Ze Utamu blogger under arrest?

Status
Not open for further replies.
Hili ni gumu kwa akina Masanja tu, ila kwa watoto wa wakubwa ni RAHISI sana na wana PASSPORT mbilimbili au tatutatu. Tuseme uko nje, unaukana ubongo. Unarudi Tz na kuchonga pass mpya. Hivi ni shida kuchonga pale pass? Ukikwama Bongo, si unaenda hata Rwanda/Burundi kama siyo Kenya na Uganda? Pia kama mtu kaweza kuchukua Uraia wa UINGEREZA, wa Tanzania utamshinda? Mnaongelea nini hapa? Kama watu waliweza kwenda BoT na kuchota pesa, itakuwa Pass? Hebu fikirieni mara mbili kabla ya kuandika. Nalaani sikuomba URAIA wa Gabon nilipopita kule.
Mkuu Sikonge,

Looh! hilo la uraia wa Gabon limenichekesha sana. Kuna ndugu yangu huwa ananiambia anaombe apewe ubalozi hata kama ni Chechenya. Huwa nacheka lakini jamaa anasema balozi ni balozi tu hata kama ni kwenye nchi yenye matatizo.

Sheria za uraia zinasema kama una uraia wa nchi mbili kwa mfano UK na Tanzania, ukifanya kosa Tanzania, uraia wako wa UK haukusaidii na wala UK authority haiwezi kukutetea kama raia wao. Hiyo ndio hasara ya uraia wa nchi mbili.

Sasa huyu kijana kafanya makosa kwenye nchi ambayo ana gamba lake, hapo UK watamrudisha TZ kama Mtanzania tu. Suala la kwamba ana passport pia ya Uingereza hawataliweka tena maanani. Angefanya kosa nchini Kenya hapo suala lake lingeshughulikiwa kama Mwingereza.

Huu mtandao ukiuchangamkia sana unageuka kuwa kilevi kama drugs tu na mwisho wake unaingia hata kwenye madudu ya ajabu ajabu.

Nchi zilizoendelea huwa hawakurupuki kukamata mtu. Wakishahisi unahusika basi watakuchunguza hata miezi kabla ya kukushutua. Inaelekea jamaa walimjua mapema na wakaamua kuwacha tu aendelee na utundu wake mpaka walipokuwa na uhakika kwamba ni yeye.
 
Niliwaonya juu ya namna wanayotumia katika kumuandama huyu jamaa.

Naona bado wanaendelea tu, impact yake nadhani wako tayari kukabiliana nayo.

Walinywea baada ya kujua ni mtoto wa 'mwenzao' leo wameamua kumbana na kumrudisha Tz?

Ngoja tusikie ni mashtaka gani atafunguliwa. Family yake itakubali?

Invisible,

Familia yake haina "hiari" ya kukubali iwapo mtoto wao ashtakiwe au asishtakiwe. Kumkashifu KIONGOZI wa NCHI ni kuikashifu NCHI yenyewe! Alivuka mipaka, he knew the risks and consequences. After all, NOBODY is above the law, even the President!

Atashtakiwa TU! Atake asitake! Aliniboa sana huyu MKWARE! Fikiria watu wangapi walivunjiwa mahusiano yao ya faragha, walidhalilishwa, wengine ndoa zao kuvunjwa kwa UONGO na UFISADI wake, na hata waliopoteza maisha? Hakuna haja ya kumtetea mtu huyu! Ningekuwa na pesa ningefanya party ya kusheherekea kukamatwa kwake, na ningeutangazia umma kwamba nasherehekea FISADI huyu kukamatwa!

./Mwana wa Haki
 
Bora atiwe mbaroni, alidhalilisha watu sana.... ila kosa lilikuwa letu... tulikubali kutekwa na blogu yake na tuliiangalia regularly.
 
Hivi wamemfuata UK au kajileta mwenyewe? Si ana uraia wa Uingereza pia?

Mkuu, unaweza kujileta kwenye moto? huyo wamemdaka na wamemleta. cha moto atakiona amedhalilisha watu sana.. tuone fisadi huyu wa akili za watu atashughulikiwa vipi....
 
Mkuu,
Siyo frustrations. Unajua sisi Wanyamwezi na MITARA ndiyo wenyewe. Sasa kama unaanya MITARA hadi kwenye uraia, ni safi sana. Ndiyo maana Wahenga wetu walisema "Wa mbili havai moja...."

DUh..Mitara ya hivo sasa mtakuwa mnazidisha....hahahaha...ndio mitara hadi kwenye siasa manake nasikia yule mwenyekiti wa kile chama dume naye ana mitara ya vijisenti? LOL
 
akifikishwa mahakamani itakuwa sawa

lkn kwa nini walisubiri mpaka mjomba adhalilishwe ndo waamke?

cyber laws zikoje hapa?
 
naona leo mada zote hazionekani JF ni hii pekee.Kuna mambo mengi sana hapa ya kujadili sio ilipekee.
Currently Active Users Viewing This Thread: 175 (55 members and 120 guests)
josm, agika, BINTI SAYUNI, Bluray, Burn, Chakaza, Chief, COMRADE44, Congo, dash, Edson, Hofstede, Idimi, Iteitei Lya Kitee, John74e, Kaizer, Kamuna, kapuchi, kicheruka, KIFARU, kiparadar, Komamanga, Kunta Kinte, Kyachakiche, locust60, M$awa, Magehema, masaiti, Mau, Mbongo, MegaPyne, Mfunyukuzi, Mndamba, Mnhenwa Ndege, Mtanganyika, Mtanzania, mtu66, Muoldmoshi, MwanajamiiOne, Ndugu, Nesindiso Sir, Njimba Nsalilwe, nkawa, Recta, Rugishar, Sikonge, Son of Alaska, SteveD, TzPride, Wakuja, watu, Who Cares?
 
Acha Ushamba. Unaonekana una donge sana na choka mbaya. Vumbi kali sana nini? Fanya kazi na acha roho korosho. Lowassa na Mkapa (Anna) hawajabadilisha uraia. Liyumba, na kundi lake pia wana uraia wa Tz tu na wameleta hasara kubwa zaidi ya huyu Lusinde (mtani wangu).

Haina uhusiano wowote wa mtu kufanya haya madudu na kuwa na raia wa nchi mbili. Sasa wakiibuka walio na uraia wa nchi moja na huku asili yao ni Watz, na huko wanakuja kama watalii, UTAFANYA NINI? Mmemshangilia Obama wee unafikiri wote watakuwa kama Obama? Hata nje ya Tanzania ni kama Bongo, kuna WABAYA na WAZURI. Nakubaliana na Mkapa kuwa kuna Mitanzania ina WIVU WA KIJINGA.

Pole sana ndugu yangu. Hayo yalikuwa maoni yangu mimi Chokambaya..heri wewe vumbi sio kali huku ulikokania uraia wako ukapokelewa au tuseme ukolewa....mmmh Sikonge vumbi lilikuwa kali sana hasa vumbi la tumbaku ukaamua kupakacha ukaenda hukoooo walipopatengeneza pakawa pazuri...hata hivyo mtu kukana uraia wake ili apate wa nchi nyingine kwa bado ni tatizo na si wivu maana siwezi kumuonea mtu wivu kwa kufanya kitu nisichopenda mimi......mmmh hii ya Mkapa kusema wtz tuna wivu wa kijinga...nakubaliana nawe kabisa....kujiuzia mgodi kwa millioni 700 tu halafu unalipa milioni 70 nakuanza kuvuna...lazima hao watu uwaite wajinga....Mkapa the national traitor......haya bwana Sikonge.
 
Yaani huweziamini kama huyo kijana (sijui mbaba maana 39 amekwenda age) mzuri hivyo ameoza kichwani mwake!! Sitaki hata kukumbuka uchafu alikuwa akiuanika kule kwake!! Duh si mzima huyu hivi hana familia? Hajaoa?

Huko UK anafanya nini hasa kimaisha au ndo wale waliokwenda kutalii?
 
jamaa zake Bongo walishapelekewa salaam alakini hawakutaka kusikia, yule mwingine states nasikia mpaka nyumba kahama

kazi kweli kweli...washalikoroga kilichobaki ni walinywe tuu
 
Mkuu Sikonge,

Looh! hilo la uraia wa Gabon limenichekesha sana. Kuna ndugu yangu huwa ananiambia anaombe apewe ubalozi hata kama ni Chechenya. Huwa nacheka lakini jamaa anasema balozi ni balozi tu hata kama ni kwenye nchi yenye matatizo.

Sheria za uraia zinasema kama una uraia wa nchi mbili kwa mfano UK na Tanzania, ukifanya kosa Tanzania, uraia wako wa UK haukusaidii na wala UK authority haiwezi kukutetea kama raia wao. Hiyo ndio hasara ya uraia wa nchi mbili.

Sasa huyu kijana kafanya makosa kwenye nchi ambayo ana gamba lake, hapo UK watamrudisha TZ kama Mtanzania tu. Suala la kwamba ana passport pia ya Uingereza hawataliweka tena maanani. Angefanya kosa nchini Kenya hapo suala lake lingeshughulikiwa kama Mwingereza.

Huu mtandao ukiuchangamkia sana unageuka kuwa kilevi kama drugs tu na mwisho wake unaingia hata kwenye madudu ya ajabu ajabu.

Nchi zilizoendelea huwa hawakurupuki kukamata mtu. Wakishahisi unahusika basi watakuchunguza hata miezi kabla ya kukushutua. Inaelekea jamaa walimjua mapema na wakaamua kuwacha tu aendelee na utundu wake mpaka walipokuwa na uhakika kwamba ni yeye.

Mkuu check your records again. Hiyo thesis haiwezekani. Ingewezekana kama sisi tungekuwa tunaruhusu dual citizenship. Kifupi hapa alishaukana uraia wa bongo..anayejua kwamba jamaa ni Mtanzania ni wewe na si sheria. Infact huyu hata akija bongo...ubalozi wa UK..ndo utawajibika kumshughulikia raia wake..upo? Siyo mtanzania tena. Otherwise uraia wa nchi nyingine unakuwa hay=una maana. Narudia tena jamaa angeweza akashughulikiwa bongo kisheria endapo tungelikuwa tunaruhusu uraia wa nchi mbili. As it is now..the guy is just a foreigner Pronto!
 
Hili ni gumu kwa akina Masanja tu, ila kwa watoto wa wakubwa ni RAHISI sana na wana PASSPORT mbilimbili au tatutatu. Tuseme uko nje, unaukana ubongo. Unarudi Tz na kuchonga pass mpya. Hivi ni shida kuchonga pale pass? Ukikwama Bongo, si unaenda hata Rwanda/Burundi kama siyo Kenya na Uganda? Pia kama mtu kaweza kuchukua Uraia wa UINGEREZA, wa Tanzania utamshinda? Mnaongelea nini hapa? Kama watu waliweza kwenda BoT na kuchota pesa, itakuwa Pass? Hebu fikirieni mara mbili kabla ya kuandika. Nalaani sikuomba URAIA wa Gabon nilipopita kule.

Sasa mkuu inaonekana hata akina Masanja, we can take it no more!

Naanza kuusaka uraia wa Abhkazia au Osetia sasa! Maana bongo ya leo akina Masanja hatuna chetu! Ukiiba kuku unachomwa moto..ukiiba EPA unapandishwa cheo na kuwa mkurugenzi kama wa TIB-Lol!
 
Wana JF, tukubali kwamba huyu jamaa jambo alilolifanya ni baya, chafu na linatia kinyaa. Kuwa mtoto wa mkubwa ama kigogo isichukuliwe kama ni kinga ya yeye kuadhibiwa vikali.

Pamoja na kwamba serikali ilichukua muda kuifungia zeutamu na kumtafuta muhusika ingawa watu walikuwa wanalalamika usiku na mchana mpaka pale Raisi wetu alipoguswa, lakini hatuna budi kuishukuru na kuipongeza serikali kwa kumpata muhusika na kuifungia website hiyo.

Kijana ametumia muda wake kusoma computer ili atumie ujuzi wake katika kufanya vitu vya maana vyenye manufaa na faida kwa dunia na wala si kutukana na kudhalilisha binadamu.

Familia ya Malecela na Lusinde wengi wao wameenda shule vyema na wanajiheshimu vya kutosha, bila shaka ili jambo limewastua kwa kiasi kikubwa sana.
Kitu cha maana wanachoweza kufanya ni kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa serikali ili kijana wao afikishwe katika sheria na kuadhibiwa kama watu wengine, kwa hili nina amini kabisa mzee John Samweli Chigwiyemisi Malecela atahakikisha linafanyika bila upendeleo. Na kwa kufanya hivyo ndiyo wanaweza kusafisha jina lao mbele ya uso wa jamii.

Nimefurahishwa sana na kukamatwa kwake na kufungiwa mtandao wake, watu tulikuwa tunaogopa kwenda kwenye tafrija ama makutano ya aina mbalimbali kwa kuogopa kupigwa picha na kutolewa katika zeutamu.

Ni lazima akanyee debe kwa miaka mingi sana na asitoke huko bila kufanywa kitu mbaya ili ajue zeutamu inaweza ikageuka na kuwa zeuchungu.
 
Sasa mkuu inaonekana hata akina Masanja, we can take it no more!

Naanza kuusaka uraia wa Abhkazia au Osetia sasa! Maana bongo ya leo akina Masanja hatuna chetu! Ukiiba kuku unachomwa moto..ukiiba EPA unapandishwa cheo na kuwa mkurugenzi kama wa TIB-Lol!

Masanja, Afghanistan ni poa zaidi kwa maisha ya kiboda boda!! Kazi nazo ziko kibao.... mashambani hadi mijini!
 
[B said:
Masanja[/B];493304]Sasa mkuu inaonekana hata akina Masanja, we can take it no more!

Naanza kuusaka uraia wa Abhkazia au Osetia sasa! Maana bongo ya leo akina Masanja hatuna chetu! Ukiiba kuku unachomwa moto..ukiiba EPA unapandishwa cheo na kuwa mkurugenzi kama wa TIB-Lol!

umenifurahisha sana ndugu,kwa hiyo unatushauri tupige deal kubwa kubwa kama akina Farijala?
 
Laiti hizo resources zingetumika kuwatafuta wamiliki wa KAGODA !!
Lakini hapana, mambo hayaendi hivyo
not in Tanzania
not under CCM.

thanks mag3

is utamu the biggest ever crime commited by a tanzanian?

watu wa JF kwa double standards wanashabikia zeutamu kukamatwa na wakati watu wana loot nchi yetu wanatembea huru, ingekuwa hivyo wakina-obama, bush si wangekamata watu wengi sana.....

wangeshirikiana na interpool kuhakikisha hela zilizokuwa duabi, jerzey na kwinginepo zinarudi TZ ingekuwa ni jambo la maana kulikoni zeutamu

zeutamu ulikuwa ni mtambo wa tabia na watu wengi waliokuwa mule wali deserve kuwa mule

hasara ya zeutamu kwa TZ nini????

kumbuka walianza na mwanahalisi, siku hizi ukiwaandama wanakuuliza kwa nini wasikufungie uliza ITV

mkishabikia zeutamu kukamatwa, baadae mjiandae kushabikia website zingine maana yake hawataishia hapo tu
baada ya zeutamu who is next????

zeutamu ujue sio kila mtu anakuchukia na ningekuwa na uwezo ningekukingia kifua........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom