Yule jamaa aliyetokea mabwepande saa 12 asubuhi alikuwa anenda wapi?

Mwangendage

Member
Jan 11, 2012
69
2
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.
 
muda huo wa saa 12 asubuhi ndugu yetu Dr Ulimboka alikua ameishajivuta kwa taabu hadi apo barabarani..ikumbukwe pia kwamba alijikaza kiume hadi akazikata zile kamba uliZOKUA UMEMFUNGA miguuni..

kwa iyo mpita njia alimkuta Dr barabarani na si msituni kama unavyojaribu kubadili maana..........

nimeamua kupoteza muda wangu kukuelezea kile ambacho unakifahamu lakini unaamua kukitafutia loop hole....anyway mmefikia wapi kumjibu Gwajima?tunasubiri
 
Si mbaya kuhojiwa. Mi nilishangaa zaidi mpaka Raisi Dhaifu aliingiza jina lake kwenye hotuba yake.
 
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.

Naomba nikufahamishe sisi watu wa maeneo hayo tunaamka saa 9 usiku kuanza safari ya kufika barabarani kwenda kwenye shughuli za kuvuja jasho. Ila usiwe mpuuzi kiasi cha kumuuliza mtu aliyechukua jukumu la kibinadamu kumsaidia tu mwingine wewe unadai ahojiwe. Si ajabu polisi hawapewi ushirikiano kwa vipengere vya kipuuzi kama hivyo
 
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.

Yaani wewe unashangaa saa 12 Asubuhi, kwa maisha ya Bunju ukitaka kufika Mwenge saa moja yakubidi kuamka saa 9:30 hadi 10:00 alfajili. Na hapo inategemea unaishi Bunju ipi, kama huko Mabwe ni balaa!!!!

Vinginevyo utafika Mwenge saa 4 Asubuhi.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
mkuu unaishi dar au nje ya dar?
Saa kumi na mbiki mbona ni muda wa kawaida sana kwa wakazi wa dsm kuwahi kwenda kwenye mihangaiko?
 
nimeambiwa huko Mabwe pande ni mabali sana na msitu mnene na pia ni reserve ya Taifa so hakuna shughuli binafsi ndiyo maana nauliza huyo jamaa alitokea wapi huko mabwe?
 
huyo jamaa ana hamana yake Mbinguni, nadhani hata BWANA, atambariki hapa hapa duniani, kama sio yeye basi kizazi chake
 
ni kati ya maswali makini ya kujiuliza na si kumlaumu mleta mada.....mleta mada YOU ARE A GREAT THINKER
 
Si mbaya kuhojiwa. Mi nilishangaa zaidi mpaka Raisi Dhaifu aliingiza jina lake kwenye hotuba yake.
That was how far police investigation went.
knowing the his identity and no profile, nothing more.
 
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.

Common sense is not always common; Pole
 
Dk, Uli mwenyewe alisema amejikokota mpaka barabarani, ndiko alikopatia msaada. Wewe haya Mabwe pande ni msitu mnene umejuaje?
 
kitu kimoja cha kumshukuru ni kumsaidia DR WETU MPENDWA,sidhan kama angekua na nia mbaya si angemuacha tu porini au angemmalizia lkn yeye alimsaidia so Mungu ambariki sana na tunaomba kama kuna mtu anaeweza kupata detail zake atupe ili tumpongeze au apelekwe kwa madr,ili ajulikane nafkiri watafurai sana kumfahamu
 
nimeambiwa huko Mabwe pande ni mabali sana na msitu mnene na pia ni reserve ya Taifa so hakuna shughuli binafsi ndiyo maana nauliza huyo jamaa alitokea wapi huko mabwe?

Kuna msitu wa Mabwepande na makazi ya Mabwepande ambapo hata waathirika wa mafuriko wamepelekwa. Sema umeteleza kwenye hili suala kama unavyoanza kujieleza
 
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.

kuelimika ni kitu kizuri sana.....! Na maumivu ya kichwa huanza taratibu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom