Yes madam Speaker, We are stupid!

Aliyeidhinisha nyongeza ya posho ni "Ridhiwani Kikwete", na signature yake ndo inayoonekana kwenye docs. za Anne makinda pale mjengoni!
 
-NGOs tusaidieni katika hili.
-Vyama vya Wafanyakazi vikiongozwa na TUCTA, mkiamua posho hizi zitashuka.
-Vyama vya SIASA hasa visivyo na WABUNGE mko wapi? Ruzuku hammo, posho pia hamumo.
Spika, fedha ya kulipana posho hizi mpya mmepata wapi au kilichoandikwa RaiaMwema ni kweli?
 
Zimeongezwa bila idhini ya rais wa jamhuri :lol:

Hivi ukiwa na mamlaka ya kukubali au kukataa jambo halafu badala ya kufanya uamuzi ukaamua kuwaandikia watu walio chini yako "Memo" kuwa "Mnaweza kuamua kuhusu suala hili kwa kuzingatia mazingira ya sasa nchini pamoja na mwongozo wa busara zenu" una maanisha nini hasa? Je kwa mfano wakiamua kukubali jambo hilo baada ya kuzingatia mazingira na mwongozo wa busara zao utasema hukuwaruhusu kufanya uamuzi? Hiki kwa ufupi ndicho kilichotokea kwenye sakata la posho za kukaa/kusinzia za wabunge.
 
nafikiri kuna wabunge ambao ni member hapa jf wangekuja humu watuambie vp kwenye acount zao mzigo umeingia kiasi gani? lkn pia nadhani hawa wabunge wetu wangekuwa kidogo na hofu ya Mungu, ugumu wa maisha sio wa kwao tu ni kwa kila mtanzania km wanaona malipo yao hayatoshi si waiache hiyo kazi ya ubunge, maana sidhani km kuna mtu analazimishwa kufanya kazi isiyo na maslahi,khs madai kwamba wanatoa hela zao mfukoni kuwapa watu, hakuna aliyewatuma ht mimi nawapaga omba omba pale mnazi mmoja, nikamlilie nani
 
Rais wangu JMK:
-Nilidhani umeshindwa kuamua juu akina Lowasa, Chenge. Sababu zilikuwa wazi kuona hata kwa kipofu.
-Ukashindwa tena kuamua juu ya mafisadi wa EPA. Hili nalo lilikuwa wazi kwa wengi.
-KATIBA ya JMT inavurugwa kila uchao na akina Jussa. Uliapa kuilinda. Bado haujaamua.
-Hili dogo nalo la posho za Wabunge linakushinda! Haiwezekani Rais wangu. Kwani unagombea tena 2015?
 
Hapa kuna tatizo kubwa, rais hajaaprove, wanalipana... je kuna kupoteza kazi?? kurudisha posho?? kufuja mali ya umma? fraud??? au ndio sisi wajinga tuliwao?
 
Rais wangu JMK:
-Nilidhani umeshindwa kuamua juu akina Lowasa, Chenge. Sababu zilikuwa wazi kuona hata kwa kipofu.
-Ukashindwa tena kuamua juu ya mafisadi wa EPA. Hili nalo lilikuwa wazi kwa wengi.
-KATIBA ya JMT inavurugwa kila uchao na akina Jussa. Uliapa kuilinda. Bado haujaamua.
-Hili dogo nalo la posho za Wabunge linakushinda! Haiwezekani Rais wangu. Kwani unagombea tena 2015?
likimshinda hata la posho itakua balaa
 
Hapa kuna tatizo kubwa, rais hajaaprove, wanalipana... je kuna kupoteza kazi?? kurudisha posho?? kufuja mali ya umma? fraud??? au ndio sisi wajinga tuliwao?
Hivi ninyi mnataka JK mpaka awafanyeje ndio mumjuwe ni mtu wa namna gani!!?? yaani wewe na akili zako timamu unaamini kweli kwamba JK hajaidhinisha hizi posho mpya? poleni sana.
 
Hapa kuna tatizo kubwa, rais hajaaprove, wanalipana... je kuna kupoteza kazi?? kurudisha posho?? kufuja mali ya umma? fraud??? au ndio sisi wajinga tuliwao?
Hili wamelichukulia kama amuzi la ndani ya muhimili huru wa dola, Bunge. Rais alipewa taarifa tu. Kama ulimsikia Ndugai anasema kwenye mihimili mingine wanalipana sana na Bunge haliulizwi ingawa ndilo linalopitisha bajeti ya Serikali na Mahakama. Wazee wa nchi hii wameamua kunyang'anyana mbao litote. Tusubiri kuzama tu kama ile meli ya maraha ya Concordia.
 
hili ni janga kama mafuriko na mabomu ya gongo la mboto. kwa busara za kawaida ni bora angekaa kimya, sijaidhinisha posho, je kaidhinisha nani mbona wamelipwa. pinda kaitisha kikao na madazktari kaenda mwenyewe, kawambia waripoti hospitalini vinginevyo atawafukuza kazi - hawajaripoti na kazi hawajafukuzwa. eeeeh nchi ina uongozi kweli !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nadhani WABUNGE wetu wamekaa wakatafakari wakakumbana na UKWELI mmoja ambao haupingiki. Uwezekano wa wengi wao kurudi Bungeni mwishoni mwa 2015 ni finyu sana hasa wenzangu wa CCM. Wafanyeje sasa. Ni kuchukua chao mapema, kwa wingi kadri wanavyoweza.
 
Waheshimiwa sana wabunge wetu watukufu hupatiwa posha ya sh. 200,000/= pale tu wanapo saini mahudhurio. Ila waandishi wa habari kwa uwongo wao wameamua kupotosha habari ili kuwagombanisha wabunge watukufu na wapiga kura wao. Kwanza kaposho kenyewe ni kiduchu tu wala hakatoshi. Sisi wananchi wenye shida za magonjwa na misiba ndio tutanufaika na kaposho hako. Waandishi wa habari wakome kabisa kutugombanisha na wawakilishi wetu. Kama hivi madaktari walivyo goma ni kaposho hako hako kametumika kuwapeleka ndugu zetu wagonjwa mahututi kwa waganga wa jadi.! eboo!!!
 
Back
Top Bottom