Hadi Desemba 2023, deni la Serikali lilikuwa trilioni 87.47 ikilinganishwa na trilioni 74.75 ya 2022

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Hadi mwezi Desemba 2023, deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 87.47 ikilinganishwa na shilingi trilioni 74.75 katika kipindi kama hicho mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 17.0. Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi trilioni 56.79 na deni la ndani ni shilingi trilioni 30.67.

Ongezeko la deni limetokana na ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, elimu, afya, kilimo, mifugo, nishati na maji.

Aidha, katika kipindi cha miezi 6 kuanzia Julai hadi Desemba, 2023 deni la Serikali limeongezeka kwa shilingi trilioni 7.14 kutoka shilingi trilioni 80.33 mwezi Juni, 2023 kufikia shilingi trilioni 87.47 mwezi Desemba, 2023.

Uchambuzi wa Kamati umebaini kuwa deni la nje limeongezeka kutokana na mabadiliko ya viwango vya kubadilisha fedha pamoja na riba kwa mikopo inayotegemea mabadiliko ya hali ya soko (floating rate).

Asilimia 28.3 ya deni la nje lipo kwenye riba inayobadilika kulingana na soko (flexible exchange rate) na asilimia 71.7 ya deni ina riba isiyobadilika (fixed exchange rate).

Kamati inashauri masuala yafuatayo: -
i. Kuimarisha makusanyo ya ndani na kuendelea kutekeleza Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo – DCF ili kuondokana na mikopo ya kibiashara ambayo ina riba kubwa na inayobadilika kulingana na hali ya soko;

ii. Serikali ihakikishe Taasisi zake zinazojiendesha kibiashara zinalipa mikopo yake ili kuepuka kihatarishi cha Mikopo Sanjari; na

iii. Mikopo ya kibiashara ielekezwe katika miradi ambayo inaleta matokeo kwa muda mfupi
 
Hizo chache mno, tutalipa tu, yaani kwa miradi inayoendelea, hizo fedha ndogo sana, huku mareli, mameli, madaraja, malami, madarasa ya mashule, mabwawa ya umeme....zilistahili kuwa hata trilioni 300
 
Serikali itakamatwa lini ili kulipa hizo deni?

Mbona huku mitaani watu wanakamatana na kupelekana police kila uchwao kwa sababu ya madeni ya buku buku tu?

Hizo trilion bado hakuna wa kumkata mkopaji??
 
Waache kutoa elimu bure ni utapeli huo

Watu walipe ada tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu na kusiwe na mikopo elimu ya juu
 
Back
Top Bottom