Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Zanzibar ni NCHI na mipaka yake sasa ndani ya KATIBA yao. Ni vigumu mno Tanzania kutawaliwa na raia wa nchi nyingine. Nilimsikia hata Maalim Seif akiyasema hayo ya kupokezana. Tulipofikia sasa sio rahisi Mzanzibar kuwa Rais wa Muungano labda ije kama ile iliomng'oa Sitta kwenye Uspika. JMK aseme kwenye CC ya CCM kwamba safari hii tunamtaka Mzanzibar kuwa Rais wa JMT kwa sababu ya minyukano na makundi yanayoitafuna CCM kwa sasa huku bara.
 
Huo utakuwa ni mwendelezo wa upuuzi wa ccm! Wakikosa namna ya kutulizana makundi yanayowatafuna ndio wanakimbilia maswala ya ukanda, visiwani na bara au jinsia. Kumbuka uchaguzi wa uvccm na sakata la Masauni. Kumbuka uchaguzi wa spika, Sitta vs Makinda. Ni upuuzi mtupu!

Kwakuwa hii nchi sio jumuia ya chama, waache waendelee na upuuzi wao ndio watajua tulivyochoka. This time I'll show up my true colour!

Period!
 
Ukiwachia huyo Salim kwa watu wa umri wake, kusema kweli sioni mwengne kutoka Zanzibar ambaye angeweza kuiongoza Tanzania, kwani wengi wao ni wale wahafidhina wa sera chakavu za CCM au wapenda kula.

Naamini wapo vijana wengi tu tatizo ni kutokuwa na jina katika duru za siasa zetu za kichama, kieneo bila ya kusahau kile ambacho kimekuwa likitutafuna muda mrefu, kidini.

Tatizo la Salim na watu wa umri kama wake, nahisi umri umepanda sana. Ingawaje umri si hoja kubwa sana bali moyo wa kuwatumikia Watanzania. Tanzania ya sasa inahitaji kuongozwa na damu mpya, damu iliyozaliwa na kukulia katika shida zetu za sasa, damu inayoelewa wapi wazee wetu wamekosea, kipi kinaitafuna Tanzania na kipi Tanzania inahitaji.

Niikipata wazo nitarejea.
 
Mtamkumbuka sana...yote hayo kutokana na ubaguzi wa rangi na dini...na mkifanya mchezo rais atakaye fuata atakuwa bomu zaidi...
 
Nawashukuru wote kwa mawazo, japo pia napinga wazo la kumfikiria Karume (mkubwa na mdogo wake) eti nao wanaweza kuwa marais wa Jamhuri. Tutafutieni mwingine huko Zanzibar kama yupo mimi nabaki na wazo langu la Salim kama chaguo bora kwa Zanzibar
 
Nawashukuru wote kwa mawazo, japo pia napinga wazo la kumfikiria Karume (mkubwa na mdogo wake) eti nao wanaweza kuwa marais wa Jamhuri. Tutafutieni mwingine huko Zanzibar kama yupo mimi nabaki na wazo langu la Salim kama chaguo bora kwa Zanzibar
SAS alidengua wakati ule Mwalimu akiwa hai, 1985 na 1995. Alipojaribu mwaka 2005 cha moto alikiona toka kwa WANAMTANDAO. Sidhani kama ana hamu ya nafasi hiyo kwa umri na afya yake mwaka 2015. Minyukano hii ya bara ikiendelea kushika kasi tunaweza kuwa na Mzanzibar akawa Rais kwa sera zilizojificha za CCM zilizompa Anna Makinda Uspika, Mohamed Chande ujaji mkuu,...
 
Nimekuwa nikihangaika sana kuuliza dhambi na makosa yaliyomfanya Salim A.Salim kushindwa kupata nafasi ya kuongoza nchi hii eti tu kwa mizengwe ya CCM ooooHizbu na kadhalika. Sasa nadhani magamba wameelewa walikosea kumchafua Salim na sasa wanataka mgombea atoke Zanzibar ili Salim aweze kuongoza na kufuta record chafu ya CCM ktk kipindi chote cha JK.

Watanzania tunasikitika tumepiga maktaimu sana kwa kukosa uongozi bora miaka hii kumi sasa bora Salim arudi na tunamuomba asikatae (huenda akasusa kwa vile walimkataa na kumuaibisha).

Ni mawazo tu, kama unadhani mwingine pia ataweza kutuongoza 2015 basi usisite kumtaja vinginevyo CCM uozo hawa watatuletea tena kiongozi mwenye kichwa cha nazi atuongoze.
Inasemekana kikwete ni mtu safi......Ila Salim A.Salim ni muuaji, Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari kipindi hicho kwemye mbio za uteuzi.
 
Mtoa mada una uhakika kuwa hiyo 2015 Tanzania itakuwepo? Wao wanataka Jamhuri yao ya Zanzibar na sisi tunaitaka Tanganyika yetu.
 
Hilo swala la kupokezana tusubiri serikali tatu. Kwa sasa hakuna rais wa URT atatoka zanzibar, maana ccm imeshakufa haiwezi tena kudictate mambo. kama sio kuchakachua 2010 isingekuwa madarakani na mjue kuwa kwa hali iliyopo uchakachuaji wowote mwingine 2015 tarajia kifo cha ccm kinachoambatana na umwagaji mkubwa wa damu. Na kwa hakika TZ haiwezi tena kuongozwa na rais bomu kama JK maana uvumilivu umefikia kikomo.
 
Nawashukuru wote kwa mawazo, japo pia napinga wazo la kumfikiria Karume (mkubwa na mdogo wake) eti nao wanaweza kuwa marais wa Jamhuri. Tutafutieni mwingine huko Zanzibar kama yupo mimi nabaki na wazo langu la Salim kama chaguo bora kwa Zanzibar


Usiwe conservative dada! Swala la Salum liliisha siku nyingi. Hapa tunajadili raisi ajae sio wa leo au jana. Inawezekana alikuwa Mzuri wakati huo na vipimo vyako vya wakati huo vikakuonesha kuwa ni bora. Leo ni miaka sita na tunajadili swala la miaka kumi tangu wakati huo. Bado ni yeye tu ndiye anastahili kuwa rais!? Huku ni kujidhalilisha, kujidharau na kuendekeza fikra mgando. Yaani tunamfikiria mtu yuleyule kwa miaka kumi!? Kwenye duru za siasa za kileo hao huwa ni washauri na wazee wenye kuheshimika kwenye chama, na sio viongozi tena!
 
Rais wa JMT kutoka ZNZ tena kulingana na geopolitics ni ndoto. Believe me una Nationalism i.e Utanganyika umeshaanza kuwaingia watu wa bara baada ya chokochoko za mda mrefu za Wa-ZNZ. CCM nao wanafahamu kumletea mgombea U-Rais wa JMT kutoka ZNZ is a like shooting themselves on foot. Because watakuwa wanawa-alliniate more >95% voters ambao wako Tanganyika. Mtaji wa kura za JMT ziko Tanganyika hivyo mgombea kutoka ZNZ is un electable.

CCM wakifanya hivyo basi CDM watachekelea kimoyomoyo maana safari ya kwenda magogoni itakuwa imerahisishwa. Kama JK mwenyewe Mtangayika tunaambiwa alipata 48% ya votes huyo mzanzibari sio ndiyo atapata 8% tu.
 
Nimekuwa nikihangaika sana kuuliza dhambi na makosa yaliyomfanya Salim A.Salim kushindwa kupata nafasi ya kuongoza nchi hii eti tu kwa mizengwe ya CCM ooooHizbu na kadhalika. Sasa nadhani magamba wameelewa walikosea kumchafua Salim na sasa wanataka mgombea atoke Zanzibar ili Salim aweze kuongoza na kufuta record chafu ya CCM ktk kipindi chote cha JK.

Watanzania tunasikitika tumepiga maktaimu sana kwa kukosa uongozi bora miaka hii kumi sasa bora Salim arudi na tunamuomba asikatae (huenda akasusa kwa vile walimkataa na kumuaibisha).

Ni mawazo tu, kama unadhani mwingine pia ataweza kutuongoza 2015 basi usisite kumtaja vinginevyo CCM uozo hawa watatuletea tena kiongozi mwenye kichwa cha nazi atuongoze.

Tanzania ni ya wote si msikiti. Mnataka kutumia ujanja wa kitoto kufanikisha lengo la muislamu tena? haiwezekani mmetosha maana sasa tabu hadi sekondari watoto wanadai nch ijae misikiti
 
Lakini kwa nini mnafikiria kiCCM CCM kwani rais ajaye lazima atoke CCM? Mimi naona huo mjadala hauna mantiki hasa kwa kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi. Ila ninachoamini ni kwamba CCM haina influence tena na siasa za URT. Wakirogwa wampitishe Makinda mwingine itakula kwao. i
Kumbukeni JK alisema hatomwachia mkristo hii nchi.Msitumike!
 
huyu Mpemba wa Cuf Maalim Sharifu baada ya kupewa Madaraka
ya kutawala Wazanzibar wenzake ambao ni kama wilaya moja ya
Tanganiyika watu ambao ni kama 600,000 laki Sita sasa anajidanganya
kuwa anaweza basi akapewa madaraka ya kuwatawala watanganyika wao
wapemba sisis ndiyo tulio waoa na sisi ndiyo wanaume ndiyo maana kila kitu
wanatutengemea kuanzia umeme awalipi bill , Maji , Chakula, madawa ,ulinzi
sasa jamani hawa watu mbona awatosheki nani anaweza kuwa rais ???????

Jambo la kujiuliza nyie mnae Rais wenu serikalli yenu sasa huku bara tanganyika
mnataka nini kama siyo upumbafu na kutafuta maneno na watu sisi tumeshawachoka
na hatuoni faida ya kuwa na nyie bado mnatungangania tu hakuna faida yoyote ya kuwa
na hawo watu sasa tunataka serikali moja kama mnataka urais wa kupokezana siyo mnajifanyia
chako chako chetu chako acheni kudeka deka na kuomba vyeo vya huruma na hizi chokochoko
zinaletwa na wapemba ,kwanza siyo wammoja wapemba na waunguja ni maadiui urafiki wa mashaka
 
Nahisi anaandaliwa rais wa sasa kule zenji (Dr. Shein) kuwa mgombea wa urais JMT. Kwa mtazamo wangu kutuletea Mzenji this time, that will be a "technical error".
 
Tutakubali mzenji atuongoze tu iwapo katiba ijayo itaitambua Tanganyika namaanisha serikali tatu, vinginevyo wasidhubutu hata kidogo na wala watanganyika tusikubali hili litokee kwani tutakuwa tunaukaribisha ukoloni wa kisultani
 
Back
Top Bottom