Haijapata kutokea ila imetokea sasa ndio maana tunawasifu na kuwaunga mkono viongozi wetu

MTANZANIA620

Member
Jun 20, 2023
34
30
Tangu mwaka 1995 Jimbo la Vunjo limepata kuongozwa na wabunge wafuatao:-

1. 1995 - 2000 Mhe. James Francis Mbatia (NCCR MAGEUZI)

2. 2000 - 2005 Mhe. Meja Jesse Jeremiah Makundi (TLP)

3. 2005 - 2010 Mhe. Aloyce Bent Kimaro (CCM)

4. 2010 - 2015 Mhe. Augustine Lyatonga Mrema (TLP)

5. 2015 - 2020 Mhe. James Francis Mbatia (NCCR MAGEUZI)

6. 2020 Mpaka sasa Mhe. Dkt Charles Stephen Kimei (CCM)

Jimbo la Vunjo limeongozwa na upinzani kwa miaka ishirini tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

Tukifanya uchambuzi kwa tuliobahatika kuona utendaji kazi wa wabunge wote hawa basi bila shaka yoyote tutakubaliana ya kwamba kipindi hiki kazi kubwa imefanyika kuliko wakati wowote ule huko nyuma.

Kwa muda wa miaka mitatu ambayo CCM imepewa ridhaa ya madiwani katika kata zote 16, Mbunge Dkt Charles Stephen Kimei na Rais Dkt SAMIA Suluhu Hassan yaliyofanyika katika Jimbo la Vunjo ni maajabu kabisa.

Ndiyo sababu tunawashukuru na kuwasifu viongozi wetu kwa maana ya madiwani, Mbunge wetu Dkt Charles Stephen Kimei pamoja na Rais wetu Mhe Dkt SAMIA Suluhu Hassan kwa kazi kubwa za maendeleo zilizofanyika ikiwa ni utekelezaji wa vitendo wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025. CCM Ikiahidi inatekeleza.

Katika kipindi cha miaka mitatu mpaka sasa tumepata miradi mingi ya maendeleo kama vile:-

1. Shule mpya ya sekondari kata ya Njiapanda shilingi milioni 470

2. Shule chakavu za msingi Msufini, Mrumeni na Mulo kuvunjwa madarasa 6-7 na kujengwa upya

3. Ujenzi wa shule mpya ya msingi Darajani kata ya Njiapanda

4. Ujenzi wa zahanati mpya na uboreshaji wake zipatazo 12 ambazo ni Kochakindo na Ghona (Kata ya Kahe Mashariki), Legho Mulo (Kata ya Kilema Kusini) , Mabungo (Kirua Vunjo Kusini) Matala (Kata ya Mwika Kusini), Kileuo (Kata ya Kirua Vunjo Mashariki), Kisao (Kata ya Kilema Kati), Njiapanda (Kata ya Njiapanda) nk

5. Ujenzi na upanuzi wa vituo vya afya vinne ambavyo ni Marangu Hedikota (kata ya Marangu Mashariki), Kirua Vunjo (Kata ya Kirua Vunjo Magharibi), Kahe (Kata ya Kahe Magharibi) na Koresa (Kata Kirua Vunjo Kusini) ambacho kiko mbioni kuanza.

6. Miradi ya maji safi
- Mradi mkubwa wa maji toka miwaleni kwenda Njiapanda uliogharimu shilingi bilioni 2.3 umekamilika na unatoa huduma kupitia MUWSA

- Mradi mkubwa wa maji unaogharimu shilingi bilioni 2.1 na pindi utakapokamilika utahudumia kata mbili za Marangu Magharibi (vijiji vyote 7) na Marangu Mashariki (vijiji 4) ambapo jumla ya vijiji 11 vitanufaika Mradi umefikia hatua 70 ya utekelezaji kupitia RUWASA

- Mradi mkubwa wa uboreshaji huduma ya maji kata ya Mwika Kaskazini vijiji vyote 6 unaogharimu shilingi bilioni 1.7 kwa sasa mradi unaendelea na upo asilimia 50 ya utekelezaji wake kupitia MUWSA

- Mradi wa uboreshaji upatikanaji wa maji katika kata za Kilema Kaskazini, Kilema Kati na Kilema Kusini uliogharimu shilingi millioni 567 kupitia RUWASA, mradi umekamilika na unatoa huduma

- Mradi wa uboreshaji upatikanaji wa maji katika kata ya Kirua Vunjo kusini unaogharimu shilingi millioni 576 na pindi utakapokamilika utahudumia vitongoji vyote vya kijiji cha Yamu Makaa. Kwa sasa mradi upo asilimia 25 za utekelezaji na kazi zinaendelea

- Mradi mkubwa wa uboreshaji upatikanaji wa maji, uchimbaji wa kisima na ujenzi wa tenki kubwa la maji katika kata ya Mwika Kusini shilingi millioni 800. Mradi wa ulazaji mabomba umeanza na unaendelea. Pia maandalizi na taratibu za kuanza uchimbaji wa kisima zimekamilika, wakati wowote kazi itaanza kupitia MUWSA kati ya Aprili na Mei.

7. Upanuzi wa daraja la Marangu Mtoni, matengenezo na ujenzi wa barabara yamefanyika kwa ukubwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Jimbo hili.

8. Uboreshaji wa upatikanaji wa umeme pamoja na usambazaji wa umeme kwa wananchi kupitia REA na TANESCO kazi hiyo imefanyika kwa ukubwa na inaendelea

9. Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji ikiwemo mifereji kama vile Ndokombeka, Masaera, Samanga, Mboni, Mananga na Masaga pamoja na skimu za umwagiliaji za Mawala na Soko kazi ambazo zitaanza kufanyiwa kazi kabla ya Juni, 2024

10. Kupitia ufadhili wa shirika la HelpUp toka Israel shule takribani 26 zimefanyiwa ukarabati mkubwa wa wastani wa shilingi millioni 25 kwa kila shule.

11. Ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za watumishi, hosteli, mabwalo ya chakula, majengo ya TEHAMA, Maktaba, Maabara, upatikanaji wa vitabu kwa shule za msingi na sekondari pamoja na vifaa vya maabara kwa shule za msingi na sekondari

12. Upatikanaji wa gari la wagonjwa (Ambulance)

13. Ujenzi na ukarabati mkubwa wa vyoo katika masoko kama vile Marangu Mtoni, Himo, Lyamwombi na Rindima. Sasa tunakaenda kuanza uboreshaji Mwika na Kisambo.

14. Ujenzi wa vivuko vya watembea kwa miguu na bodaboda kama vile Mshiri, Yamu - Uparo, Lekura - Mkolowony nk

15. Mradi wa uhimilishaji ng'ombe bure kwa maana ya kuchoma homoni na kupandikiza mbegu wafugaji zaidi ya 750 walinufaika katika kata zote 16.

16. Mradi wa ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara, majengo ya utawala na matundu ya vyoo kwa ajili ya kuanzisha kidato cha 5&6 katika shule za sekondari za Mangoto (Kata ya Kahe) na Himo (Kata ya Makuyuni). Mradi huu unagharimu shilingi milioni 984 mpaka utakapokamilika.

17. Mradi wa ukamilishaji wa daraja la Sembeti - Samanga kata ya Marangu Mashariki lililoanza kujengwa miaka 16 iliyopita utaanza wakati wowote mwanzoni mwa Aprili, 2024 maana limeshapata fedha za kulikamilisha shilingi millioni 103.

18. Uwezeshaji vikundi vya wajasiriamali kwa nyenzo na mitaji

19. Kuchezeshwa Ligi ya soka vijana katika kila mwaka na Bingwa amekuwa akijinyakulia shilingi millioni 3 pamoja na kualikwa bungeni

20. Ujenzi wa sekondari mpya ya Pumuani kata ya Kirua Vunjo Kusini

21. Mradi wa taa za usiku kata ya Njiapanda

Kwa mambo haya katika kipindi cha miaka takribani mitatu kwanini tusiwasifu viongozi wetu?

Safari ya maendeleo bado inaendelea, hayo ni baadhi kati ya mengi yaliyofanyika na yanayoendelea. Tuendelee kuwapa ushirikiano Madiwani, Mbunge wa Jimbo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei na Rais Mhe Dkt SAMIA Suluhu Hassan ili kuijenga Vunjo tunayoitamani ambayo sote tutaona fahari kupaita nyumbani.

IMG_20240404_125437_069.jpg
IMG_20240405_140822_604.jpg
IMG_20240405_141028_201.jpg
IMG-20240325-WA0080.jpg
IMG-20240325-WA0045.jpg
IMG-20240325-WA0075.jpg
IMG-20240220-WA0023.jpg
IMG-20240220-WA0031.jpg
FB_IMG_1708258121989.jpg
IMG_20240217_133150_334.jpg
IMG_20240216_125632_298.jpg
IMG-20240208-WA0055.jpg
IMG_7451.JPG
IMG_7708.JPG
IMG_7615.JPG
IMG_7588.JPG
IMG_7569.JPG
DSC_0065.JPG
 
Dr Kimei Jiwe alimdanganya atampa alipo Mwigulu sasa hivi na aliamini kabisa ila hatasau kilichotokea. Ni kabila lake tu ndo lililomuangusha.
kama alifata iwaziri sio sawa ila kama alifata kutumikia nchi alikua sahihi.

leo nasoma uzi huu kwa mengi mazuri anayofanya jimboni kwake pengine angekua waziri asingepata muda mzuri wa kutumikia jimbo lake.🙏
 
Sema kuwatumia wabunge kama mawaziri sio sahihi ni sawa na kuzorotesha utendaji kazi kweny majimbo yao ... Kaangalie Jimbo la Makamba kumeoza hata hawamjui kwanza nyumba yake kajenga huko Dodoma wala hafiki.

Wakina Aweso barabara miaka 5 haikamiliki yuko busy kupeleka maji Dodoma ,yaani usiombe Mbunge wako awe waziri ni tabu tupu ...Anajiona wizara ndio imempeleka bungeni.
 
Serikali inatutoza sana kodi ilitakiwa kufanya yooote hayo miaka 40 iliyopita. Poleni sana mmedumazwa na serikali yenu na kupotezewa muda mmmno,wapingeni sana walikuwa wanaongoza serikali!!
Kwakuwa wajinga niwengi sasahivi mnadhani hiyo ni hisani wakati mmecheleweshewa saana maendeleo na SERIKALI bila kujali mbunge ninani ama ni chama gani!!
Kusema vinginevyo maana yake nchi hii Kuna ubaguzi mkubwa wa kiitikadi nk ambao ni hatari Kwa amani na ustawi wa taifa!!
Tuelimikeee....
 
Mwika kusini kukipata hilo tank la maji kabla ya 2025 uchaguzi..kura yangu nitampa Kimei!
 
Sema kuwatumia wabunge kama mawaziri sio sahihi ni sawa na kuzorotesha utendaji kazi kweny majimbo yao ... Kaangalie Jimbo la Makamba kumeoza hata hawamjui kwanza nyumba yake kajenga huko Dodoma wala hafiki.

Wakina Aweso barabara miaka 5 haikamiliki yuko busy kupeleka maji Dodoma ,yaani usiombe Mbunge wako awe waziri ni tabu tupu ...Anajiona wizara ndio imempeleka bungeni.
Tanga kuna Umaskini wa kutupwa

Uchawi
 
Tangu mwaka 1995 Jimbo la Vunjo limepata kuongozwa na wabunge wafuatao:-

1. 1995 - 2000 Mhe. James Francis Mbatia (NCCR MAGEUZI)

2. 2000 - 2005 Mhe. Meja Jesse Jeremiah Makundi (TLP)

3. 2005 - 2010 Mhe. Aloyce Bent Kimaro (CCM)

4. 2010 - 2015 Mhe. Augustine Lyatonga Mrema (TLP)

5. 2015 - 2020 Mhe. James Francis Mbatia (NCCR MAGEUZI)

6. 2020 Mpaka sasa Mhe. Dkt Charles Stephen Kimei (CCM)

Jimbo la Vunjo limeongozwa na upinzani kwa miaka ishirini tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

Tukifanya uchambuzi kwa tuliobahatika kuona utendaji kazi wa wabunge wote hawa basi bila shaka yoyote tutakubaliana ya kwamba kipindi hiki kazi kubwa imefanyika kuliko wakati wowote ule huko nyuma.

Kwa muda wa miaka mitatu ambayo CCM imepewa ridhaa ya madiwani katika kata zote 16, Mbunge Dkt Charles Stephen Kimei na Rais Dkt SAMIA Suluhu Hassan yaliyofanyika katika Jimbo la Vunjo ni maajabu kabisa.

Ndiyo sababu tunawashukuru na kuwasifu viongozi wetu kwa maana ya madiwani, Mbunge wetu Dkt Charles Stephen Kimei pamoja na Rais wetu Mhe Dkt SAMIA Suluhu Hassan kwa kazi kubwa za maendeleo zilizofanyika ikiwa ni utekelezaji wa vitendo wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025. CCM Ikiahidi inatekeleza.

Katika kipindi cha miaka mitatu mpaka sasa tumepata miradi mingi ya maendeleo kama vile:-

1. Shule mpya ya sekondari kata ya Njiapanda shilingi milioni 470

2. Shule chakavu za msingi Msufini, Mrumeni na Mulo kuvunjwa madarasa 6-7 na kujengwa upya

3. Ujenzi wa shule mpya ya msingi Darajani kata ya Njiapanda

4. Ujenzi wa zahanati mpya na uboreshaji wake zipatazo 12 ambazo ni Kochakindo na Ghona (Kata ya Kahe Mashariki), Legho Mulo (Kata ya Kilema Kusini) , Mabungo (Kirua Vunjo Kusini) Matala (Kata ya Mwika Kusini), Kileuo (Kata ya Kirua Vunjo Mashariki), Kisao (Kata ya Kilema Kati), Njiapanda (Kata ya Njiapanda) nk

5. Ujenzi na upanuzi wa vituo vya afya vinne ambavyo ni Marangu Hedikota (kata ya Marangu Mashariki), Kirua Vunjo (Kata ya Kirua Vunjo Magharibi), Kahe (Kata ya Kahe Magharibi) na Koresa (Kata Kirua Vunjo Kusini) ambacho kiko mbioni kuanza.

6. Miradi ya maji safi
- Mradi mkubwa wa maji toka miwaleni kwenda Njiapanda uliogharimu shilingi bilioni 2.3 umekamilika na unatoa huduma kupitia MUWSA

- Mradi mkubwa wa maji unaogharimu shilingi bilioni 2.1 na pindi utakapokamilika utahudumia kata mbili za Marangu Magharibi (vijiji vyote 7) na Marangu Mashariki (vijiji 4) ambapo jumla ya vijiji 11 vitanufaika Mradi umefikia hatua 70 ya utekelezaji kupitia RUWASA

- Mradi mkubwa wa uboreshaji huduma ya maji kata ya Mwika Kaskazini vijiji vyote 6 unaogharimu shilingi bilioni 1.7 kwa sasa mradi unaendelea na upo asilimia 50 ya utekelezaji wake kupitia MUWSA

- Mradi wa uboreshaji upatikanaji wa maji katika kata za Kilema Kaskazini, Kilema Kati na Kilema Kusini uliogharimu shilingi millioni 567 kupitia RUWASA, mradi umekamilika na unatoa huduma

- Mradi wa uboreshaji upatikanaji wa maji katika kata ya Kirua Vunjo kusini unaogharimu shilingi millioni 576 na pindi utakapokamilika utahudumia vitongoji vyote vya kijiji cha Yamu Makaa. Kwa sasa mradi upo asilimia 25 za utekelezaji na kazi zinaendelea

- Mradi mkubwa wa uboreshaji upatikanaji wa maji, uchimbaji wa kisima na ujenzi wa tenki kubwa la maji katika kata ya Mwika Kusini shilingi millioni 800. Mradi wa ulazaji mabomba umeanza na unaendelea. Pia maandalizi na taratibu za kuanza uchimbaji wa kisima zimekamilika, wakati wowote kazi itaanza kupitia MUWSA kati ya Aprili na Mei.

7. Upanuzi wa daraja la Marangu Mtoni, matengenezo na ujenzi wa barabara yamefanyika kwa ukubwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Jimbo hili.

8. Uboreshaji wa upatikanaji wa umeme pamoja na usambazaji wa umeme kwa wananchi kupitia REA na TANESCO kazi hiyo imefanyika kwa ukubwa na inaendelea

9. Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji ikiwemo mifereji kama vile Ndokombeka, Masaera, Samanga, Mboni, Mananga na Masaga pamoja na skimu za umwagiliaji za Mawala na Soko kazi ambazo zitaanza kufanyiwa kazi kabla ya Juni, 2024

10. Kupitia ufadhili wa shirika la HelpUp toka Israel shule takribani 26 zimefanyiwa ukarabati mkubwa wa wastani wa shilingi millioni 25 kwa kila shule.

11. Ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za watumishi, hosteli, mabwalo ya chakula, majengo ya TEHAMA, Maktaba, Maabara, upatikanaji wa vitabu kwa shule za msingi na sekondari pamoja na vifaa vya maabara kwa shule za msingi na sekondari

12. Upatikanaji wa gari la wagonjwa (Ambulance)

13. Ujenzi na ukarabati mkubwa wa vyoo katika masoko kama vile Marangu Mtoni, Himo, Lyamwombi na Rindima. Sasa tunakaenda kuanza uboreshaji Mwika na Kisambo.

14. Ujenzi wa vivuko vya watembea kwa miguu na bodaboda kama vile Mshiri, Yamu - Uparo, Lekura - Mkolowony nk

15. Mradi wa uhimilishaji ng'ombe bure kwa maana ya kuchoma homoni na kupandikiza mbegu wafugaji zaidi ya 750 walinufaika katika kata zote 16.

16. Mradi wa ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara, majengo ya utawala na matundu ya vyoo kwa ajili ya kuanzisha kidato cha 5&6 katika shule za sekondari za Mangoto (Kata ya Kahe) na Himo (Kata ya Makuyuni). Mradi huu unagharimu shilingi milioni 984 mpaka utakapokamilika.

17. Mradi wa ukamilishaji wa daraja la Sembeti - Samanga kata ya Marangu Mashariki lililoanza kujengwa miaka 16 iliyopita utaanza wakati wowote mwanzoni mwa Aprili, 2024 maana limeshapata fedha za kulikamilisha shilingi millioni 103.

18. Uwezeshaji vikundi vya wajasiriamali kwa nyenzo na mitaji

19. Kuchezeshwa Ligi ya soka vijana katika kila mwaka na Bingwa amekuwa akijinyakulia shilingi millioni 3 pamoja na kualikwa bungeni

20. Ujenzi wa sekondari mpya ya Pumuani kata ya Kirua Vunjo Kusini

21. Mradi wa taa za usiku kata ya Njiapanda

Kwa mambo haya katika kipindi cha miaka takribani mitatu kwanini tusiwasifu viongozi wetu?

Safari ya maendeleo bado inaendelea, hayo ni baadhi kati ya mengi yaliyofanyika na yanayoendelea. Tuendelee kuwapa ushirikiano Madiwani, Mbunge wa Jimbo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei na Rais Mhe Dkt SAMIA Suluhu Hassan ili kuijenga Vunjo tunayoitamani ambayo sote tutaona fahari kupaita nyumbani.

View attachment 2955982View attachment 2955983View attachment 2955984View attachment 2955985View attachment 2955986View attachment 2955987View attachment 2955988View attachment 2955989View attachment 2955990View attachment 2955991View attachment 2955992View attachment 2955993View attachment 2955994View attachment 2955995View attachment 2955996View attachment 2955997View attachment 2955998View attachment 2955999
Kama hamuweki lami ile barabara ya kwenda Kilema Hospitali hamtakuwa mmewatendea haki wananchi
 
Ujinga tu. Kwani kipindi chote hicho serikali ilikuwa imeundwa na chama gani?

Hujui kuwa mkusanya Kodi na mtekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wananchi ni serikali? Mbunge anakusanya Kodi? Mbunge ni mwakilishi tu (mesenja) wa wananchi. Jinga kabisa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom