Yu Wapi Askari Mkama Sharp?

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,855
8,253
Kwa wale wakazi wa Dar kuanzia miaka ya mwishoni mwa `1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 pale kituo cha polisi Msimbazi kulikuwa na askari mmoja mkakamavu kwelikweli ambaye alikuwa kiboko cha makonda na madereva jeuri na sugu wa daladala,wakati wote alikuwa akitembea na vitendea kazi vyake muhimu kama vile bastola,pingu na rungu huku buti zake zikishine na uniform zake zikiwa safi na zimepigwa pasi kwa kutumia wanga,hata inzi alikuwa anaogopa kutua kwenye nguo zake,yuko tofauti na askari wa siku hizi ambao wanavitambi,uniform chafu na sifa yake kuu ilikuwa ni UKAKAMAVU NA KUTOCHUKUA KITU KIDOGO,alikuwa ahongeki.
 
Huyu jamaa alishakufa muda mrefu tuu,namkumbuka sana nambwembwe zake uwanja wa taifa akiwa na farasi na bastola mbili mbili,kazi ilikuwa kwetu waruka ukuta!!
 
Asante kwa kunisaidia kama kazaliwa mwka wa 2YK asiparamie asiyeyajua
 
Oh Mungu amrehemu kwa kweli nilikuwa namfikiria sana huyu askari kwa kuipenda kazi yake ,hope wengine wangejifunza,
 
sasa hata mnatuchanganya mara maruhumu ,oh mwingine anakula vyuku tumweelewa nani sasa
 
Eh kwaheri ,kesi ya rushwa tena! ama kweli mdudu rushwa si mashikhara hata kidogo,huanza taraatibu
 
Naona kama kawaida yetu badala ya kutoa jibu la kueleweka kila mtu anarusha jibu lake ilimradi aonekanae anamjua sana. Muulizaji ningekushauri uende kituo cha Msimbazi au makao Makuu ya Polisi ukamuulizie.
 
Wakuu habari,

Wale watoto wa mjini wa enzi hizo miaka ya tisini hili jina la mkamashamu hakuna asiyekuwa analijua
ni polisi machachari ambaye hajawahi tokea kwa Tanzania.

Mkama Sharp huyu bwana alikuwa anabeba pingu, kirungu, bastola, smg zote yeye tu na zote kazining'iniza.

Mkama sharp huyu huyu alikuwa anaweza kwenda kukamata kundi la vibaka hata ishirini na wote akawafunga mashati na kuwapeleka mpaka polisi.

Mkama Sharp huyu alikuwa akikaa uwanja wa taifa kwenye mechi kubwa kubwa kulikuwa hakuna cha vurugu wala kukuru kakara za siku hizi.

Mkama Sharp huyu huyu alikuwa akisema sitaki vurugu watu walikuwa wanatuli autafikiri wamemwagiwa maji ya moto.

Mkama sharp alipotea ghafla na kuna conspirancy kibao kuhusu Mkama sharp,wengine wanasema yuko jela sasa hivi wengine wanasema amekwishafariki.

Wale wanaomkumbuka huyu jamaa nani anaweza kutuambia yuko wapi huyu jamaa na sifa zake ambazo bado ziko kwenye memory ya kichwa chako waweza ku share na sisi.

Karibuni kwenye mada........
 
Sio Mkamashamu ila ni Mkama Sharp, alikua ni Corporal yaani mwenye V mbili begani. Huyu alishafariki dunia na kuzikwa kwao mkoa wa Mara.

Mara ya mwisho kumuona alikuwa osteray polisi miaka ya 2004/2005 alikuwa na cheo cha major(staff sajent),kwa kijeshi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom