Zitto aivua nguo serikali maandamano ya Gesi Mtwara | Dar inachangia 80% ya pato la Taifa!

Tuseme kweli. Haya ni matokeo ya uundwaji wa matabaka, upendeleo, ubaguzi, udini, umkoa ukabila nk

1. Zito ni mtu hatari zaidi kwa mstakabali wa umoja wa nchi yetu. ZZK anaona upande mmoja wa shilingi, na siku zote yeye anajiona ni sahihi na wengine ni wakosefu. Alianzia ya Kigoma sasa ameenda ya Mtwara baadaye atakuja na Jihad we subiri uone

2. Hoja ya pande zote ni sahihi, tatizo ni kuwagawa watanzania kimkoa, kidini nk, sera ya serikali ya sisiem na mshawishi mkubwa ZIto. Sasa tumekaribia kuvuna tulichopanda.

3. Tutambue mchango mkubwa wa raisi BWM kwenye uudaji wa sera hizi mbovu.

4. Tumwombe Mungu tusifike huko kwani tunaelekea kusiko stahili. Leo ni Mtwara, Je na Morogoro wakianza na Umeme utakuwaje? Au ile nguzo inayopita juu ya kijiji chetu na sisi hatuna umeme tuiangushe mpaka sis tupate?

5 Kila kitu nchi hii ni kwa kujuana, iwe kugawa mkoa, wilaya, viwanda, miradi hata kujenga misikiti au makanisa japo sina uhakika. Haya ndiyo matokeo ya ubaguzi.

5 Mnyika alisha sema JK ni dhaifu. Na sote tunajua serikali dhaifu na ya wala rushwa. Kila kitu dili tu


 
umekuja jf kujifunza au umekuja jf kutafuta bwana??
rudi facebook bwana mdogo
hahaaaa ukweli unauma etiiiiii@ unamsema vibaya kamanda Zitto wakati una copy akili yake akaitumie kuelimisha umma mwache Zitto aitwe zitto Nguzu kuu ya Chadema
 
Mwongo kabisa huyo!! kwani dar wanachimba tanzanite, au almasi, au makaa ya mawe, au wanalima pamba, kahawa, karafuu, mkonge, au wanavua sangara?? Pale si wamejaa wamachinga tu wanauza pipi au nswiti au vile vya pweza wanavyouza jioni ndio vinaongeza pato la taifa.
 
hahaaaa ukweli unauma etiiiiii@ unamsema vibaya kamanda Zitto wakati una copy akili yake akaitumie kuelimisha umma mwache Zitto aitwe zitto Nguzu kuu ya Chadema

hebu angalia mwenyewe ulichokiandika kisha upime unastahili kuzungumza na mimi au la,
ujue unaongea na wazaz wako humu??
hebu ficha upumbavu wako
 
Honestly sijaona hoja hapo, bali MALUMBANO.

Kama vile Prof. Mhongo asivyo sahihi ndivyo naye Mh. Zitto asivyo sahihi.

Kama ni kuonewa na kudhulumiwa maendeleo na huduma muhimu kama afya, elimu, barabara, umeme nk ni nchi nzima imeonewa tena kwa muda mrefu. Hakuna uwiano wa rasilimali/mapato wenye kukidhi thamani (cost value) ya matumizi ya serikali za CCM toka 1977. Hivyo mimi naona wote wawili wanafanya siasa kwa gharama za umoja wa Taifa, ukweli na maendeleo ya DHATI kwa Tanzania na Wananchi wake. Becuase they've picked "few and selective" issues to foster partisan/ individual agendas.

Ni hoja dhaifu maana leo watu wa Kanda ya Ziwa wakianza kudai, wakafuatiwa na wa Pwani, kisha Kaskazini nao kudai wamepunjwa, wameonewa nk tutafikia tamati ya hizo hoja kweli? Of coz ni CCM na serikali zake tu ndio watakaokuwa hatiani lakini mkiwa selective lazima watapata mwanya wa kukwepa na kuendelea kunyonya wananchi na kufuja utajiri wa nchi hii.

Je ni Kwanini kusiwe na upana wa wigo ktk hoja ya kuishinikiza serikali ipeleke maendeleo vijijini/wilayani/mikoani? Jinsi lilivyo kwa sasa lina mushkeli.

Kwa namna moja unakubali udhaifu wa mfumo na sera tuliyonayo ya uchumi ambayo nafikiri ndiyo watu wa Mtwara wanalalamikia. Hata hivyo ikiwa ulimsikiliza vyema Mh Mhongo Jana inaonekana kila mkoa una aina fulani ya madini na gesi iko karibu mikoa yote! Hivyo hapatakuwa na tatizo ikiwa kila raslimali iliyopo itatumiwa vyema kufaidisha sehemu inayotoka kwanza na kisha sehemu zingine za taifa. Kinachotakiwa ni sera sahihi!
 
Mwongo kabisa huyo!! kwani dar wanachimba tanzanite, au almasi, au makaa ya mawe, au wanalima pamba, kahawa, karafuu, mkonge, au wanavua sangara?? Pale si wamejaa wamachinga tu wanauza pipi au nswiti au vile vya pweza wanavyouza jioni ndio vinaongeza pato la taifa.
Kwa ufupi pale kuna wachuuzaji
 
Nyie waswahili mna matatizo sana. Sasa hii gesi mnataka mfanyie nini yote? Kupatikana Mtwara ndio iwe hiyo hiyo ugali, hiyo hiyo mboga, au?

Mi sioni mnachopigia kelele. Mnaongea as if hiyo gesi imechukuliwa na Mtwara haikupata. Mna sababu yeyote zaidi ya kutumiwa? Pamoja na kwamba naichukia CCM kuliko konokono asiye na nyumba lkn ni upuuzi kupinga kila kinachofanywa na serikali.
 
80%-90%=-10%???Is it!

tuendeleze hesabu mkuu....

Tumeambiwa kua deni la taifa kwa sasa limefikia trillion 22 (hapa hilo deni tunalodaiwa na mafisadi yaani -10% halijajumlishwa). Rais ametangaza idadi ya watu kua tumefikia 44,929,002 (alhamdulah tumeongezeka angalau deni la kila mmoja limepungua)

twende kwenye hesabu sasa:

22x10[SUP]12[/SUP] gawanya kwa 44,929,002 unapata kua kila mtanzania anadaiwa Tshs 489,661.4 sasa hapa unatakiwa ujumlishe deni tunalodaiwa na mafisadi. Hii calculation ina assumptions kibao ambazo kama tukizi-ignore deni linakua laki tano kila mtanzania (mojawapo ya assumption ni kua kuna watoto wamezaliwa ku-replace waliofariki tangia kukusanya sensa na kutangaza matokeo.
 
Nyie waswahili mna matatizo sana. Sasa hii gesi mnataka mfanyie nini yote? Kupatikana Mtwara ndio iwe hiyo hiyo ugali, hiyo hiyo mboga, au? Mi sioni mnachopigia kelele. Mnaongea as if hiyo gesi imechukuliwa na Mtwara haikupata. Mna sababu yeyote zaidi ya kutumiwa? Pamoja na kwamba naichukia CCM kuliko konokono asiye na nyumba lkn ni upuuzi kupinga kila kinachofanywa na serikali.
Tatizo la Watanzania wengi ikiwemo wewe ni wavivu kusoma na kuelewa hoja. Hoja hapa ni kwanini mara hii malighfi ya kuzalisha umeme inasafirishwa kutoka inakopatikana badala ya mitambo ya kuzalisha umeme kujengwa huko ma umeme ndio usafirishwe huku mikoa inakopita pia ikipata huduma ya umeme.

Wakati nchi badi inaendeshwa kwa maadili mitambo ya kuzalisha umeme ilijengwa Kihansi, Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu, Hale n.k badala ya mabomba kujengwa ili kusafirisha maji ili kuzalisha umeme DSM, Kutoka maeneo yote hayo umeme ulisafirishwa kuletwa DSM huku mikoa ya njiani ikipata huduma ya umeme ambayo haikuwa nayo. Nini kimebadilika hivi sasa. Ni viongozi wa CCM na CCM kujinufasiha kupitia mitambaoa ya kuzalisha umeme wa dharura kama vile IPTL, RICHMOND, DOWANS n.k kwa miongo miwili.

Kwa kuwa wawekezaji feki akina Rostama Aziz walijenga mitambo hiyo DSM ndio maana gesi hiyo lazima iletwe DSM. Prof Muhongo alisema gesi iligunduliwa mwaka 1974 huko Lindi na Mtwara, ni kwanini hadi sasa miaka 40 baadaye mitambo ya kuzalisha umeme haijajengwa huko Lindi na Mtwara?
 
tuendeleze hesabu mkuu....

Tumeambiwa kua deni la taifa kwa sasa limefikia trillion 22 (hapa hilo deni tunalodaiwa na mafisadi yaani -10% halijajumlishwa). Rais ametangaza idadi ya watu kua tumefikia 44,929,002 (alhamdulah tumeongezeka angalau deni la kila mmoja limepungua)

twende kwenye hesabu sasa:

22x10[SUP]12[/SUP] gawanya kwa 44,929,002 unapata kua kila mtanzania anadaiwa Tshs 489,661.4 sasa hapa unatakiwa ujumlishe deni tunalodaiwa na mafisadi. Hii calculation ina assumptions kibao ambazo kama tukizi-ignore deni linakua laki tano kila mtanzania (mojawapo ya assumption ni kua kuna watoto wamezaliwa ku-replace waliofariki tangia kukusanya sensa na kutangaza matokeo.
safi sana mku,this is very good and logical analyses!
 
mbona wakati huu mradi wa kupeleka gesi dar unazinduliwa na zitto kabwe alikuwepo? Mbona hakuyasema haya? Mi nilikuwepo pale na yeye mwenyewe alikuwepo, sasa hii kweli inatoka kwa zzk? Mkuu, wewe hutabiriki na umechelewa sana katika hili...

heereee its big shoooooooooow

the big show gives you a big liiiiiikeeee,,,,,
tupo pamoja mkuu
 
Zitto Kabwe is, and has remained as mjenga hoja mzuri wa kutegemewa ndani ya chama chetu na taifa kwa ujumla.....

nimshukuru kwanza kwa kuwithdraw kwenye public mshawasha wa kukimbilia ikulu.... he has got plently to do in various positions kabla ya kumalizikia kwenye uraisi...

ishu ni kwamba ninashangaa kwanini maprofesa wengi wetu wanakuwa wenye hamaki hamaki... kwani naelewa jambo moja kubwa ambalo msomi mwenye shahada ya uzamivu anatakiwa kuwa nalo: ni kukubali sauti za wengine zisikike, kukubali kuadopt hoja yopyote ijayo ilimradi ina logic, kukubali kuendelea kujifunza na hivyo kukuza na kuendeleza sayansi...

ninarudia kusema hili kwakuanza na jinsi mama profesa tibaijuka alivyomcharukia halima mdee masikini wa mungu mwanafunzi wake alipohoji kuhusu uporwaji wa ardhi na akasahau facts zifuatazo

1. ardhi ni ultimatam resource ya uchumi kwa taifa lolote....

2. anasahau hata kuwa baadhi ya kanunni za classic economist ni exploiting eg theory of comparative adavantage...

3. anasahau kuwa ardhi iliyopo available to tanzanians ni mwendelezo wa vita kali aliyoipigana mwalimu

4. ameshindwa kabisa kuona wakenya wenye uwezo wa kuzaklisha wanateseka hawana ardhi, na kwamba hata sie tunagain...na tunaopaswa kuwa promoted

5. ameshindwa kuifore see kuwa what is happening to zimbabwe now is potentia to tanzania in 15 yrs time....

na ni aibu kuwa serekali imekiri kuwa kulikuwa na uyzembe......

tuje kwa prof muhongo....

1. amesahau kuwa yeye sio mtaalamu wa maendeleo..bali wa madini......

2. amesahau kuwa anapawswa kujifunza kwa wataalamu wa maendeleo na nchi mbali mbali

3. amekataa kukiri kuwa review ya sera za madini ni muhimu....

ATAKUJA KUKUBALI KUWA ZITTO UMMA NA WENZIWE WALIKUWA SAHIHUI

BUREEEEEE KABISA

Zitto ana heshima yake katika taifa hili, 100% Waziri asipokuwa makini hoja za zitto zitamng'oa kabla 2015.
 
hapo hapo kwenye red usinune...

hakuna sehemu yoyote ya tanzania ilowahi kufaIDIKA NA EXPLORATION ZILIZOFANYIKA.....

NDIO MAANA SHINYANGA IS THE POOREST..JAPO NI MASKANI YA ALMASI...


SIO PWANI WALA KANDA YA ZIWA WALIOFAIDI..SANA SANA KUISHIA KUPIGWA RISASI....

NA KUONA HAMMER ZIKIONGEZEKA DAR, AKAUNTI ZIKIPUMUA USWISI, NA WATOTO WETU WAKIENDELEA KUKALIA MATOFALI....

UZURI THE WHOLE COUNTRY IS ENORMOUSLY RICH...

SERA YA MAJIMBO NDIO DAWA....


Tuko ukurasa mmoja. Sera ya majimbo ni sawa ila inahitaji refinery kidogo.

Unakumbuka ishu ya Buzwagi, Kiwira na nyinginezo hazikuwa fostered na mwavuli wa ukanda au ueneo. Hili la kusini tayari lina ila aina ya ufisadi na soon itakuwa realized lakini kulitetea kwa hoja ya ukanda is to me a meek surrender to mafisadi ploy.
 
Hongera Mkuu THE BIG SHOW katika jitihada zako za kuwafungua macho wananchi wa Mtwara ili waweze kunufaika katika rasilimali kubwa zilizogunduliwa mkoani mwao. Dhahabu yenye thamani ya $11 billioni imeshachimbwa na kuuzwa toka katika mikoa yenye dhahabu kuanzia mwaka 1998 mpaka 2011 lakini mikoa hiyo bado iko nyuma kimaendeleo na Wananchi walio wengi katika maeneo hayo ambapo dhahabu inapatikana bado wanaishi maisha ya ufukara wa kutisha huku makampuni ya nje, shareholders wao wakifaidika na mafisadi wa Serikali na magamba wakijikusanyia mabilioni ya pesa na kuzificha katika foreign bank accounts zao katika nchi mbali mbali duniani. Hongera sana Mkuu.

thanks na usijal
,
makala hii nimeicopy na tutaijumuisha katika hizi zingne ambazo tayari tushaziandaa katika mikutano mingne ya kutoa elimu zaid kwa wananchi,mchango wako una thaminiwa sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
umekuja jf kujifunza au umekuja jf kutafuta bwana??
rudi facebook bwana mdogo

We big show naona lengo lako kuu ni kuponda...unaponda kila anaemsemea zitto vizuri...sidhani kama huna malengo mazuri na chama chetu..kumchafua mbowe,zitto ama slaa ni kukichafua chama indirectly....
 
Back
Top Bottom