Zitto aibua Ufisadi mpya BOT, ni wa karibu 620bil

Hivi JF siku hizi kuna watu wa aina gani? hata kugawa bilioni 55 kwa say 1000 mtu hawezi?Jamani tuache majung fitna na kushadadia tuuuu. Ninavyojua mimi BOT inawafanyakazi kama 1,500 hivi nchi nzima. Sasa bil 55 gawa kwa hao ni sh.milioni kama 37 hivi. Huo ni mkopo wa nyumba. Sasa tuwe wa kweli na kumuogopa Mungu wetu hivi mfanyakazi kukopeshwa 37m mkopo wa nyumba ni hela nying sana kweli? hivi hiyo 37 m unajenga nyumba ya hadhi gani? hiyo si bei ya kiwanja tu?hebu fanyeni utafiti jamani acheni kuchukua vitu blindly sababu tu kasema Zito.Jamaa ni mjanja ndio maana hakuenda kwenye details alijua low thinkers watashadadia tu.

hao wafanyakazi ni mpaka wafagizi na walinzi au ni wa ngazi ipi , na wana haki ya kukopeshwa? Pia usisahau kuna zile bilioni 34 za mfuko wa mikopo ya nyumba , kuhusu mahesabu ngoja tukukokotolee kinagaubaga , JF is full of Mathematicians...
 
Hivi ni macho yangu au vipi au ? kama ni kweli ni Billion 55 na wafanyakazi 1,000 na kama hizo hela zigawane sawa sawa

ina maana kila mfanyakazi angepata mkopo wa Tshs. 55,000,000 au milioni hamsini na tano (55,000,000,000/1000)

Tuwe wawazi kwa mambo mengine.
Tshs 550,000,000/=
 
Nafikiri nimekosea njia hili jukwaa la stress huwa sitembelei maana kupata ban hapa ni kufumba na kufumbua macho
Aaahhh inatia hasira £&€$#$¥€¥$€#€$$¥$€
 
Hivi ni macho yangu au vipi au ? kama ni kweli ni Billion 55 na wafanyakazi 1,000 na kama hizo hela zigawane sawa sawa

ina maana kila mfanyakazi angepata mkopo wa Tshs. 55,000,000 au milioni hamsini na tano (55,000,000,000/1000)

Tuwe wawazi kwa mambo mengine.

haya ndio mahesabu yake , sasa ni haki watu kukopeshana kwa mwaka mmoja mabilioni yote hayo?
 
Duh, 55 billion, huu ni mtaji tosha wa kuanzisha Bank tena kubwa tu! FNB, Amana, Equity, ECO, zote zimeanza na Mtaji usiozidi Million 35 Killa moja! Balaa!
 
Hivi JF siku hizi kuna watu wa aina gani? hata kugawa bilioni 55 kwa say 1000 mtu hawezi?Jamani tuache majung fitna na kushadadia tuuuu. Ninavyojua mimi BOT inawafanyakazi kama 1,500 hivi nchi nzima. Sasa bil 55 gawa kwa hao ni sh.milioni kama 37 hivi. Huo ni mkopo wa nyumba. Sasa tuwe wa kweli na kumuogopa Mungu wetu hivi mfanyakazi kukopeshwa 37m mkopo wa nyumba ni hela nying sana kweli? hivi hiyo 37 m unajenga nyumba ya hadhi gani? hiyo si bei ya kiwanja tu?hebu fanyeni utafiti jamani acheni kuchukua vitu blindly sababu tu kasema Zito.Jamaa ni mjanja ndio maana hakuenda kwenye details alijua low thinkers watashadadia tu.

Wewe lazima ni mnufaika, ukisoma hoja hapo utaona kuwa mwaka 2011 walijikopesha jumla ya Bilioni 37 , mwaka 2012 wakajikopesha tena bilioni 55 za nyumba , magari nk.
aidha , ukisoma kwa makini utaona kuwa kuna mfuko wenye bilioni 34 kwa ajili ya mikopo ya nyumba , wewe unaona ni haki?
 
ii. Mfuko wa Elimu wa Mwl.Nyerere (Mwl.Nyerere Scholarship fund) , mnamomwaka 2009 BOT ilianzisha mfuko huo kwa ajili ya kuwapa udhamini wasichanakusoma shahada ya kwanza kwa wale ambao watafaulu vizuri masomo ya Sayansi naHisabati na hadi mwezi Juni 2011 Mfuko ulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 1.715 .Aidha , katikamwaka wa fedha 2012 mpaka tarehe 30 Juni mfuko ulikuwana shilingi 0 Je,ni utaratibu gani huwa unatumika katika kupatafedha hizi na ni wanafunzi wangapi mpaka mwaka huu wa fedha wamesomeshwa namfuko huu na wanasoma vyuo gani?

Hahhahah, VICK KAMATA anahusika hapa na Degree ya Uingereza.
 
Kwa hyo wafanyakazi wote BOT wako na mkopo. Hahahahahaaaaaaa danganya toto hyo. Ile ya EPA walisema ni Usalama wa Taifa mara Balali alidanganya sasa ni mikopo kwa wafanyakazi.

TULIME PAMOJA TUPALILIE PAMOJA TUVUNE PAMOJA KULA ULE MWENYEWE.
 
Hivi ni macho yangu au vipi au ? kama ni kweli ni Billion 55 na wafanyakazi 1,000 na kama hizo hela zigawane sawa sawa

ina maana kila mfanyakazi angepata mkopo wa Tshs. 55,000,000 au milioni hamsini na tano (55,000,000,000/1000)

Tuwe wawazi kwa mambo mengine.

Kwahiyo kila mwaka wanakopeshana 55MIl ?
Kumbuka na mwak jana wamebunya tena 30Bil + mwaka juzi tena 30 Bil. +

Alafu hili la wafanya kazi ni UONGO haiwezekani BOT ikawa na wafanya kazi 1000, Benki kubwa nchi hii ni NMB inatawi ila wilaya na inawafanya 2000+ tu,.
Sembuse hii BOT yenye matawi hata Mwanza, arusha na Mbeya ?
 
TIB yenyewe inatakiwa iwe na mtaji wa 100Bil. Lakini mpaka leo hawajapata hela.

N kweli mkuu, mwaka wa fedha 2009/10 walitoa 50 Billion. Na mwaka 2010/11 wakatoa 42 Billion za Kilimo Kwanza. Hadi leo hawajatoa hata senti ingine. Kwa maana hiyo TIB inadai
(1) 2009/10 - Shs 50 Billion
(2) 2010/11 - Shs 100 Billion
(3) 2011/12 - Shs 100 Billion
(4) 2012/13 - Shs 100 Billion
na mwaka wa Tano yaani 2013/14 pia wanatakiwa wapewe 100 Billion

Mkuu wa Kaya ana ahadi za kihuni kweli manake aliahidi 100 Billion kila mwaka for 5 years consecutive, lakini hatimizi ahadi!
 
wafanyakazi wako zaidi ya 1500.Hili nina uhakika nalo ukigawanya utapata kama m37 hivi. hii si hela nyingi kwa mkopo wa nyumba. Tuache majungu jamaaaaaa. kama kuna sababu ya kweli tuseme ila kwa hili hizi ni fitna tu. mwambieni zitto aseme BOT inawafanyakazi wangapi?
 
Wakopeshwe wote kwa mkupuo wa mwaka mmoja ? Za mwaka jana ziko wapi? Wameshalipa na kumaliza deni husika la bilioni 34 za mwaka uliopita? Mbona waalimu, askari , na wafanyakazi wengine hawana hizo fursa?
 
mh hizo nyumba wanajenga kila mwaka? je kila mfanyakaz wa BOT amekopa? hicho ni kiasi kikubwa sana cha pesa. hivi BOT ina wafanyakazi wengi kuliko NMB?
 
Manufaa ya upinzani, mbona taasisi kama BOT kwa miaka nenda rudi wafanyakazi wake hawalingani kabisa na jamii ya wafanyakazi wa serikali ya tz, taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wake usioingiliwa wa kuendesha mambo yake, na kibaya zaidi umekuwa utaratibu wa kifisadi zaidi, dr ndullu jua hata zimbabwe kuna benki kuu na ina gavana, kwa hiyo msiwafanye watu wawaheshimu kwa utangulizi wa dr na jina kubwa la BOT, bali wawaheshimu na kuwakumbuka kwa uzalendo na weledi katika kulitumikia taifa, mmejaa ufisadi mpaka mnapoteza maana ya elimu zenu
 
Huu ni ufisadi nimethibitisha sasa kwani waziri wa fedha hakuzungumza lolote na badala yake kasema kuwa atajibu kwa maandishi baadae wakati ameacha muda wa dk 25 kwa mujibu wa Spika, ,sijui hii nchi inaenda wapi ....
 
The country is built by hardworking whitehearted individuals but the proucts is eaten (consumed) by sharp edged teeth corrupt minority.
 
Hivi BOT kuna wafanyakazi wangapi? Maana wakiwa wako jumla ya wafanyakazi 5000 kila mmoja atakuwa amepata wastani wa shilingli milioni 100 kama mkopo kwa mwaka ....this is a hell of money......

Wacha majungu na fitna kijana.

52,000,000,000 / 5000 =10,400,000

Uliishia chumba cha ngapi? Au ndio kukimbia umande?

Haya tuseme wapo wafanyakazi 1000 unapata ngapi hapo?

Hebu acheni fitna na wivu na nyie nendeni mkafanye MSC Strathclyde na CPA.
 
Back
Top Bottom