Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,755
- Thread starter
- #61
Bila kuwasahau wataalam wa Tatunane.....
Hawa jamaa walikuwa wakiupiga muziki wetu wa asili kwa kutumia ala/vyombo vya kisasa.....Hawa waliutangaza sana muziki wetu nje ya nchi(hasa Denmark na Uholanzi) ambako walikuwa wakifanya maonesho ya mara kwa mara....
Bendi hii iliundwa na wa wanamuziki kama Omary Naliene(mtaalamu wa kucheza ngoma,kupiga marimba,kuimba na kupuliza filimbi huyu,alikuwa anapuliza filimbi kwa pua), Charles Mhuto(Mpiga drums), Mahdi Tumbo(Mpiga gitaa la solo na muimbaji), Seif Rengwe(Mpuliza trumpet), Teddy Mbaraka(Mpiga gitaa la besi na muimbaji), Omary Abdallah Dulla Mnanga(Mpiga ngoma na muimbaji) na Kipara Yusuph(Mpiga ngoma)
Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Kulalama,Sangula,Msewe,Wasknaia,Furahia ngoma,Utamaduni,Pili, Naukala,Dunia, Tanzania, Dogoli, Zanzibar, Mangaka, Juma ndala, Kala hasara, Mdundiko, Filimbi, Ludewa na nyingine nyingi ambazo ziliitangaza nchi yetu katika medani ya muziki wa kimataifa....