa inachangiwa na uwezo wa kifedha wa NSSF ukilinganisha na wawekezaji wengine ambao malengo yao makubwa ni kuchota pesa za mradi badala ya kuwekeza pesa. Mfano mzuri ni hiyo kampuni iliyoshindwa hapo Kiwira iliyokuwa ikimilikiwa na comradi Nkapa....

Mwisho nawaombeni tumuache kijana afanye kazi...ingawaje kumkosoa ni vizuri lakini ingekuwa vizuri zaidi kumkosoa pale alipo haribu na sio kumfuatilia kwa kila jambo. Kwanza kumbukeni huyu ni member mwezetu hapa jamvini, tusimfanye achukie na mwisho ajitoe jamvini...:washing:

Philosophy ya huyu ni mwenzetu is at work, ndio maana tupo bottom kwenye list ya maendeleo.
 
Sitaki kukumbusha mambo yaliyopita lakini, uelewe jina lako limekua sana kwa kuwa wananchi wengi tuliamini una nia ya dhati ya kuondoa ufisadi unaokumbatiwa na serikali ya JK.

Siku za karibuni umekuwa unatoa matamko na kufanya vitendo vingi ambavyo vinawashtua wengi wetu na kujikuta wanahoji udhati wako katika kuwahudumia walio wengi na maskini. Sihitaji kukukumbushia maana unayajua na baadhi umeyatolea maelezo japo bado unaendelea kushutumiwa.

Leo nakupa ushauri wangu, tena bure na kukuonya. RA, JK na EL watakutumia sasa hivi na fedha utapata sana tu, kamatini, Bungeni kawaida, nk. Inawezekana ukawa miongoni mwa matajiri wakubwa sana miongoni mwa mafisadi uliopanda ngazi kwa kuwashambulia kama Karamagi na Lowasa. Ninachojaribu kukwambia hapa Kaka, ni kwamba jiangalie sana. TISS wanalinda watawala na si nchi. Ingekuwa nchi ufisadi wote mkubwa usingetokea kwa kuwa wana macho yaliyo-trainiwa kuona na ni wazi waliona lakini, haikuwa issue kwao.

Kubali kataa wewe ni silaha tu kwao. Utatumika leo kudhoofisha chama chako na walalamikaji wengine na mwishowe watakuacha hapo. CCM ilipofikia si wakati wa kina Tambwe, Wasira, Lamwai wala wengine waliofanikiwa kutukana weee na mwishowe wakapokelewa kundini walipoamua kurejea. Wewe kuna baadhi watakukataa maana tayari kuna wanaokuona Mzandiki kwa kujipendekeza kwa Mwenyekiti wao na kumpelekea majungu dhidi yao. Wanakujua na wakipata nguvu kidogo tu dhidi ya RA ujue huna chako.

Haya mambo unayojaribu kuyatetea wakati huu kama mitambo ya DOWANS, Kiwira nk wengi hatuelewi kama ni kweli una nia ya kusaidia kupatikana kwa umeme tu au unahangaikia posho yako na ahadi za RA.

Kama nia yako ni safi namwomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema akubariki sana na ndoto yako ya kuwa rais itimie mapema kuliko unavyotamani. But... kama umenunuliwa kweli (kwa fedha na ahadi) halafu unatumia mbinu hizo ili kuwaumiza wanyonge kwa maslahi yako binafasi kisiasa na kiuchumi, Zitto my Bro. nakwambia utaporomoka vibaya na utaona haya hata kuwasalimia wapiga kura wako.

I am sure (and I pray) Mwenyezi Mungu atakuadhibu kwa nguvu zote pale utakapokuwa umewahadaa wananchi walio wengi tena wanyonge na walioamini utawatetea kwa kuwa tu kuna fedha zaidi katika usaliti huo kuliko kule ulikoanzia.

Jiulize swali, Unadhani kwa fedha za mafisadi pasipo wananchi wanyonge lakini wenye matumaini na wewe Bunge ungeliona? Huoni kama wangepewa T-Shirt zao, kanga na kofia na kukutupilia mbali tangu mwanzo.

Nakuomba sana Zitto, please please jitafiti na ufikirie upya hiyo safari yako. Upande uliochagua ni mgumu kwako kuliko upande wa wanyonge. Amini usiamini utafail wakati you least expect.
 
Umeongea kwa uchungu sana na naamini mhusika kakuelewa. Ila inaonekana unayafaham mengi kuhusu Zitto ila haujayasema hapa!!??
 
Don't waste your time on this guy, sisi wengine hapa ni marafiki wakubwa wa huyu bwana na ni mwezi December tu mwaka jana tumemkalisha kitako juu ya masuala mengi sana tu na tukakubaliana.

Hivi leo kukifunuliwa chungu alichokifunika Kabwe uvundo utakaofumuka mle hata mama yake mzazi hatoamini kwamba kweli ni yeye tena ndani ya fukuto ambalo safari hii si kwa sauti pinzani ndani ya CHADEMA TU bali hadi dhidi ya vinara wa nndani ya vikundi mbali mbali ndani ya CCM yenyewe.

Huyu mwenzetu ni sikio la kufa eti kaambiwa anapewa uenyekiti wa kamati ili apate fedha za kutosha aje ajitokeze kugombea urais CHADEMA na mwisho kucheza kucheza KAMARI YA KALONZO MUSYOKA WA KENYA kwa kujipenyeza kati na kupewa eti Uwaziri Mkuu huku Lowassa akijimegea urais kwa wao kuunda serikali ya mseto.

Lakini hayo yote si vibya akajibembeleza roho yake kwa kuota ndoto mchana mchana tu, JAMBO LA HATARI ZAIDI HAPA NI UWEPO WAKE KWA MARA NYINGINE kwenye biashara ya KUFIKIRIA KUSHIRIKI KUCHUUZA DAMU YA BAADHI YA SAUTI PINZANI NCHINI (mpaka sasa ni wa 15) na baadhi ya wana-JF tukiwemo.

Zitto, Zitto, Zitto toka huko, Zitto achana na na tabia zako za kusimama mbele ya wanachokipenda umma wa Tanania lakini nyinyi hamipendi. Zitto huwezi kamwe kumfanya Lowassa awe rais kwa janja zozote bila Wa-Tanzania kuridhi kitu hapo.

Zitto ulizaliwa uchi ukaikuta fedha, nguo, magari na nyumba nzuri dunia na siku ya kuondoka kwako ahera hutoenda na chochote. Acha hizo tamaa za Lowassa ambaye tayari anaamini hela zake na za Rostam Aziz ni USAFIRI TOSHA KUFIKIA URAIS hata bila kuhitaji Wana-CCM wenzake.

Na ninasema kwa uchungu kwa taifa la Tanzania linawaangalia kila mlitendalo; Zitto, Makamba na Lowassa tunasema Tanzania inalia, wanyonge tunalia; wazee jamvi sasa tunalikunja!!!
 
It is hard to let this thread pass. For the love of JF, CDM and Zitto I will sit on the rails and watch.

Gone are the days when Zitto was Daruso Prime Minister (he remains to be the first Daruso PM) and Albert the Speaker.....age has caught with us. And so many things more.

I am all ears and eyes!
 
Morality is of the highest importance - but for us, not for God. Let our brother Zitto be guided by God's wisdom accordingly.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom