Zitto amkaribisha Kafulila CHADEMA

kwani huyu kafulila hana haki ya kukata rufaa mahakamani? grounds anazo nyingi sana ikiwemo mamluki waliochahaguliwa na mbatia kwani alisahwapnga kumkataa,mbatia kawa a judge on his own course.

pili tuhuma zake zimethibitishwa pasipo kuacha mashaka??? walifikiria wananchi waliomchagua? kwanii wasiige kwa wenzao magamba
¨kule hata uwe fisadi mla watu haufukuzwi chama unaambiwa vua gamba iweje chama chenye wabunge wawili watatu wamtimue uanachama huku wakijua wanapoteza mbunge na ruzuku itapunguzwa??

huyu mchaga kadata kabisa kaniudhi sana,Kafulila hebu rudi kasulu pale nunua radi ya sh 20 tuma kwa mahasimu wako. Waambie ni kwanii Malecela haendi Kigoma.
Ni kweli kwa Tanzania ana haki ya kwenda mahakamani lakini hana haki ya kurudi na ushindi, hata kama akirudi na ushindi itakuwa very late 2015 mwezi mmoja kabla ya bunge kuvunjwa rasmi.
 
Ni kweli kwa Tanzania ana haki ya kwenda mahakamani lakini hana haki ya kurudi na ushindi, hata kama akirudi na ushindi itakuwa very late 2015 mwezi mmoja kabla ya bunge kuvunjwa rasmi.
Akienda mahakamani si bado anakuwa mbunge? Mpaka mahakama ihalalishe?
 
Mbowe ametoa angalizo kwa Mbatia kutumia busara kwenye suala la Kafulila ili kuepuka ,kurudia uchaguzi ambapo ni gharama na matumizi Mabaya ya Kodi za wananch wakati Wafanyakazi wanakosa Mishahara kwa wakati!.source Majira Leo.
 
Kama mwananchi mchangia kodi ningependa kujua kiini cha tatizo lililomfanya kafulila apigwe chini?
Kwa wanaojua naomba msaada kujulishwa
 
Naanza kupata hisia hoja ya Magamba kufuta Chaguzi ndogo kupata nguvu zaidi. Lets wait and see.
 
Jamani uchumi wa nchi yetu hivi sasa tunavyoingia mwaka mpya 2013 ni tete kuliko unavyoweza kufikiri. Pengine tukikuwekea ushahidi hapa, kama ni kigogo pengine tutakusikia tena tu hospitali ya Apollo kule India. Usipime kaka!!!
 
Naanza kupata hisia hoja ya Magamba kufuta Chaguzi ndogo kupata nguvu zaidi. Lets wait and see.

Hii hoja hina nguvu kabisa. Gharama za uchaguzi zinakuzwa na vyama husika hasa katika kuhonga wapiga kura na kuweka mikakati ya kuiba kura. Mfano huu wa kafulila ni muhimu sana hasa pale chama kinapomuona mbunge kuwa anakipinga.

CCM wanapendekeza mfumo wa cham kuteua mtu mbadala. Sakata hili maana yake ni kuwa Mtu anaweza fukuzwa kama Kafulila na mwingine kuteuliwa.

Kuna njia za kuepuka chaguzi ndogo na moja wapo ni kuwa na mgombea huru, na hata mbunge akifukuzwa chama bado anatakiwa aendelee na ubunge wake maana aliyechaguliwa ni yeye si chama.
 
Swala la Kafulila linaonyesha jinsi gani sheria ya mgombea binafsi ni ya muhimu sana nchini kwetu. Sasa hivi jambo linaloonekana mbele yetu hapa ni la watu wawili waliogombea Ubunge katika majimbo yao; mmoja akashinda na mwingine akashindwa. Sasa yule aliyeshindwa akatokea kuwa ni mwenyekiti wa chama kilichowasimamisha wagombea hao wawili. Kutokana na uneyeyekiti wake, anaamua kumvua unachama mbunge aliyechaguliwa na wanachi kwa kujua kuwa hatua hiyo itamvua ubunge pia.

Kwa wenzetu kama Marekani, mtu unaweza kuchaguliwa kwa kupitia chama kimoja halafu ukaamua kuachana nacho na kuingia chama kingine kama vile alivyofanya Senator Arlen Spector alipohama kutoka Republican na kujiunga na Democrat. Utaratibu wetu unaonyesha jinsi gani wapiga kura wetu wasivyokuwa na sauti, kwani mgombea wao waliyempigia kura anaweza kuvuliwa kiti chake kirahisi tu kwa vile eti hakubaliani na mwenyekiti wa chama chake. Na hiyo ndiyo tabia mbaya tunayotaka ikomeshwe mara moja kusudi wabunge wetu wasitumike kama rubber stamp tu.

Kama Mbatia anaona kuwa hatua aliyochukua dhidi ya mbunge Kafulila ni sawa, je atawakemea nini wabunge wa CCM wakiamua kukubaliana na kila upupu unaoletwa na serikali bungeni ilihali serikali hiyo inaongozwa na mwenyeketi wao ambaye akitumia madaraka yake kama Mbatia alivyoyatumia anaweza kuwafukuza wote kutoka ndani ya CCM na hivyo kupoteza ubunge wao?

Kwa kumbuku,bu yangu kama mwalimu wake ninajua kuwa Mbatia alikuwa na mapungufu mengi sana wakati akiwa kiongozi wa wanafunzi pale UDSM mwishoni mwa miaka ya themaninini ila nilitegemea kuwa ulikuwa ni utoto wakati ule na baada ya kuingia kwenye siasa angebadilisha tabia yake na mapugufu hayo. Inaonekana wazi kuwa theory ya evolution haifanyi kazi hapa: na nyani hawezi kugeuka kuwa binadamu.
 
Hii yani bora angeshauri mtu mwingine kwa ninavyomjua James ushauri kama umetoka kwa Free hata kama ni mzuri vipi kutokana na ma biff yao ya kitoto hawezi kuukubali...
 
Anarudi kufanya nini wakati alisema CDM ni chama cha kikanda?faida ya kuropoka ndio hiyo.Kama alipiga magoti kwa Mbatia basi awapigie magoti wana CDM kwa maneno yake ya kebehi ili asamehewe.Bado yeye ni kijana mpambanaji ila tuu nidhamu ni ziro.

sisimizi hatakiwi cdm
 
Jamani uchumi wa nchi yetu hivi sasa tunavyoingia mwaka mpya 2013 ni tete kuliko unavyoweza kufikiri. Pengine tukikuwekea ushahidi hapa, kama ni kigogo pengine tutakusikia tena tu hospitali ya Apollo kule India. Usipime kaka!!!

mkuu,

mbona una forward miaka au unahamu 2015 ifike haraka
 
habari za uhakika ambazo mimi tu naweza kuzithibitisha, Mbowe na Mbatia (hawa ni homeboys) walikuwa na mazungumzo marefu sana kwa njia ya simu ya kutaka kujaribu kutuliza hali ya upepo mbaya kwa kafulila. Tusubiri tuone
 
Swala la Kafulila linaonyesha jinsi gani sheria ya mgombea binafsi ni ya muhimu sana nchini kwetu. Sasa hivi jambo linaloonekana mbele yetu hapa ni la watu wawili waliogombea Ubunge katika majimbo yao; mmoja akashinda na mwingine akashindwa. Sasa yule aliyeshindwa akatokea kuwa ni mwenyekiti wa chama kilichowasimamisha wagombea hao wawili. Kutokana na uneyeyekiti wake, anaamua kumvua unachama mbunge aliyechaguliwa na wanachi kwa kujua kuwa hatua hiyo itamvua ubunge pia.

Kwa wenzetu kama Marekani, mtu unaweza kuchaguliwa kwa kupitia chama kimoja halafu ukaamua kuachana nacho na kuingia chama kingine kama vile alivyofanya Senator Arlen Spector alipohama kutoka Republican na kujiunga na Democrat. Utaratibu wetu unaonyesha jinsi gani wapiga kura wasivyokuwa na sauti kwani mgombea wao anaweza kuvuliwa kiti chake kirahisi tu kwa vile eti hakubaliani na mwenyekiti wa chama chake. Na hiyo ndiyo tabia mbaya tunayotaka ikomeshwe mara moja kusudi wabunge wetu wasitumike kama rubber stamp tu.

Kama Mbatia anaona kuwa hatua aliayochukua ni sawa, je atawakemea nini wabunge wa CCM wakiamua kukubalia kila upupu unaoletwa na serikali bungeni iluhali serikali hiyo inaongozwa na mwenyeketi wao ambaye akitumia madaraka yake kama Mbatia anaweza kuwafukuza wote kutoka ndani ya CCM na hivyo kupoteza ubunge wao?

NCCR kwisha kazi.......watch!
 
Niliwahi kushauri kitu hiki katika moja wapo ya mitandao ya kijamii na leo narudia. Ningetamani kuona ibara hii katika katiba "IWAPO MBUNGE ATAJIUZURU KWA HIARI YAKE BASI CHAMA KILICHOMDHAMINI KICHANGIE ASILIMIA 50 YA BAJETI YA UCHAGUZI MDOGO NA GHARAMA ZOTE ZITAKAZOONGEZEKA.

NA IWAPO CHAMA KIKIMFUKUZA UANACHAMA MBUNGE WAKE BASI KICHANGIE 100% YA GHARAMA ZA UCHAGUZI MDOGO, NA MCHANGO HUU WA UCHAGUZI UTAPUNGUZWA KATIKA RUZUKU YA CHAMA NDANI YA KIPINDI MAALUM"

Tungekuwa na hii kitu ktk katiba yetu ya Kafulila na gamba la Igunga tusingeyasikia na tungeokoa kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi wenye njaa,hawana mikopo ya elimu,hawana barabara,walimu wanaoidai serikali na mengine kibaooo, nawasilisha
 
Back
Top Bottom