Zitto alipuka tena bungeni

Hakika Serikali ya JK haibebeki kabisa , leo Kamati ya Ardhi Maliasili na Mazingira ya Bunge kwa mara nyingine imemlipua waziri maige na watumishi wa Wizara ya Mali asili na utalii kwa kashfa kubwa ya kugawanya vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa rushwa na pia utoroshaji wa wanyama pori kwenda Nje...

ninachoona hapa siamini..duh!
 
uyu Zito anapenda sana masifa,ata kama ndio mbio za urais...yani anajifanya anauchungu sana na nchi wakati ela za barrick anatafuna.

Judi wa K,
Ninaomba ushahidi wa kashifa ya Zitto ili naye ajadiliwe tusipige longolongo kavu.
 
Miongoni mwa maandiko magumu sana niliyowahi kusoma ni yale yanayosema

"Wapendeni Adui Zenu, Waombeeni Wanaowaudhi"

Jifunze kupenda hata unaowachukia akiwemo spika

Du mkuu hata mimi nipo kuwapenda maadui zangu wote ispokuwa huyu spika ambae aliapa ataitetea na kuilinea katica ya Tz ila cha kushangaza matendo yake yanaenda kinyume kwakuwalinda na kuwatetea mafisadi na ccm kwa ujumla
 
Mh Zitto leo, hivi punde, alitoa taarifa kwa Spika kuwa maelezo ya Waziri na Naibu Waziri wa Nishati na Madini kuhusu sakata la Mgodi wa Kiwira ni ya uongo mtupu na akafafanua jinsi Ufisadi wa kusikitisha ulivyofanyika, Spika akadai kuwa taarifa hiyo iletwe kwake kwa maandishi ili Serikali iweze kujibu, cha kushangaza Zitto akamjulisha Spika kuwa taarifa hiyo ipo kwake Spika kwa maandishi labda apelekewe upya, nae Spika Anna Makinda bila kusita akajibu "ndiyo ilete upya!" Sasa wanajamvi wenzangu sijui mumemuelewaje Spika anavyofanya jazi yake! Ina maana hasomi taarifa sensitive kama hizo au anapuuza kwa vile zimeongozwa na wapinzani au anawalinda mafisadi kwa makusudi?
 
uyu Zito anapenda sana masifa,ata kama ndio mbio za urais...yani anajifanya anauchungu sana na nchi wakati ela za barrick anatafuna.

una uhakika na usemalo ndugu yangu,kama kweli anakula fedha za barick ajitokeze mtu mwenye uhakika na jambo ilo na amshutumu .NDIYO UWAJIBIKAJI KWA MANUFAA YA NCHI YETU.
 
Kwa maelezo ya Zitto ni kwamba tayari kamati yake walishawasilisha taarifa kwa ofice ya Speaker lakini cha kusikitisha Speaker anamtaka Zitto awasilishe tena (re-submit) taarifa hizo kwa speaker! Hapa napata wasiwasi kama kweli Speaker ana uwezo wa kuongoza bunge maana anaonekana kutofanyia kazi taarifa anazopewa na kamati za bunge!

Yani huyu Speaker akiona Zitto/Lissu wamesimama basi yeye anakuwa na majibu ya kukataa tu....hili jambo ni kama limemtia aibu maana Zitto kamwuliza tulete tena(re-submit) nilitegemea speaker angeshtuka lakini kwa mshangao kasema taarifa iletwe tena...hapa nakubaliana na ww kuwa huyu mama hanaga muda wa kusoma hizo ripoti anazopewa
 
Mh Zitto leo, hivi punde, alitoa taarifa kwa Spika kuwa maelezo ya Waziri na Naibu Waziri wa Nishati na Madini kuhusu sakata la Mgodi wa Kiwira ni ya uongo mtupu na akafafanua jinsi Ufisadi wa kusikitisha ulivyofanyika, Spika akadai kuwa taarifa hiyo iletwe kwake kwa maandishi ili Serikali iweze kujibu, cha kushangaza Zitto akamjulisha Spika kuwa taarifa hiyo ipo kwake Spika kwa maandishi labda apelekewe upya, nae Spika Anna Makinda bila kusita akajibu "ndiyo ilete upya!" Sasa wanajamvi wenzangu sijui mumemuelewaje Spika anavyofanya jazi yake! Ina maana hasomi taarifa sensitive kama hizo au anapuuza kwa vile zimeongozwa na wapinzani au anawalinda mafisadi kwa makusudi?

She is not competent for the position she is Possessing
 
Spika Makinda ama haelewi maana ya uspika au anatenda asichojua au ana amua bila kufikiri
 
Kwa kweli hata anachokifanya mwenyewe nadhani roho inamuuma sana na sidhani kama ni muumini wa kanisa ama msikiti wowote maana kwa mambo anayoyakingia kifua bungeni hata shetani mwenyewe anayaogopa na hii laana inayotolewa na waTz itamtafuna maisha yake yote na alaaniwe!
 
Hongera ww usiekuwa na uchungu na rasilimali za nchii hii...kazi umagamba tu...
uyu Zito anapenda sana masifa,ata kama ndio mbio za urais...yani anajifanya anauchungu sana na nchi wakati ela za barrick anatafuna.
 
Spika makinda ni mwanamke, na CCM ilikuwa inahitaji spika mwanamke, hayo mengine ni yenu nyie wapinzani
 
uyu Zito anapenda sana masifa,ata kama ndio mbio za urais...yani anajifanya anauchungu sana na nchi wakati ela za barrick anatafuna.
na wewe ulete taarifa yako kwa maandishi hapa ima tutahisi una misifa zaidi ya zito ***********
 
Back
Top Bottom