Zitto aivua nguo serikali maandamano ya Gesi Mtwara | Dar inachangia 80% ya pato la Taifa!

ubaguz wa kanda na udini ndio kiin cha chadema kwa kushangilia hili hatushangai kwa nini musiwambie korosho zao watafune wanakuja kubanngua dar?

Delta Rufiji kama ni msomi nina wasiwasi na usomi wako la haujasoma,na ndio maana wasomi wetu wa Tanzania huwezi kuwalinganisha na wasomi wa nchi yeyote sababu ni maboya tu, Umesoma kilichoandikwa hapo juu kuhusu gas ya Mtwara? Unakurupuka kuandika utumbo,haujui unachoandika wanatetewa wananchi wa Mtwara unaandika utumbo,kwanza walioandika wanakuzidi IQ unakurupuka tu ACHA kufikiri kwa kutumia makalio wewe huelewi nyamaza usiandike upumbavu wako humu jf
 
Last edited by a moderator:
zitto kabwe is, and has remained as mjenga hoja mzuri wa kutegemewa ndani ya chama chetu na taifa kwa ujumla.....

Nimshukuru kwanza kwa kuwithdraw kwenye public mshawasha wa kukimbilia ikulu.... He has got plently to do in various positions kabla ya kumalizikia kwenye uraisi...

Ishu ni kwamba ninashangaa kwanini maprofesa wengi wetu wanakuwa wenye hamaki hamaki... Kwani naelewa jambo moja kubwa ambalo msomi mwenye shahada ya uzamivu anatakiwa kuwa nalo: Ni kukubali sauti za wengine zisikike, kukubali kuadopt hoja yopyote ijayo ilimradi ina logic, kukubali kuendelea kujifunza na hivyo kukuza na kuendeleza sayansi...

ninarudia kusema hili kwakuanza na jinsi mama profesa tibaijuka alivyomcharukia halima mdee masikini wa mungu mwanafunzi wake alipohoji kuhusu uporwaji wa ardhi na akasahau facts zifuatazo

1. Ardhi ni ultimatam resource ya uchumi kwa taifa lolote....

2. Anasahau hata kuwa baadhi ya kanunni za classic economist ni exploiting eg theory of comparative adavantage...

3. Anasahau kuwa ardhi iliyopo available to tanzanians ni mwendelezo wa vita kali aliyoipigana mwalimu

4. Ameshindwa kabisa kuona wakenya wenye uwezo wa kuzaklisha wanateseka hawana ardhi, na kwamba hata sie tunagain...na tunaopaswa kuwa promoted

5. Ameshindwa kuifore see kuwa what is happening to zimbabwe now is potentia to tanzania in 15 yrs time....

Na ni aibu kuwa serekali imekiri kuwa kulikuwa na uyzembe......

Tuje kwa prof muhongo....

1. Amesahau kuwa yeye sio mtaalamu wa maendeleo..bali wa madini......

2. Amesahau kuwa anapawswa kujifunza kwa wataalamu wa maendeleo na nchi mbali mbali

3. Amekataa kukiri kuwa review ya sera za madini ni muhimu....

Atakuja kukubali kuwa zitto umma na wenziwe walikuwa sahihui

bureeeeee kabisa
umesahau mkuu? Maneno ya dr. Kitila mkumbo? Elimu yetu sio ya udadisi ni elimu ya kufaulu mitihani baada ya mitihani kwisha ubongo unakuwa empty? Kamwe elimu ya tanzania haitengenezi wataalam inatengeneza wafaulu mitihani uoni kuwa hili limeathiri mpaka uko juu kwenye level za uphd? Tuna phd ngapi nchi hii mkuu zinatusaidia nini wakati mpaka nyembe na sindano tuna import? Msigwa nae alisema professor akichangia hoja hatofautiani na mtoto wa darasa la pili! Mkuu msigwa alikuwa na maana hii
 
ubaguz wa kanda na udini ndio kiin cha chadema kwa kushangilia hili hatushangai kwa nini musiwambie korosho zao watafune wanakuja kubanngua dar?

watu wa mtwara sio misukule kama mnavyotaka iwe.
hili swala la gas ni kipimo cha udhaifu na dharau kubwa ya serikali dhidi ya wapiga kura.
 
HONGERA MH ZITTO kwa uzalendo wako kwa wanamtwara na lindi na watanzania wote kwa ujumla. hivi tumekosa nini katika nchi yetu? halafu wabunge wa mikoa hii mko wapi? hamuoni haya yanayotendeka mpaka zitto aje awasemee? inasikitisha sana.
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye haya madai ya Dar kuchangia 80% ya pato la Taifa. Ukipitia makabrasha ya serikali utaona kuwa kilimo kinachangia almost 50% ya pato, communications about 20% na manufacturing ni less than 10%.

Sasa Dar ni jiji - la viwanda. Hakuna kilimo Dar es salaam. Aprox 80% ya watanzania wanaishi vijijini (nje ya Dar) ambako ndiko kilimo kinapofanyika. Sasa haya madai ya Dar kuchangia 80% yanatoka wapi? Kwa kitu gani maana viwanda hata havifiki 10%?

Mkuu hiyo 80 % inayozungumziwa hapo si pato la taifa kwa ujumla wake (yaani pamoja na mapato ya watu binafsi wakiwemo wakulima) bali ni (Tax revenue income). Yaani mapato yote yatokanayo na kodi 80% inatoka DAR. Si unajua nchi ilivyo shaghalabaghala ukiwauliza tunapata kiasi gani cha kodi kutoka kwenye kilimo hakuna data, kwakuwa wakulima sanasana hulipa ushuru kwenye viji-soko wanakouza mazao yao basi.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Na Zitto Kabwe

'Dar inachangia asilimia 80 ya mapato. Kitovu cha Uchumi. Dar inachangia 90% ya ufisadi. Uti wa mgongo wa ufisadi nchini'

Malumbano kati ya wananchi wa Mtwara na Serikali kuhusu matumizi bora ya utajiri wa nchi yameendelea kwa takribani wiki moja sasa. Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Nishati na Madini kuwaita Watanzania wa Mtwara Wahaini, wapuuzi na watu hatari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye aliingia kwenye mjadala huo kwa kuonya watu wanaowaunga mkono watu wa Mtwara na kuwaita watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa na wanaotaka kugawa nchi. Siku moja baada ya hotuba ya Rais, Waziri wa Nishati na Madini alifanya mkutano na waandishi wa habari kueleza suala lile lile ambalo bosi wake alilielezea usiku wa kuamkia mwaka mpya 2013. Hii ni dalili ya Serikali kuweweseka.

Katika kauli ya Serikali, ambayo haikuwa na jipya zaidi ya wimbo ule ule wa ‘kugawa nchi’ ‘umaarufu wa kisiasa’ nk, Serikali ilitaka kuonyesha umma kuwa watu wa Mtwara hawana shukurani. Kwamba miaka yote toka Uhuru watu wa Mtwara wamekuwa wakilishwa na Pamba, Kahawa, Chai, Tumbaku, Sukari, Kidatu nk. Kwamba watu wa Mtwara na Lindi hawakuchangia hata kidogo kwenye hazina ya Taifa. Hivyo wao kupigia kelele gesi yao ni uchoyo na roho mbaya na kukosa shukurani. Kauli ya Serikali ni kauli ya chombo kinachoendelea kukosa ‘legitimacy’ ya kuongoza taifa. Ni kauli ya kukata tamaa. Ni kauli hatari sana dhidi ya Watanzania waliojitolea damu kulinda uhuru wa nchi yetu.

Moja, Serikali katika kauli yake haitaji kabisa kwamba toka Uhuru watu wa Mtwara na Lindi wamekuwa wachangiaji wakubwa sana katika uchumi wa Taifa kupitia zao la Korosho. Takwimu za Uzalishaji wa Korosho zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka 1965 mpaka 2011 Korosho imeliingizia Taifa fedha kigeni jumla ya dola za Kimarekani 4.58 bilioni ( Cashewnuts Sub-sector study 2003, Hali ya Uchumi 2012, Cashewnuts Tanzania Report 2010). Katika Mwaka wa Uchumi unaoishia Novemba 2012, Korosho imeliingizia Taifa jumla ya dola za Kimarekani 151 milioni. Katika mwaka 2011 zao hili liliingiza dola 130 milioni wakati Pamba iliingiza dola 53 milioni tu. Licha ya Zao la Korosho kuingiza fedha hizi za kigeni -(sawa ni shilingi trilioni 7.2) kwa nchi mikoa ya Lindi na Mtwara ipo miaka 50 nyuma kimaendeleo kulinganisha na mikoa mingine ya Tanzania. Serikali inataka kufuta historia ya mchango wa zao la Korosho kwenye uchumi wa nchi yetu kwa sababu ya uroho wa gesi asilia. Kwa nini kauli rasmi ya Serikali haijataja Korosho kabisa? Kauli hii ilipitishwa na ngazi zote za Serikali? Mawaziri wa Serikali wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara walikubali kauli kama hii itoke dhidi ya wananchi wao wanaoteseka na zao la Korosho miaka nenda miaka rudi?

Pili, Serikali imesahau kabisa mchango wa watu wa Lindi na Mtwara katika ulinzi wa Taifa letu. Moja ya sababu ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa nyuma kimaendeleo ni juhudi za ukombozi wa kusini mwa Afrika. Kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji ilikuwa Nachingwea. Kambi ya Frelimo iliwekwa kwenye Shamba la Mkonge kilometa 17 tu kutoka mjini Nachingwea ambapo ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa Msumbiji. Rais Samora Machel, Rais Joaqim Chissano na Rais Guebuza waliendesha mapambano kutoka kusini mwa Tanzania. Makaburu wa Afrika Kusini na Wareno walikuwa wanashambulia nchi yetu na mikoa hii miwili ya Lindi na Mtwara ikawa ‘buffer zone’. Wakati Dar es Salaam inaendelea kwa kila aina ya maendeleo, mikoa ya Lindi na Mtwara ilikuwa inalinda ili wanaoishi Dar es Salaam na mikoa mingine waishi wa amani na starehe. Serikali inapimaje mchango huu wa mikoa hii? Tunaipima kwa fedha? Uroho wa gesi asilia kuzalisha umeme wa kufurahisha walalaheri asilimia 14 nchini ndio inaifanya Serikali kusahau kabisa ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara katika kulinda uhuru wa Taifa letu?

Tatu, Serikali inasema lazima bomba lije Dar es Salaam kwa sababu Dar ndio inazalisha asilimia 80 ya Mapato ya Serikali. Kwanza huu ni uwongo. Ni aibu Serikali kujitetea kwa uwongo. Dar es Salaam ni kituo tu cha kukusanyia mapato ya Serikali. Uzalishaji mkubwa wa nchi yetu wenye kuzalisha kodi unafanyika nje ya Dar es Salaam. Walipa kodi wakubwa wengi Ofisi zao Kuu zipo Dar es Salaam lakini uzalishaji wao unafanyika nje ya Dar es Salaam. Serikali itoe orodha ya walipa kodi wakubwa 100 tuone uzalishaji halisi wa mapato hayo unafanyika wapi.

Hata hivyo inawezekana kuwa ikawa kweli Dar es Salaam inakusanya asilimia 80 ya mapato ya nchi. Basi na tuseme Dar es Salaam inachangia asilimia 90 ya ufisadi wote nchini. Kashfa zote kubwa za Ufisadi zinafanyika Dar es Salaam na fedha nyingi za ufisadi zinatumika Dar es Salaam.Mwisho, maandamano ya watu wa Mtwara ni kielelezo tosha kwamba watu wa mikoa ya Lindi na Mtwara wamechoshwa na longolongo za Serikali. Wananchi wa Mtwara na Lindi wanataka Uwajibikaji wa Serikali kuhusu utajiri wa nchi. Mtanzania yeyote mwenye tahadhari ya nchi yetu kutokuwa na laana ya rasilimali ataungana mkono na watu wa Lindi na Mtwara kudai maendeleo. Nilitoa mfano wa Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega.

Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, -Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni. Kabla Serikali haijawaita watu Mtwara wahaini, wapuuzi na watu hatari, iwaambie watu Watanzania kodi kiasi gani imekusanywa kutoka mgodi huu katika kipindi cha miaka 14. Mpaka mwaka 2008, kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bomani, kampuni hii ilikuwa imelipa mrahaba wa dola 11 milioni na kodi nyingine dola 16 milioni. Serikali itwambie ilipofika Disemba 2012 kodi kiasi imekusanywa kutoka kampuni hii?

Pia watu wa Mtwara na Lindi wameona historia ya bomba la Songosongo. Hata kodi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (0.3%) ilikuwa inalipwa Halmashauri ya Manispaa Ilala na kampuni ya Pan Africa Energy. Ilichukua juhudi za mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu kuingilia kati ndio kodi ikaanza kulipwa Kilwa ambapo uzalishaji unafanyika. Watu wa Mtwara ni werevu, wanajua wafanyalo. Wanataka utajiri wa nchi unufaishe nchi kwa kuanzia kule utajiri ulipo. Kuna dhambi gani?

Uwajibikaji katika uvunaji wa Rasilimali ya Gesi ndio chanzo cha maandamano ya watu wa Mtwara. Serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa kwamba ndio wamechochea maandamano haya. Haya ni maandamno ya wananchi wakitaka Serikali yao iwajibike kwao. Serikali ithubutu kufanya ubabe wa kujenga bomba la gesi bila ridhaa ya Wananchi wa Lindi na Mtwara. Wananchi wanapohitaji uwajibikaji ni wajibu wa Serikali kuwajibika kwao ni sio kuwaita wahaini, wachochezi, watu hatari, wapuuzi. Watu wa Mtwara wamechangia maendeleo ya Taifa letu kwa jasho na damu. Serikali ina wajibu wa kuwasikiliza, kuwaelimisha na kupata mwafaka. Kauli ya Serikali imewatukana watu wa Mtwara na Lindi. Hawatakubali kudhalilishwa. Hawatakubali historia yao kufutwa. Hawatakubali waendelee kubaki nyuma kimaendeleo. Serikali ifikirie tena.

Kwanza nashangaa kuona serikali inatumia kigezo dhaifu ili kuhalalisha uporaji wandani wa rasilimali na kusababisha mrundikano wa maendeleo katka eneo moja tena dogo la nchi kama Dar. Unyonyaji unaofanywa na viongozi wazalendo (maana si wakoloni) kwa wananchi wa nje ya Dar ni kosa na hautavumiliwa! Leo ni Mtwara na Lindi ila kesho ni Kanda ya Ziwa. Kama Dar serikali inakusanya 80% hii ni sababu tosha ya kusambaza miradi ya maendeleo kwingine nchini na si kuweka mikakati ya kufikia 100%.

Kama kaka angu ZZK alivyosema kuwa ni uongo kusingizia 80% revenue collection kwani kukusanyiwa Dar haimaniishi zinazalishiwa hapo hapo. Kanda ya ziwa na madini yake na samaki wanakusanyia huko huko Dar. Je! Dar kuna mgodi au ziwa? Utasikia mara treni ndani ya Dar au barabara za angani wakati umaskini wa kutupwa unatuuwa huku vijijini.

Lazima tugawane rasilimal za taifa kwa usawa bila ubaguzi. Watnzania tuna hadhi sawa tuache kubaguana kwa rasilimali zetu! Nawaponeza wananchi wa Mtwara mkimaliza tunaingiza sisi wa kanda ya ziwa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nawashukuru sana viongozi wa vyama pinzani lakini mimi nilitamani viitwe vyama mbadala wanaeleza ukweli ingawa viongozi walioko madarakani wanajifanya hawasikii wala kuelewa,na kuhusu wabunge wa mtwara na lindi ni kuwa wanadhani kila siku ni jumamosi au kila mzungu ni padre.....watu wanaelewa siku hizi sio kama enzi za zamani na natamani sana nyie watu mnaoelewa haya mambo jaribuni kuhakikisha kuwa hii elimu inawafikia watu wengi iwezekanavyo ili tusiwe tena mambumbumbu kiukweli imetosha sana kuona raia tulio wengi tunahangaika wakati walewale wanakula bata.....nawapenda sana mnaoona umuhimu wa gesi kuprocesiwa mtwara ili raia wanufaike na ingekua vizuri zaidi na sehemu zote zenye maliasili kuona wananufaika hayo ndio maendeleo ya kweli.
 
Cheap answers to a serious problem. Hili sio suala la kisiasa bali ni suala la kiuchumi. There are facts which the minister need to have at hand before they give out any information to the publicjuu ya hii gesi. Ningeshauri yafuatayo:
1. Tuachane na ministers/politicians na maelezo yao na tutafute maelezo kutoka kwa wachumi/wataalam wetu
2. Kwa nini wana harakati wasije na facts juu ya hii project badala ya kutegemea wanasiasa wetu ambao siku zote wamekuwa ni wepesi and very shallow!
 
Hii ya 80% ni matusi kwetu mikoa mingine, na tunasubiri mjenge daraja lenu na flyovers ndo mtajua hii nchi si Dar pekee
 
Wengi wa wanasiasa na hasa ma-profesor wa Tanznaia siyo wanasiasa wamefuta pay roll kubwa basi hakuna zaidi....Lakini hii ni very temporal some of us are determined to show them how it pays to be an academician kuliko kuwa mwanasiasa ila lazima kuwe na political will ilikujenga huo mfumo ambapo siasa itabakiwa na wanasiasa wazuri na siyo watu wenye kutafuta shortcut ya maisha
Ni kweli. kama profesa ataacha fani yake na kufuata siasa kwa sabbu kuna kipato zaidi ujue hatasaidia lolote zaidi ya kujisaidia mweyewe. hapo lawama humwandama kila kuchapo.
 
moja kati ya hotuba za hayati baba wa taifa katika kukemea rushwa, amewah kusema serikali corrupt duniani kote haikusanyi kodi. itakimbizana na wafanyabiashara wadogo wadogo na kuwaacha wengine kwenye neema, nina huzunika sana kuona kama serikal yangu iko ivyo(corrupt), et 80% ya pato la taifa linapatikana dsm, vp mikoa mingine 29? kuna tra au dra? yani dar revenue authority? mahotel yanabadil majina kukwepa kod, makampuni ya cm hal kadhalika, makampuni ya kitalii, likiwemo la mh. naibu wazir wake, bado deni la taifa 22trln.. tutaendelea kwel???????? NYERERE BABA ULIONDOKA UNGALI BADO TUNAKUHITAJI, UPUMZIKE KWA AMANI. AMINA.
 
Ni ukweli kabisa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
tukumbuke pia mgawanyo wa viwanda kama wakati wa Nyerere tulikuwa na viwanda vya cement Mbeya, Dar na Tanga. viwanda vya nguo karibu kila kanda ya nchi na angalau reli iliwekwa kaskazini, kati na kusini magharibi. hii ilileta matumaini kwa watu wa maeneo yote ya nchi kuhusu kunufaika na rasilimali za nchi yao. na ndiyo maana amani ikawepo Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
profesa amefundishwa kukariri na siyo ubunifu na ufaraguzi yani creativity and improvization ndio maana akisimama anaongea kama mtoto wa darasa la pili.
 
Yaani mhongo alikuwa anataka kulia wakati anatoa maneno yake. Cha kushangaza vyombo vya habari vimelazimika kuandika ya serikali na inavyotaka iandikwe. Kama uelewa wa waziri ni huu basi nchi haiwezi kuendelea hata kidogo

Tatizo la wanazuoni kuwa wanasiasa ndio hilo. Professor anashindwa kuelewa wanachokitaka wananchi wa mikoa ya kusini. hawajakaataa gesi kuchimbwa, wanataka mitambo ya gesi ifungwe mtwara, wapate ajira. Professor alitoa mfano wa madini, but migodi ya madini haikuahamishiwa dar, mitambo ya kuchimba madini, kukata madini etc ipo sehemu husika, inatoa ajira direct and indirect pale pale yalipopatikana madini. je hilo ni kubwa kuombwa na wananchi wa mtwara? Kufunga vinu vya kuzalisha umeme pale mtwara na kuunganisha huo umeme kwenye grid ya taifa kuna tatizo gani? kutafungua maendeleo ya kusini etc. What is point ya kujenga bomba la kusafirisha gesi hadi dar? i would suggest serekali kujenga bomba la gesi kwenda msumbiji kuwauzia gesi labda hilo litakuwa jambo lenye mantiki kiuchumi. Sijui reasoning capacity ya viongoizi wetu imeelekea wapi. i am not suprised, kama raisi wa nchi anakwenda kwenye kila msiba, kuhani na kuzika, atabakiwa na uwezo wa gani zaidi wa kufikiri zaidi!!
 
Muda mwingine najaribu kutafakari matamshi ya viongozi lakini nakosa kujua ama wanachokisema ndio ukweli au kwa mida flani unakuwa ndio kutosheleza mahitaji ya muda; Kwanza Jiji la Dar lina mzigo mkubwa sana kiasi kwamba linaomba kupunguziwa na kauli hizi tata hazisaidii chochote; Tukisema sote tuhamie Dar watasema turudi kijijini tukalime, kwa niniii ???? wakati 80% ya mazuri yapo huko, tena kiongozi anatangaza hili kama vile ni sifa kubwa sana kuwa na mji mmoja tu ukibeba asilimia kubwa hivyo ya utajiri, hivi hawaoni kama wanahatarisha amani ya mji na nchi kwa ujumla

Nadhani bora wakisema Jiji la Dar ninachangia asilimi 80 ya matumizi - (mabaya)...
 
Back
Top Bottom