Zitto: Hali ya uchumi ya watu wetu hapa Tanzania ni mbaya sana

Demokrasia na Ustawi wa Taifa: Tunaendelea kusisitiza rai yetu kuhusu umuhimu wa kuitisha Mkutano wa Kitaifa wa Maridhiano ya Kisiasa kama jukwaa la kuzijadili changamoto za uendeshaji wa siasa nchini. Jambo hilo litaondoa uadui unaoendelea kukua sasa kati ya Serikali na wananchi, viongozi wa dini, mashiriki yasiyo ya Kiserikali, taasisi za wanafunzi, pamoja na vyama vya Upinzani. Tunaamini mazungumzo ya Kitaifa ndio jambo sahihi la utatuzi wa suala hili.


Hiyo hapo nimeipenda
 
Tunahitaji mawazo tofauti ili nchi iendelee, ila kinachoshangaza nchi hii mawazo ya kiongozi fulani ndio hupigiwa chapuo na kusimamiwa yasikosolewe. Hii sio Demokrasia, kama vyama vya siasa mtashindwa kulipinga hili basi mawazo yenu kama haya yatabaki kwenye makashabrasha na umasikini utaendelea kushamiri.
 
Back
Top Bottom