ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mimi bana sikinde tuuu, jamani sikinde watani wangu msondo mtaniwia radhi. Dah kuna vibao nikivisikia mpaka natokwa na jasho kuna kitu km Duniani Kuna mambo, wikiendi nalala kwa taabu, kwa ujumla sikinde you rock my heart!! ningekuwa na pesa ninge invest trillions pale basi tu sina kitu. haya kuna hawa marques du zaire enzi za kamanyola bila jasho kuna kibao kama dola mtoto wa Dodoma( yakaa yaka eeehn mwana mama ndimandimaeee mwana mama ...... mtoto wa dodoma) kuna kinanda flani kinapigwa mle na gitaa yaani ni raha tupu!! inanikumbusha sana dada yangu marehemu Mage jamani wakati niko Sumbawanga alikuja toka Dar basi anaziimba hizi nyimbo za makwizzz aaah jamani KAMANYOLA BILA JASHO! ikaja telemuka telemuka chekechaaaaaa

Hapa tuko pamoja sana mkuu.....Sikinde daima(damu damu).....

Pia zamani nilikuwa mnazi wa Vijana Jazz wana Pambamoto kabla haijaanza kupotea na kufifia kabisa....
 
View attachment 31871

Haya ni matangazo ya bendi zetu za zamani kwenye magazeti yetu ya kipindi kile....

Picha kwa hisani ya John Kitime
matangazo.jpg
 
Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............Hakika ya kale ni dhahabu...
Mi mdau sana wa nyimbo za bendi ulizotaja. Swali langu kwako ni umewakumbuka vp wanamziki wote hao? Naomba uanachama kwenye maktaba yako.
 
Duu mkuu umetukumbusha mbaaaali enzi hizo za DDC - keko, magomeni kondoa, kariakoo, mkirikiti bar, wapi wapi bar- maduka mawili, mtakuja bar kwikwi kwi.....
 
Bala upo juu kama Hussein Zomboko..au mzee Kufii na Maestro Masoud masoud ( huyu bwana anaujua vyema mziki wa dance).Inaonekana Maktaba ta RTD ipo nyumbani kwako Balantanda.

Ntarejea nikikamilisha maelezo mazuri ya Bendi za UDA jazz, Urafiki na Biashara Jazz band!! Zaman tuliiziimba sana kule DHW!!
 
Mkuu uko juu...

Mimi nakumbuka Orchestra Makassy chini ya Mzee Kitenzogu "Mzee" Makassy...enzi hizo akiwa na marehemu Dr Remmy Ongala kabla hajaanzisha Matimila...
 
Hahaaaaaaaaa,nimekusoma Home boy,nitafanya utaratibu wa kukutumia,shaka ondoa Nkwingwa...


bwana mzee unanikumbusha mbali sana,lakini ndio hivyo miziki inakufa sijui nani aje aokoe hili
kila siku nafikiria nitoe mchango gani bendi hizi zirudi lakini nashindwa
nakuuliza kaswali kadago, reheni bichuka yuko hai?je yuko wapi na maisha yake yakoje?
 
bwana mzee unanikumbusha mbali sana,lakini ndio hivyo miziki inakufa sijui nani aje aokoe hili
kila siku nafikiria nitoe mchango gani bendi hizi zirudi lakini nashindwa
nakuuliza kaswali kadago,reheni bichuka yuko hai?je yuko wapi na maisha yake yakoje?

Si wewe tu mkuu wangu,kila mtu akizikumbuka bendi kama Marquis(wana sendema,zembwela n.k),Sambulumaa,Vijana Jazz(pambamoto),Washirika Tanzania Stars(watunjatanjata,njata one),Tancut Almas(wana fimbo lugoda,kinyekinye kisonzo tisa kumi mangala),JKT Mafinga(kimulimuli),JKT Kimbunga stereo,Ngorongoro Heroes Band(sukuma push),Kurugenzi Jazz,Six Manyara,Bima Lee(Magnet tingisha),Super Matimila(Bongo beats,talakaka),Zaita Musica(wana zuke muselebende),MK Group(wana Ngulupa tupatupa dansi),MK Beats(wana tukunyema,wowowo),MK Sound,OSS(wana masantula ngoma mpwita,dukuduku,ndekule,power Iranda,rashikanda wasaa),MCA Internationa(wana munisandesal,Orch. Makassy,Magereza Jazz(Mkote Ngoma),Bicco Stars(wana kindumbwe ndumbwe),Super Rainbow,Bantu Group Band(wana kasimbagu kaabuka),Legho Stars(wana sopabango),Afriso International ya Lovy Longomba na nyingine nyingi lazima utatokwa chozi mkuu,kifo cha bendi hizi ndio kifo cha muziki wetu ule mtamu tulioupenda,haupo tena.......Nyingi kati ya bendi hizi zimekufa na zilizopo zinajikongoja........Natamani kuurudisha wakati nyuma aisee....

Kuhusu Super Stereo Hassan Rehani Bitchuka,kwa sasa yupo Mlimani Park orch wana Sikinde ambako alihamia akitokea Msondo Ngoma....
 
Si wewe tu mkuu wangu,kila mtu akizikumbuka bendi kama Marquis(wana sendema,zembwela n.k),Sambulumaa,Vijana Jazz(pambamoto),Washirika Tanzania Stars(watunjatanjata,njata one),Tancut Almas(wana fimbo lugoda,kinyekinye kisonzo tisa kumi mangala),JKT Mafinga(kimulimuli),JKT Kimbunga stereo,Ngorongoro Heroes Band(sukuma push),Kurugenzi Jazz,Six Manyara,Bima Lee(Magnet tingisha),Super Matimila(Bongo beats,talakaka),Zaita Musica(wana zuke muselebende),MK Group(wana Ngulupa tupatupa dansi),MK Beats(wana tukunyema,wowowo),MK Sound,OSS(wana masantula ngoma mpwita,dukuduku,ndekule,power Iranda,rashikanda wasaa),MCA Internationa(wana munisandesal,Orch. Makassy,Magereza Jazz(Mkote Ngoma),Bicco Stars(wana kindumbwe ndumbwe),Super Rainbow,Bantu Group Band(wana kasimbagu kaabuka),Legho Stars(wana sopabango),Afriso International ya Lovy Longomba na nyingine nyingi.......Nyingi kati ya bendi hizi zimekufa na zilizopo zinajikongoja........Natamani kuurudisha wakati nyuma aisee....

Kuhusu Super Stereo Hassan Rehani Bitchuka,kwa sasa yupo Mlimani Park orch wana Sikinde ambako alihamia akitokea Msondo Ngoma....


asante mkuu
nitaenda sikinde kuonana na bitchuka,nafikiri nataka ajue kwamba tunamweshimu sana sana kutokana
na kazi yake
 
Mkuu uko juu...

Mimi nakumbuka Orchestra Makassy chini ya Mzee Kitenzogu "Mzee" Makassy...enzi hizo akiwa na marehemu Dr Remmy Ongala kabla hajaanzisha Matimila...

Hawa nao(Orchestra Makassy) wamechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa Muziki wetu.....Kilikuwa ni kikosi matata kabisa cha enzi zake,fikiria nyimbo kama Mambo bado, Siku ya Kufa, Mke wangu, Harusi ya Mwanza, Namolema, Athumani Valuvalu, Sisca, Mosese, Nakolela Cherie, Binadamu hatosheki, Kufilisika Si Kilema, Zimbabwe, Ciska, Bakoka bolakate, Ubaya wa nini, Muungano(CCM) na nyingine nyingi utaona ni jinsi gani bendi hii ilikuwa moto wa kuotea mbali.....Jamaa walikuwa wanatisha kutokana na vipaji vya muziki vilivyokuwa vinaunda bendi hii....

Bendii hii ya Orchetra Makassy ilikuwa inaundwa na wanamuziki kama mzee mwenyewe Kitenzogu Makassy ,Ramdhani Mtoro Ongara(Dk Remmy) ,Mose se Sengo(Fan fan) ,Tshimanga Kalala Assossa, Aimala Mbutu, Kassim Mganga, Kyanga Songwa, John Kitime, Andy Swebe, Choyo Godjero, Issa Nundu, Keppy Kiombile na wengine ambao wamenitoka kidogo....
 
Bila kuwasahau Bicco Stars Band wana kindumbwendumbwe.......

Hawa nao walikuwa moto wa kuotea mbali maana walitamba sana na wimbo wao maarufu wa Muuza chipsi utunzi wake Ramadhan Kinguti(Kinguti system)...Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa kindumbwendumbe(chalia)....Ilikuwa burudani kweli kusikiliza tungo tamu za bendi hii ambayo iliibuka ghafla...Kingine kilichovutia kwa bendi hii ni kwamba ilikuwa na mpiga kinanda mwanamke mwanamama Asia Darwesh kitu ambacho kilikuwa ni cha ajabu sana kipindi hicho....

Bendi hii japo haikukaa muda mrefu sana ilitamba na nyimbo kama Muuza chipsi, Visa vya wenye nyumba, Nyumba ya kifahari, Magreth Maggie, Leyla, Kitambaa cha kichwa, nyumba ya kupanga na nyingine....

Bicco Stars iliundwa na wanamuziki kama Ramadhani Kinguti(Kinguti system), Asia Darwesh, Mafumu Bilali Bombenga, Fresh Jumbe, Andy Swebe, Aimala Mbutu, Hamisi Amigolas, Nyota Abdallah Kinguti(Nyota Waziri wa Njenje) na wengine.....
 
Pia ilikuwepo bendi ya Afriso Ngoma/Afriso International iliyokuwa ikimilikiwa na Mzee Juma Mwendapole(R.I.P),bendi hii ilikuwa chini ya uongozi wa marehemu Lovy Longomba ambaye Mungu alimjalia sauti kwa kweli(kama Eddy Sheggy vile)....Bendi hii ilitamba sana Bongo kipindi kile na binafsi nilikuwa napenda sana kuisikiliza sauti ya Lovy Longomba.....

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Elly, Pesa ni maua, Amana mpenzi, Estther Usituchonganishe,Zaina na nyingine nyingi ambazo zilitamba enzi zake...

Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Lovy Longomba, Nyota Kinguti (Nyota Waziri),Kassim Mponda, Madaraka Uledi, Kinguti system, Anania Ngoliga, Toffy Mvambe, Salim Shaaban, Maliky Star , John Maida, Peter Kazadi, Robert Mabrish, Mjusi Shemboza, Ayub Karume, Magoma Sony,Juma Urungu, Mbaraka Othman Belly Kankonde na wengine wengi.
 
Bala, huwakumbuki Mzinga Troupe ya Moro? Waliibuka na kibao kiitwacho mazoea yanikondesha kilichotungwa na kuimbwa na Issa Mrisho kwa sauti nzuri sana. Kibao hicho kikipigwa hata leo utadhani ni cha jana. Baadhi ya Masahiri ni haya

Mazoea yananikondesha eee
Sio kama nimelishwa kizizi, labda,
Laini siamini alijua matatizo

Hata Mjusi hata Kinyonga,
wao hula Vijidudu hai
Hasa vyenye kurukaruka, mbona yeye hana mbawaaaa
Anapata riziki yakeee, sembuse mimi mwanadamu

Bala, umtaja Kurugenzi Jazz, bila shaka ni ile ya Arusha iliyokuwa na kibao kikali sana Wivu

Wivu ukizidi nyumbani mapenzi yapunguaa
Wivu usiyo na maana waleta hasara
Umefanya kitu gani, bibi umemkataza kufanya kazi
ati sababu wachelelewa nyumbani....


Kibwagizo
Maisha ya leo, ni kufanya kazi
Mke na mume, kusaidiana
 
Mi mdau sana wa nyimbo za bendi ulizotaja. Swali langu kwako ni umewakumbuka vp wanamziki wote hao? Naomba uanachama kwenye maktaba yako.

Ukweli ni kwamba ninaupenda sana muziki wa dansi na maktaba yangu mimi kwa asilimia kubwa ni kichwa changu ambacho nachelea kujisifu kwamba Mungu kakibariki kuweza kuhifadhi kumbukumbu nyingi tu mkuu wangu......Pia ninayo hazina ya nyimbo nyingi sana za zamani kwenye kompyuta yangu......

Nilikuwa mpenzi sana wa vipindi vya muziki RTD,nilikuwa sikosi vipindi kama Misakato, Club Raha Leo Show, Disco Show, Chaguo la msikilizaji, Starehe na BP, Kijaruba, Top ten show na vipindi vya salamu kama Jambo na mchana mwema ambavyo vilikuwa vikipiga sana muziki wa dansi....

Pia ni msikilizaji mzuri sana wa vipindi vya Muziki vya radio zetu za FM kama Salamu za Milenia(RFA na Wambura Mtani),Hizi nazo(Radio One) na Enzi hizo(Radio Uhuru) ...

Hebu pitia pitia thread hizi hapa chini:

https://www.jamiiforums.com/entertainment/43161-tumetoka-mbali-unawakumbuka-watu-hawa-na-mambo-haya.html

[URL="https://www.jamiiforums.com/entertainment/113422-enzi-hizo-s02.html"]https://www.jamiiforums.com/entertainment/113422-enzi-hizo-s02.html

[URL]https://www.jamiiforums.com/entertainment/50455-tukumbushane-wimbo-bora-wenye-jina-la-kike.html
[/URL][/URL]
 
Mkuu Balantanda big up sanaaa!!
Tusisahau pia UDA Jazz wana Bayankata...kama sikosei Ally Choky alianzia huko
 
Bala, huwakumbuki Mzinga Troupe ya Moro? Waliibuka na kibao kiitwacho mazoea yanikondesha kilichotungwa na kuimbwa na Issa Mrisho kwa sauti nzuri sana. Kibao hicho kikipigwa hata leo utadhani ni cha jana. Baadhi ya Masahiri ni haya

Mazoea yananikondesha eee
Sio kama nimelishwa kizizi, labda,
Laini siamini alijua matatizo

Hata Mjusi hata Kinyonga,
wao hula Vijidudu hai
Hasa vyenye kurukaruka, mbona yeye hana mbawaaaa
Anapata riziki yakeee, sembuse mimi mwanadamu

Bala, umtaja Kurugenzi Jazz, bila shaka ni ile ya Arusha iliyokuwa na kibao kikali sana Wivu

Wivu ukizidi nyumbani mapenzi yapunguaa
Wivu usiyo na maana waleta hasara
Umefanya kitu gani, bibi umemkataza kufanya kazi
ati sababu wachelelewa nyumbani....


Kibwagizo
Maisha ya leo, ni kufanya kazi
Mke na mume, kusaidiana

Nawakumbuka sana mkuu wangu....

Unajua kipindi cha nyuma bendi za majeshi yetu zilikuwa juu sana na karibu kila jeshi lilikuwa na bendi yake kama ifuatavyo:-

1.JKT walikuwa na bendi za JKT Mafinga chini ya Zahir Ally Zorro,JKT Kimbunga Stereo,JKT Taarab ya akina Issa Matona,Shakira Ally,Elizabeth Sijila,Paticia Hilary na wengine wengi

2.JWTZ walikuwa na Mwenge Jazz(wana paselepa),Silent Inn Mwenge ya Arusha(kama sikosei) na Sanaa JWTZ ikiongozwa na Capt.John Damian Komba na hiyo ya Mzinga Troupe iliyokuwa inamilikiwa na Shirika la Mzinga Morogoro...

3.Magereza ilikuwepo bendi yao ya Magereza Jazz(wana mkote ngoma) ambao walikuwa chini yake Abel Barthazar na Nanah Njige hawa nawakumbuka kwa wimbo wao mtamu wa Ashura

4.Polisi wao walikuwa na bendi yao ya Polisi Jazz chini ya uongozi wake Kassim Mapili enzi hizo

Yaani zamani burudani ilikuwa kila sehemu.....
 
Mkuu Balantanda big up sanaaa!!
Tusisahau pia UDA Jazz wana Bayankata...kama sikosei Ally Choky alianzia huko

Wakati UDA Jazz wanatamba Ally Choki alikuwa mtoto mdogo sana mkuu,sema UDA Jazz imepitiwa na mwalimu(baba wa muziki) wa Ally Choki Komando Hamza Kalala...

Bantu Group Band ndiyo imemtoa Ally Choki japo kuna taarifa kwamba aliwahi pia kupitia bendi ya Lola Afrika ya Profesa Vulata...

Sikiliza kibao cha Baba Jane na 1 cha Bantu Group utamsikia Ally Choki kwenye kiitikio 'Mimi ooooo(mimi oooooh) Baba Jane bye bye, bado nakupenda mume wangu,baba Jane bye bye, narudi nyumbani baba Jane,baba Jane bye bye, narudi kwa baba na mama,baba Jane bye bye"......Hapo Choki ndio kwanza alikuwa anaanza kusikika katika anga za muziki wa kibongo
 
Mkuu uko juu...Mimi nakumbuka Orchestra Makassy chini ya Mzee Kitenzogu "Mzee" Makassy...enzi hizo akiwa na marehemu Dr Remmy Ongala kabla hajaanzisha Matimila...
unanikumbusha MOLEMA na siku ya kufa alioimba DR. REMMY wakati akiwa makassy. kuna mosese hawa jamaa nao waliimba bana. jf kulikuwa ns zilipendwa MODS kwa nini mmeziondoa jamani?
 
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila,Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyongise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...
kWANINI SAFU YA WAIMBAJI KARIBU WOTE WALOTAJWA HAPO JUU 'WAMENUNA' WAMEFARIKI DUNIA?
 
Haaa Bala umeturudisha kwenye mambo yetu yaleeeee,
Vijana walikuwa machachari na ndio walikuwa bendi neutral ya wapinzani wa Jadi DDC na Msondo
Umenikumbusha Dudumizi mtaalamu wa nyimbo za mapenzi[/QUOTE

Jamaa(Jerry Nashon Dudumizi) alikuwa mtunzi kwelikweli wa nyimbo za mapenzi hasa akiwa na Bima Lee na Vijana Jazz...

Angalia kama kitu hiki kitamu hapa chini ambacho ni utunzi wake..

V.I.P-Jerry Nashon 'Dudumizi"


(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,

(Dudumizi): Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yangu,ila ni wewe VIP,
Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yanguuu,iila ni weweeeee,VIP
Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa,na kisirani cha kufokewa na boss,
Nahitaji VIP wa kunibembeleza,nakutaka wewe mama,unibembeleze,
Si kwa maneno ila kunitomasatomasa,kwa mikono yako laini yenye bangili,
Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP).

Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa,na kisirani cha kufokewa na boss,
Nahitaji VIP wa kunibembeleza,nakutaka wewe mama,unibembeleze,
Si kwa maneno ila kunitomasatomasa,kwa mikono yako laini yenye bangili,
Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP)

(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,
Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo.

Dudumizi: VIP sogea karibu,ubipe busu mwanana mama

(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,

Bridge

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka


Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP,
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP
Natamani penzi live sio penzi la ndotoni,nakuomba uwe wangu VIP,
Tafadhali nakusihi, ili niondokane na ndoto za mapenzi.

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka


Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP,
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP
Natamani penzi live sio penzi la ndotoni,nakuomba uwe wangu VIP,
Tafadhali nakusihi, maaa mamaa,maaa....maaa yoooo,maa mamamaaaaaaaaaaaaaaa,
Tafadhali nakusihi, ili niondokane na ndoto za mapenzi.


Dudumizi: Ukinikubali VIP,mimi niko tayari,kubadili dini,
Ukinikubaliii VIP mimi niko tayari,kubadili dini,
Hata kama wazazi wangu hawapendi,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba)
nitafanyafanya mipango niwe nawee sambambaaa

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.


Ukinikubalii VIP,mimi niko tayari kubadili dini,
Ukinikubalii VIP,nitatoa mahaliii ya mbuzi saba,
Hata kama sina VIP,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba) nitafanyafanya mipango niwe na wewe
sambamba.

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.

:music::violin::music:
 
Back
Top Bottom