Zitto aishauri Serikali namna ya Kupunguza matumizi

Hongera sana Mh. Zitto kwa ushauri mzuri. Hii inathibitisha kwamba mngekuwa mnaongoza serikali, tungekuwa tunakimbia na sio kupiga tu hatua kimaendeleo!

Sasa ngoja tuone huo "usikivu" wa serikali ya ccm unaopigiwa debe na wabunge pa1 na watumwa wake!

Sintajitendea haki kama sintasema upuuzi wa serikali ya sasa. Eti baraza la mawaziri limekaa na kuamua ujinga huu. Upungunze bajeti ya maendeleo halafu wanasema wanawajali wananchi!? Ndio maana akina Rejao, ritz1, Mzee, Topical na wenzao wamekaa kimya. Hao maprofesa na madaktari walioko kwenye baraza la mawaziri.ndio wamekuja na upuuzi wa namna hii! Kweli shule hazijawasaidi viongozi wa ccm!?
 
Chanzo cha habari hii ni Zitto na Demokrasia

PRESS RELEASE

MPANGO WA SERIKALI KUPUNGUZA MATUMIZI
Punguza Matumizi ya Posho SIYO Matumizi ya Reli, Barabara, Elimu na Afya

Mwezi Disemba mwaka 2011 Waziri wa Fedha na Uchumi alimwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kumwahidi mambo yepi Serikali ya Tanzania itafanya ili kurekebisha Bajeti yake. Utaratibu huu hufanyika kila mwaka kupitia mpango unaoitwa ‘Policy Support Instrument (PSI). Katika barua hiyo Waziri wa Fedha wa Tanzania ameahidi kwamba Serikali itafanya juhudi kupunguza matumizi ili kuweza kupunguza uwiano wa nakisi ya Bajeti na Pato la Taifa (fiscal deficit to GDP ratio) kutoka asilimia 7.2 mpaka asilimia 6.6 ya Pato la Taifa.
Waziri wa Fedha na Uchumi ameiambia IMF kwamba ifikapo mwisho wa Mwezi Disemba mwaka 2011 (wiki mbili zilizopita) Baraza la Mawaziri la Tanzania limefikia maamuzi ya kupunguza nakisi ya Bajeti kwa kiwango kilichotajwa. Maeneo yanayotajwa ni Pamoja na Miradi ya Maendeleo ambapo jumla ya miradi yenye thamani ya Tshs 157bn itakatwa. Waziri wa Fedha ametaja miradi hiyo katika Ukarabati na Ujenzi wa Miundombinu.

Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga kuondolewa kwa miradi ya maendeleo ili kupunguza matumizi ya Serikali. Kimsingi wakati kama huu ambapo hali ya uchumi ni mbaya na vijana wengi vijijini na mijini hawana ajira tunasisitiza umuhimu wa kutumia zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

Punguza matumizi ya kawaida: Kambi ya Upinzani Bungeni inarejea wito wake kwa Serikali kupunguza matumizi ya kawaida ili kupata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo. Haiwezekani kamwe tukawa Taifa huru iwapo miradi yetu yote ya maendeleo inafadhiliwa na wahisani. Kiwango kidogo tulichokiweka katika Bajeti ya mwaka huu ndicho hicho sasa kinakatwa na hivyo miradi yote ya maendeleo kubakia kwa wahisani ama kwa mikopo au misaada. Kiwango cha Tshs 203bn sawa na 0.5% ya Pato la Taifa ambacho Serikali imeahidi kupunguza ni kidogo mno na kinalenga kuumiza watumishi wa kada ya chini ya Serikali na sio viongozi wakubwa. Bajeti ya Mafunzo inayoenda kukatwa itaumiza Manesi na Walimu au watumishi wanaoongeza ujuzi ili kuboresha kazi zao. Serikali ikate matumizi yote yasiyo ya lazima na hasa posho (360bn), ipunguze matumizi ya magari na yale yasiyo na uhitaji yapigwe mnada na viongozi wote isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika na Jaji Mkuu washushwe madaraja ya kusafiria kwenye ndege. Safari zote ambazo hazina mahusiano na miradi ya maendeleo zipigwe marufuku kwa muda wote wa miezi sita ya Bajeti iliyobakia.

Serikali ihakikishe matumizi katika Sekta ya Elimu na Afya hayakatwi kabisa ili kuhakikisha tunalinda mafanikio kiduchu ya upanuzi wa sekta hizi na kuongeza uwezo wa Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wa vijijini.

Matumizi ya Maendeleo yasiguswe, yaongezwe:Tayari imeonekana kwamba katika kipindi chote cha nusu ya Bajeti Halmashauri za Wilaya hazijapata fedha za maendeleo. Mfano Halmashauri ya Wilaya Kigoma imepata asilimia 0.3 tu ya Bajeti ya Maendeleo ilhali Halmashauri ya Mji wa Mpanda imepata asilimia 4 tu. Ni dhahiri miradi ya maendeleo kwa maeneo mengi ya vijijini itakwama kwani ni wazi kabisa kwamba Halmashauri hazipati fedha zote za Bajeti ya Maendeleo. Serikali itambue kwamba miradi ya maendeleo sio anasa bali ndio vyanzo vya baadaye vya mapato ya serikali. Miradi ya maendeleo hutoa ajira kwa wananchi na hivyo kuwapunguzia umasikini wa kipato. Jumla ya Tshs 157bn zinazotakiwa kukatwa zisikatwe bali ziongezwe ili kupata fedha za kurekebisha miundombinu kama Reli ya Kati.Kwa mfano Reli ya Kati inahitaji Tshs 200bn katika kipindi cha miaka 3 ili iweze kusafirisha mizigo tani 1.5m kwa mwaka kila siku na kuzalisha faida.

Ongeza Mapato ya Ndani: Inashangaza kwamba katika mpango wa Serikali kupunguza nakisi ya Bajeti mkazo umewekwa kwenye kuondoa miradi ya maendeleo badala ya kuongeza mapato. Nakisi hupunguzwa ama kwa kupunguza matumizi au kwa kuongeza Mapato. Serikali katika Taarifa yake kwa IMF imeibua njia moja tu ya kuongeza mapato, kodi ya mapato kutoka Kampuni ya Geita Goldmine. Huu ni uvivu wa kufikiri.
Serikali imeambiwa mara kadhaa suala la kuanza kutumika kwa sheria mpya ya madini kwa Kampuni za Madini zilizokuwapo. Makusanyo ya Mrahaba peke yake kwa sheria mpya, kiwango kipya na kanuni mpya ya kukokotoa ingeongeza mrahaba mpaka Tshs 203bn kutoka Tshs 99bn za sasa. Kwanini Serikali ianvuta miguu katika kutekeleza hili? Waziri wa Nishati na Madini aliahidi Bungeni kwamba mazungumzo na Kampuni za Madini yanaisha Mwezi Septemba. Mbona Serikali imekuwa BUBU katika hili?

Serikali iliahidi kuangalia suala la mauzo ya mali za makampuni zilizoko Tanzania na kodi ambayo tunapaswa kukusanya, Serikali imekuwa kimya kabisa katika suala hili. Marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kuondoa msamaha kwenye ‘deemed capital goods yangeongeza mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa na kupunguza mzigo wa
misamaha ya Kodi.

Uwajibikaji kwa Bunge: Inashangaza zaidi kwamba sasa imekuwa ni mtindo kwa Serikali kutoa ‘commitments' muhimu za kibajeti kwa Shirika la IMF badala ya wananchi kupitia Bunge. Bunge limepitisha Bajeti, mapitio yeyote ya Bajeti yanapaswa kuidhinishwa na Bunge. Bila kufanya hivyo maana ya Bunge kupitisha Bajeti inakuwa haina mantiki na uhuru wa Taifa letu unakuwa haupo kwetu.

Umuhimu wa Bunge kutunga haraka Sheria ya Ofisi ya Bajeti ya Bunge (Parliamentary Budget Act) sasa unaonekana waziwazi. Muswada umewasilishwa Bungeni na Wabunge binafsi kutaka kuundwa kwa mfumo wa kuisimamia Serikali katika Bajeti. Ofisi ya Spika wa Bunge ihakikishe muswada huu unachapishwa katika Gazeti la Serikali mara moja ili usomwe kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Sita wa Bunge na kutungwa kuwa sheria katika mkutano wa Saba.

Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali ilete mpango wa kupunguza matumizi Bungeni ili ujadiliwe na kuidhinishwa na Bunge kabla ya kuanza kutumika. Vinginevyo Mpango wa Serikali kwa IMF utakuwa ni kudharau wananchi na kuuza uhuru wetu kwa Shirika la Fedha la Kimataifa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mwishoni mwa miaka ya Sabini ‘toka lini Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekuwa Wizara ya Fedha ya Kimataifa (International Ministry of Finance)?'

Kabwe Zuberi Zitto, Mb Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni (NKUB)
Dar es Salaam, 10 Januari 2012.

Thread kama hii haiwezi kuwa na wachangiaji wengi....ingekuwa na heading kama 'Zitto amiliki Ghorofa la kifahari' au " Zitto achangia kuivuruga NCCR-Mageuzi' ndipo ungeona kila Rangi za Wanafiki.

Anyways,Hapo kwenye kupunguza Budget deficit kuna tatizo kubwa.Sasa hivi nadhani tuwe na tume au mamlaka kabisa ya kudhibiti government Expenditures.Tuna tataizo kubwa sana.

Pia Inabidi tuangalie njia za kuongeza Tax kwa Matajiri wakubwa lakini tuzingatie athari katika uzalishaji bila kuathiri upatikanaji wa ajira.
Tuweke malengo ya kati na muda mrefu(medium and long term planning) katika kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi na kutoa vipaumbele kwa nakampuni yatakayoongeza volume ya employment katika investments.Ili kuongeza Revenue in future ni lazima tupanue Tax base wakati huo huo tukiangalia njia ya kukusanya kodi ambayo imekuwa ikiachwa kwa miaka mingi

Tuweke policy itakayosaidia makampuni au viwanda vitakavyofanya uwekezaji.Tutoe priorities katika Ratio nzuri kati ya capital intensive Technology na Labour intensive Technology.Tukimaliza mwaka Waziri wa fedha na uchumi afanye evaluation tujue mwaka huu tumeongeza ajira kiasi gani na kupitia makampuni mangapi katika sekta binafsi.siyo muda wa kutia uzito kwenye sekta zisizo Rasmi tena.

Kuna tataizo katika kukusanya kodi kwenye makampuni ya madini.Kwa mfano utagundua wizi uliotaka kufanyika Geita gold mine ulionyesha ni kiasi gani hawa watu wanazalisha.Matofali zaidi ya 30 ya dhahabu yenye kg 24 kila moja na ni mzigo wa wiki 1 tu?

Angalia hizi figure hapa chini.

Currently one ounce is sold $1608. 1 ounce = 31.1g.
It means 1g of gold is $51.7042. 1kg of gold=$51704.2. 30 bricks of gold x 24 = 720Kg.
Weekly shipment = 51704.2x720= $37,227,024
Monthly shipment 37,227,024x4.3=$160,076,203.2
Annual shipment= $160,076,203.2x12=$1,920,914,438.4

Je wanalipa kodi kiasi gani kwa mwaka? Ina maana uzalishaji kwenye makampuni kama TBL uko juu kuliko hawa watu wa Madini?
 
Wazo zuri lakini elimu hii inafikishwaje kwa Mwananchi wa chini Mtanzania,anaeishi Kazulamimba Kigoma au Isungangwanda Shinyanga,kwamba Serikali yake ina mkakati wa kuondoa fedha kwenye bajeti ya maendeleo yake hivyo afaamishwe asishangae kuona daraja lake linalopita kijijini kwao au mradi wa visima haujengwi kwa kuwa fedha ya mradi huo imekatwa na Waziri wake wa Fedha na Uchumi kwa kufuata ushauri wa Shirika la Fedha la Dunia [IMF].

Zitto na wenzake kambi ya upinzani, nao wawe na ubunifu wa kufikisha elimu hii kwa Wananchi wa Manyovu Kigoma au Kinampanda Singida kama walivyotufikishia hii ambayo wanajf wamepata japo nakara iliyotumwa kwa waziri wa fedha na uchumi kama ushauri wa mapendekezo kwa Serikali kama ushauri toka kambi ya upinzani.

Ni vyema kama Zitto na wenzie ambao wako upinzani kama kweli wanawatakia mema Watanzania taarifa kama hii wangetafuta vipindi vya TV,kama ITV,DTV.TBC One na Radio,Radio one na kuongea na Wanachi Wa Tanzania nzima kwa kuwaambia nini Waziri wao wa Fedha na Uchumi anakusudia kufanya na wao wanampa ushauri gani kuepusha madhara na mateso kwa Wananchi.|

Hii ni elimu muhimu na ni kichocheo cha kuamsha ufahamu wa Watanzania, isiishie kwa wanajf tu hata kupitia elimu ya vipindi vya TV Wananchi wa kawaida wanaweza kueleweshwa kwa njia na mifano myepesi.Wakina Zitto na Kambi yake Wizara ya Fedha na uchumi kivuli wawe ni wabunifu wa kuyakuza na kuongeza ufahamu wa Mambo ya Fedha na Uchumi kiufahamu kwa Wananchi, haswa wa mambo sensitive kama haya ambayo ki mfumo huwa yanaonekana kama ni ya ufahamu wa wachache ndani ya mfumo na kumbe impact yake ni Taifa zima na kwa vizazi.

Tufike sehemu upinzani msikae kuwa mnasubilia Bunge ndio kipindi mnajulikana mpo kumbe kipindi kama hiki ndio muhimu nyie kuwa wachokonozi wa mambo ya Fedha na Uchumi kama hili la mpango huu wa IMFna mengineyo yanayohusu maendeleo na ustawi wa Taifa zima,kisha nyie Kambi ya Upinzani mnajenga hoja kwa kuomba vipindi vya Radio na TV au Press Conference kisha mnamwaga elimu kwa Wananchi kwa Taarifa kisha mnatuachia Wananchi kupima kati ya Zitto kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi kivuli na Mkuro Waziri Halisi wa Fedha na Uchumi nani Mkweli hivyo Wananchi kujua nani ahaminike kwa umma.

Hamuitaji kukaa na kusubilia mpaka Bunge lije kukaa huku mambo muhimu,mmeshikilia mikononi mwenu kila siku ndio maana tunawamind kwenye scandal hata kama ni za uongo kwa kuwa tunayoyasikia kitaani kwenye runinga taarifa za habari ni ziara za Wakuu wa Nchi na sio hoja za msingi kutoka midomoni mwenu kuhusu maisha yetu, yenu na Watakao kuja.
 
tATIZO SIO sERIKALI WALA VIONGOZI BALI SISI WANANCHI TU WABINAFSI MNO KILAMTU ANATAKA MBUNGE WAKE ALETE MAENDELEO JIMBONI HIVYO SERIKALI KUBAKI BILA MSIMAMIZI. UMEFIKWA WAKATI SASA WATANZANIA TUKASAMEHE HOJA YA WABUNGE KULETA MAENDELEO KATIKA MAJIMBO MOJA ILI WAWEKEZE NGUVU ZAO KATIKA KUISIMAMIA SERIKALI ILI IWEZE KUKUSANYA FEDHA ZA KUTOSHA KUTOKANA NA KODI, MADINI RASLIMALI, BIASHARA NA KILIMI ILI MAENDELO HAYO MAJIMBONI YAWEZE KUPATIKANA.

TUKIENDELEA NA UBINAFSI HUU WA KUWAPIMA KWA VIWANGI VYA MAENDELO MAJIMBONI BADALA YA NAMNA WANAVYOTEKELEZA WAJIBU WAQ KUISMAMIA SERIKALI AMBAYO NDIO YENYE DHAMANA JUU YA UKUSANYAJI KODI, MADINI NA RASLIMALI ZETU NA MATUMIZI YA FEDHA ZITOKANZO NA VYNAZO HIVYO UMASKINI NA TANZANIA UTAENDELEA KUWA KAMA PETE NA KIDOLE.
 
Thread kama hii haiwezi kuwa na wachangiaji wengi....ingekuwa na heading kama 'Zitto amiliki Ghorofa la kifahari' au " Zitto achangia kuivuruga NCCR-Mageuzi' ndipo ungeona kila Rangi za Wanafiki.

Anyways,Hapo kwenye kupunguza Budget deficit kuna tatizo kubwa.Sasa hivi nadhani tuwe na tume au mamlaka kabisa ya kudhibiti government Expenditures.Tuna tataizo kubwa sana.

Pia Inabidi tuangalie njia za kuongeza Tax kwa Matajiri wakubwa lakini tuzingatie athari katika uzalishaji bila kuathiri upatikanaji wa ajira.
Tuweke malengo ya kati na muda mrefu(medium and long term planning) katika kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi na kutoa vipaumbele kwa nakampuni yatakayoongeza volume ya employment katika investments.Ili kuongeza Revenue in future ni lazima tupanue Tax base wakati huo huo tukiangalia njia ya kukusanya kodi ambayo imekuwa ikiachwa kwa miaka mingi

Tuweke policy itakayosaidia makampuni au viwanda vitakavyofanya uwekezaji.Tutoe priorities katika Ratio nzuri kati ya capital intensive Technology na Labour intensive Technology.Tukimaliza mwaka Waziri wa fedha na uchumi afanye evaluation tujue mwaka huu tumeongeza ajira kiasi gani na kupitia makampuni mangapi katika sekta binafsi.siyo muda wa kutia uzito kwenye sekta zisizo Rasmi tena.

Kuna tataizo katika kukusanya kodi kwenye makampuni ya madini.Kwa mfano utagundua wizi uliotaka kufanyika Geita gold mine ulionyesha ni kiasi gani hawa watu wanazalisha.Matofali zaidi ya 30 ya dhahabu yenye kg 24 kila moja na ni mzigo wa wiki 1 tu?

Angalia hizi figure hapa chini.

Currently one ounce is sold $1608. 1 ounce = 31.1g.
It means 1g of gold is $51.7042. 1kg of gold=$51704.2. 30 bricks of gold x 24 = 720Kg.
Weekly shipment = 51704.2x720= $37,227,024
Monthly shipment 37,227,024x4.3=$160,076,203.2
Annual shipment= $160,076,203.2x12=$1,920,914,438.4

Je wanalipa kodi kiasi gani kwa mwaka? Ina maana uzalishaji kwenye makampuni kama TBL uko juu kuliko hawa watu wa Madini?

hAYA NDIO AINA YA MASWALI WABUNGE WETU WANAPASWA KIJULIZA NA KUULIZA BUNGENI LAKINI HAWAWEZI KUPTAMUDA HUO KWA KUWA WANAFAHAMUA KUWA SISI WANANCHI TUNATOA KIPUMBELE ZIDI KWA MAJI, SHULE BARABARA N.K MAJIMBONI. SASA BILA KUKUSANYA HIZI FEDHA HAYO MAENDELO MAJIMBONI YATAFIKA VIPI?
 
Kweli naungana na Kamanda katika kupunguza matumizi yasio ualazima kwa viongozi wa serikali hususani magari ya kifahari.Waziri/katibu mkuu/jaji/wakurugezi wa mashirika ya uma wanakaa Osterbay /Masaki ofisi ipo Posta, 4WD V8 ya nini?

Tunatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza mafuta petrol na desel wangeangalia jinsi gani ya kupunguza hili.Njia zipo ambazo ni kuencourage Public transport kuingia katikati ya miji/majiji hili litaambatana sambamba na kupunguza foleni ambayo pia kimsingi inachangia ongezeko la matumizi makubwa ya mafuta.Wanaoingia katikati ya jiji na magari binafsi watozwe tozo fulani ni moja ya kuongeza mapato japo ni kiwango kidogo.

Kuna mambo yanayoweza kufanywa kwa malengo ya muda mrefu na yatasaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Mfano kuboresha usafiri wa reli ili mizigo yote mizito isafirishwe kwa njia hiyo.Kwa sasa serikali inatumia fedh nyingi kila kukicha katika kukarabati barabara zetu kuu kutokana na uharibifu unaofanywa na kusafirisha mizigo mizito kwa njia ya barabara.
 
hAYA NDIO AINA YA MASWALI WABUNGE WETU WANAPASWA KIJULIZA NA KUULIZA BUNGENI LAKINI HAWAWEZI KUPTAMUDA HUO KWA KUWA WANAFAHAMUA KUWA SISI WANANCHI TUNATOA KIPUMBELE ZIDI KWA MAJI, SHULE BARABARA N.K MAJIMBONI. SASA BILA KUKUSANYA HIZI FEDHA HAYO MAENDELO MAJIMBONI YATAFIKA VIPI?

WATANABE,

Tuna watu ambao hawawezi kujikita katika kujadili issues...wengi wao wanapenda kujadili watu,vijembe/mipasho na matukio.Hawana muda na mambo ya kitaifa na wala hawapendi kujisomea

Kibaya zaidi wanatumia muda mwingi kuangalia majimboni mwao ni nani anaweza kuibuka kuchuana nao.Baadhi yao wameanza kujenga chuki hata na baadhi ya vijana majimboni mwao

Ni bora sasa suala la matumizi ya serikali likajadiliwa na ikiwezekana upelekwe mswada mkali au kuboresha sheria iliyopo kupamabana na matumizi mabaya ya fedha za umma na ufisadi

Kama yupo mbunge anaona uzito wa hili anaweza kukusanya maoni,tutkatoa maoni na yeye afanye kazi ya lobbying kwa ajili ya hili
 
Kama wewe unavyoanza kuundiwa zengwe kisa Kinondoni!
 
Zitto Kabwe ni matatizo matupu! Chadema kuweni makini na huyo mbunge wenu hajji majukumu ya Chama cha upinzani. Unaishauri serikali ipunguze matumiIzi kwa mujibu wa kanuni zipi?

Austerity measures zinapaswa kupelekwa Bungeni na kujadiliwa of course najua CCM wana a huge majority hawawezi kuipinga serikali Yao. Utaratibu unaotumika haueleweki mara anaibuka Katibu Mkuu Kiongozi anaagiza kupunguza ajira by 50% lakini
kwa sababu ni utawala wa imla hakuna anayesema au kukemea Nakumbuka mjinga Ruksa alisitisha ajira matokeo yake inabidi Mkapa kuongeza muda wa kustaafu hadi miaka 60 aka Jakaya na kuwpatia watumishi wanaotakiwa
wastaafu kwa mujibu wa sheria mikataba ya miaka miwili miwili kuanzia Katibu Mkuu Kiongizi hadi makamanda wa Polisi wa Mikoa.

Kila mtu anahamia atakavyp hakuna official policy. Zitto badala ya kuainusha madudu hayo Watz. walolala waikimboe Tz come 2015 anishauri ibane matumizi. Walikaa kula posho Dodoma for more than two month kupitisha budget ambayo haina hata mwelekeo kwa kutumia mungkari wa Kichama na pia wamekaa two weeks November bila kuona uchumi unashuka bora warudi Wajerumani tuanze moja!
 
Jamani pengine mimi ndio sikusoma vizuri. Lakini nilichosoma hapo juu haya ni maoni ya kambi ya Upinzani..
Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga kuondolewa kwa miradi ya maendeleo ili kupunguza matumizi ya Serikali. Kimsingi wakati kama huu ambapo hali ya uchumi ni mbaya na vijana wengi vijijini na mijini hawana ajira tunasisitiza umuhimu wa kutumia zaidi kwenye miradi ya maendeleo.
Sioni Zitto anamwambia mtu au kuwa ni mawazo yake binafsi bali ni mkusanyiko wa mawazo tofauti ya kambi hiyo na imewakilisha na sii mtu mwingine ila yule alopaswa kuwakilisha..Pengine sijawasoma vizuri haswa matatizo yako wapi lakini binafsi sioni tatizo lolote.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
sanks Zitto!! - you always tell them but they pretend to be deaf! hopefully this tyme they will listen.
 
Back
Top Bottom