Yu Wapi Askari Mkama Sharp?

Aisee mungu amrehemu...nilimshuhudia akiwaswaga vijana 9 walioleta vurugu taifa mpaka kituo cha polis I changombe peke yake.
 
wakuu habari

wale watoto wa mjini wa enzi hizo miaka ya tisini hili jina la mkamashamu hakuna asiyekuwa analijua
ni polisi machachari ambaye hajawahi tokea kwa tanzania

mkamashamu huyu bwana alikuwa anabeba pingu, kirungu, bastola, smg zote yeye tu na zote kazining'iniza

mkamashamu huyu huyu alikuwa anaweza kwenda kukamata kundi la vibaka hata ishirini na wote akawafunga mashati na kuwapeleka mpaka polisi

mkamashamu huyu alikuwa akikaa uwanja wa taifa kwenye mechi kubwa kubwa kulikuwa hakuna cha vurugu wala kukuru kakara za siku hizi

mkamashamu huyu huyu alikuwa akisema sitaki vurugu watu walikuwa wanatuli autafikiri wamemwagiwa maji ya moto

ila mkamashamu alipotea ghafla

na kuna conspirancy kibao kuhusu mkamashamu

wengine wanasema mkamashamu yuko jela sasa hivi

wengine wanasema mkamashamu amekwishafariki

wale wanaomkumbuka huyu jamaa nani anaweza kutuambia yuko wapi huyu jamaa

na sifa zake ambazo bado ziko kwenye memory ya kichwa chako waweza ku share na sisi

karibuni kwenye mada........
ni kweli aliitwa mkama sharp, huyu alishafariki tangu mwaka 2007, alizikwa huko maeneo ya kibara bunda mara, hadi anafariki alifikia cheo cha nyota moja. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, amina!
 
Ni Mkama Sharp jamaa alikua na mikwara sana ana bastola kiunoni, rungu,pingu na farasi.Ukiambiwa Mkama anakuja enzi hizo unataka kuruka ukuta Taifa lazima uchachawe.
Mkama alifariki na alienda kuzikwa kwao Majita huko
 
namkumbuka Sajini Sharp enzi zile. kwa kweli polisi ilikua polisi kweli hata majambazi walimkubali Sharp. RIP SHARP

sikubahatika kumfahamu. vipi anafanana na yule koplo wa ferry..kigamboni!??

anyway huwa najiuliza nini kilitokea mpaka askari wetu wa sasa wanachukiwa na kudharaulika kiasi hiki?

je si ni hawa hawa kina Mkama Sharp na wengine wenye sifa nzuri kama yeye waliowapokea na kuwafundisha kazi?

Ni wapi tulikosea?

mzee mmoja aliwahi kusema, "tunakuwa wa kwanza kuwalaumu vijana wa leo kwa mabaya wanayoyafanya huku tukijifanya kusahau kuwa ni sisi tuliowalea."
 
Ni Mkama Sharp jamaa alikua na mikwara sana ana bastola kiunoni, rungu,pingu na farasi.Ukiambiwa Mkama anakuja enzi hizo unataka kuruka ukuta Taifa lazima uchachawe.
Mkama alifariki na alienda kuzikwa kwao Majita huko
haikuwa bastora,ni mfoko unaohifadhi bastora,ni moja ya mikwara yake,rip mkama sharp.tuliokulia mishion quarters tunakukumbuka sana.
 
Usafiri wake mkubwa ulikuwa ni baiskeli na ule wembamba wake ukiambiwa na mambo anayoyafanya huwezi kuamini.
 
wakuu habari

wale watoto wa mjini wa enzi hizo miaka ya tisini hili jina la mkamashamu hakuna asiyekuwa analijua
ni polisi machachari ambaye hajawahi tokea kwa tanzania

mkamashamu huyu bwana alikuwa anabeba pingu, kirungu, bastola, smg zote yeye tu na zote kazining'iniza

mkamashamu huyu huyu alikuwa anaweza kwenda kukamata kundi la vibaka hata ishirini na wote akawafunga mashati na kuwapeleka mpaka polisi

mkamashamu huyu alikuwa akikaa uwanja wa taifa kwenye mechi kubwa kubwa kulikuwa hakuna cha vurugu wala kukuru kakara za siku hizi

mkamashamu huyu huyu alikuwa akisema sitaki vurugu watu walikuwa wanatuli autafikiri wamemwagiwa maji ya moto

ila mkamashamu alipotea ghafla

na kuna conspirancy kibao kuhusu mkamashamu

wengine wanasema mkamashamu yuko jela sasa hivi

wengine wanasema mkamashamu amekwishafariki

wale wanaomkumbuka huyu jamaa nani anaweza kutuambia yuko wapi huyu jamaa

na sifa zake ambazo bado ziko kwenye memory ya kichwa chako waweza ku share na sisi

karibuni kwenye mada........

mwingine maarufu alikuwa anaitwa JUMA KICHWA.
 
Namkumbuka huyu jamaa ni nilishawahi kumuona siku moja tu kariakoo akiwa kafungisha watu mashati. Alikuwa Mwembamba kama RELI ila huwezi kuamini Ma-Train kama TGV yalikuwa yakipita pale bila Mikwaruzo.

Jamaa alipendwa na Majambazi, Vibaka na watu wa kawaida. Mungu ampe mapumzisho mema.
 
Mm ni Mkama Sharp Chombo cha dola nakuamuru shuka chini kabla cjakukata, nikikukamata break ya kwanza Central...! Nayakumbuka haya maneno cku moja kwenye Shindano la Ndondi alishika Mic na kuamuru waliokuwa wamepanda juu ya Miti kuchungulia show, baada ya Tangazo jamaa walirukaje? Pingu, Kirungu, Bastola, Mbwa, Farasi vyote vilikuwa vyake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom