Zanzibar ni NCHI na mipaka yake sasa ndani ya KATIBA yao. Ni vigumu mno Tanzania kutawaliwa na raia wa nchi nyingine. Nilimsikia hata Maalim Seif akiyasema hayo ya kupokezana. Tulipofikia sasa sio rahisi Mzanzibar kuwa Rais wa Muungano labda ije kama ile iliomng'oa Sitta kwenye Uspika. JMK aseme kwenye CC ya CCM kwamba safari hii tunamtaka Mzanzibar kuwa Rais wa JMT kwa sababu ya minyukano na makundi yanayoitafuna CCM kwa sasa huku bara.