Yes madam Speaker, We are stupid!

Zmeongezwa tena kibabe.. Maana kama raisi hajatia baraka zake bas spika na pinda wametumia ubabe..!
 
Hili la madakatari linaonekana kutukera zaidi ya mengine pengine ni kwasababu kazi yao inagusa maisha yetu moja kwa moja.
Kumekuwa na kauli kama za 'kukosa uzalendo', kazi ya wito n.k.
Kwa vile tunaogopa kukosa huduma zao na kupoteza maisha basi lawama ni juu ya kukosa uzalendo na kazi ya wito.

Nimeuliza maswali haya na wale wanaopinga mgomo wa madaktari hawalijibu. Hivi uzalendo unaanzia kwa nani na unaishia kwa nani.
Pili, hivi kazi ya udaktari haiuruhusu mtu kuwa na maisha ni mpaka akanyagwe kichwani kwa 'kosa' la kuwa mtaalam muhimu sana.

Ninavyofahamu, uzalendo ni suala la kila mtu. Wabunge ambao wanatembea juu ya zulia lenye bendera ya taifa na kula sehemu kubwa ya keki ya taifa ndio wangetuongoza katka uzalendo.
Wabunge si wataalam na yoyote yule mwenye mdomo anaweza kuwa mbunge, lakini si kila mtu aweza kuwa mwalimu au daktari. Uwepo wa wabunge ni heshima ya uzalendo wanaopewa na jamii ndiyo maana hakuna qualification.

Kama mbunge anayepata ( 130,000 kwa sasa) bado anataka apewe 330,000 KWA SIKU kwasababu maisha ni magumu hatuoni hili tunaona 'stupidity' ya yule anayeuliza kwanini wagonjwa walale chini basi we're real stupid.
Kama hatuoni kuwa mbunge anapaswa kuwa mzalendo bali tunaona madai ya masilahi kama usaliti, we're real stupid

Endapo hatuoni mil 64 kwa siku kwa posho za wabunge tu zingeweza kununua vitanda katika wodi moja basi we're stupid.

Hivi kwanini ukisema sijatosheka ionekane ni ukosefu wa uzalendo, lakini yule aliyekula na kusaza na sasa anatupa jalalani aonekana shujaa!!


Off topic: Comment number 55 imetumwatumwa na Bakuza kwa kutumia avatar yangu. Nakanusha ya kuwa hayo si maoni yangu
A very elaborate answer to mkandara et al.....
 
Unaishi nchi gani ndugu yangu!! wanyonge wa nchi hii unaowatetea ni bahati mbaya sana hawajui haki zao otherwise wangekuwepo wooote leo barabarani kwa yanafofanywa na watawala wa nchi hii......believe me.....sasa hivi imebaki kila mtu kuanza kuitafuta haki yake kwa nafasi yake......when your basic employment rights are not met by the employer(despite persistent requests)kinachobaki ni strikes tu...there is no point for morality here....kwani madaktari wao malaika wanaoishi mbinguni??madaktari ni employees wenye madai ya msingi yasiyosikilizwa na waajiri....Mbona huwazungumzii wabunge wanaopokea 200,000 na wanakaa kimya...wakati hao ndio tungetegemea wawe wa kwanza kuwazungumzia raia maskini waliowapa kura??........unawalaumu madaktari bure kwani wao robots!!......ndugu yangu..udaktari ni fani ambayo inadharauliwa sana na watawala hapa tz(just do a research on how doctors are treated in other countries in africa alafu linganisha na tz).My brother...of all the people you should throw stones at are your pathetic Government and not the doctors who are just fighting for their rights....just like any other employees who know their unsatisfied rights.....
Mkuu nadhani bado kabisa hujanielewa na hutanielewa kwa sababu unafikiria Kikugandanyika - Na ndio maana napingana na dhana, itifaki za asili ya utumwa wa mtanzania kufikiria kwamba fedha ndio msingi wa maendeleo. Kudai imekuwa kudai fedha badala ya kudai haki na freedom ambayo ndio tangulizi..

Sote tunaona hakuna justice kwa wabunge kujiongezea Posho..Hapa tulipo sote tunapiga vita Posho za wabunge - sawa? Sasa tumefanya nini kuonyesha tunapinga posho hizo!. Nambie hata kazi moja tuloifanya wananchi kupinga posho hizi zaidi ya Chadema na NCCR walioondoka Bungeni na wakachekwa mitaani..Tumefanya nini?..hakuna zaidi ya kumshukuru Mungu na kuendelea kulaani ili walaaniwe kwa dua la kuku limfike mwewe!
Halafu juu ya yote haya anatokea nguchiro naye anavizia banda la kuku, hawa madaktari nao wanataka wapewe posho kama wabunge, sisi wananchi tunaona bora nao wapewe!.. Ghafla tunabadilisha mtazamo wetu badala ya kulaani posho tunawaunga mkono sasa madaktari ili nao wapewe posho kwa sababu Wabunge wanachukua, ati wao sio robot.. Kwani nani Robot nchini kwetu?.. Hizo fedha za kuwalipa wabunge na madaktari zinatoka wapi kama sio mfukoni mwa wewe mwananchi mlipa kodi maskini ambaye unaipinga serikali hii na madai ya kupuuzi kama haya au mnafikiri zinachotwa benki kuu mfuko wa EPA na Meremeta. Je, tunapodai na wengine wapewe ndio inatuondoa ktk stupidity?..au nasi tunapodai ujinga ule ule wa wabunge ndio inatuweka ktk U stupid kama wao?...

Madai yetu mkuu wangu hayana base, na hii inamaanisha tumekata tamaa ktk kupinga posho za Wabunge hivyo kama ni kupata posho kila mtu apewe. Leo madaktari kesho walimu na kesho kutwa itafuata watumishi wengine kwa kufanya migomo ambayo inatokana na kwanini madaktari wamepewa sisi hatukupewa. Kwa nini tusidai mfumo bora wa mishahara kwa watumishi wa Umma. Hawa madaktari walipoajiriwa hawakujua kwamba mishahara yao ni midogo? Wewe unapokwenda kuomba kazi ukaambia mshahara wako utakuwa kiasi kadhaa na ukaweka saini mkataba kukubali yote, inakuwaje unapoanza kazi unataka kulipwa zaidi wakati ulikubali masharti ya kwanza!..Hutaki kazi acha kaombe kazi sehemu nyingine lakini sio kufanya mgomo ili uongezewe malipo ya posho kwa sababu wabunge wamepewa.

Mkuu wangu kazi ya Udaktari ni sawa na Usaint, Daktari ni taaluma inayojali kuokoa maisha ya watu kwanza kabla ya kila kitu na unapokubali mshahara fulani mambo mengine yote yanakuwa pembeni hasa vipozea kama posho. Daktari ni sawa na Firefighter au askari jukumu lake kubwa ni kuokoa maisha... Kila siku anapokuwa kazini ni sawa na yupo vitani kuokoa maisha ya watu na huwezi kuacha kuponesha maisha ya watu ili kuweka madai binafsi lazima kuwepo na njia ambazo unaweza zitumia kwanza kabla ya kufikia maamuzi hayo.

Ndio maana Hospital na madaktari huendelea kutibu watu hata wakati wa vita vinaendelea na ni makosa ya kimataifa kushambulia Hospital na zaidi ya yote daktari hutibu hata adui aliyejeruhiwa bila kumtenga. Huu ndio Uzalendo unaotangulia na hakika daktari anaweza kumtibu mtu bure kama mtu huyo hana uwezo isipokuwa sheria za Hospital ama alipoajiriwa pekee ndizo zinaweza kumfunga asitoe huduma hiyo bure..

Kama wewe na wengineo mnafikiri kwamba haki hizi zinaweza kuombwa kwa makundi, kila mtu abebe msalaba wake basi mtakesha na hamtafanikisha hata moja na CCM itaendelea kuwakanyaga iwe JK au awe Lowassa au Asha Rose Migoro.. Sasa naanza kuelewa kwa nini Mkapa alituita wajinga na watu wenye wivu maana sisi sio wabunifu ktk kutatua matatizo yetu bali tunalalamika tuuu kumtaka yule aliyeshindwa kuona umuhimu achukue mawazo yenu..

Mkuu wangu mtanisamehe sana sintokubaliana na madai ya madaktari hasa baada ya kuona hawakupitia njia zozote za kisheria. Madai yao yanabadilika kila kukicha kwanza ilikuwa posho sasa wamebadilisha na kuwa mishahara yao midogo, sijui kuna Ufisadi unaotendeka lakini hawataki kuwataja wahusika. Majuzi tu rafiki yangu mtoto wake anaumwa walimpeleka Muhimbili haikujulikana kitu wakamhamishia AghaKhan mtoto kapewa kitanda week mbili akiongezewa maji tu wasimtibu mguu nje ndani kufikia kifo.. Matokeo yake wamempeleka India, haya nambie wamekuta ana infection ktk damu na leo siku ya pili kaanza dose na tayari kesha anza kupata nafuu. Kapoteza kiasi gani wala sina haja ya kusema!

Unataka kunambia madaktari wetu wote walishindwa kujua kwamba mtoto huyo alikuwa na Infection ktk damu? ni vipimo vipi haswa vilivyokosekana kiasi kwamba hata Zitto ilibidi akatibiwe India. Mwakyembe alikwenda India baada ya sisi kushindwa kumtibu wala kujua kama alipewa sumu.

Report iliyotoka India ndio wnaaitumia sasa hivi, Nina mdogo wangu kila mara anasumbuliwa na tumbo leo miaka 10 Hospital zetu hawajui anaumwa kitu gani waliisha mfanyia Operation ya Appendix kwa laki 6 miaka miwili tu iliyopita lakini hakuna nafuu hadi leo hii anasumbuliwa na tumbo.. Wamefanya vipimo vya Ctscan na Ultrasound hawaoni kitu wakati anazidi kuumia na maumivu na hawezi hata kukaa sehemu yenye baridi (air condition) kabisa..In total tumekwisha tumia zaidi ya 1.2 mil kwa tiba hapo Bongo lakini hana nafuu yoyote..Kwa hiyo viongozi wanapokwenda tibiwa India wanajua nyumbani hatuna madaktari wazuri pengine kwa sababu sawa kabisa na zile za walimu na shule za kata..

Hivyo mkuu wangu ndio maana nasema viongozi wetu hao Wabunge mnaowasema sana, hawa ni reflection yetu, Uozo wa madai ya wabunge hauna tofauti na uozo wa madai ya madaktari wetu na uozo wa fikra zetu sisi wenyewe. Madaktari hawakugoma kwa sababu hawana vifaa huu uongo sawa na ule wa Wabunge kudai maisha yamepanda sana Dodoma...wakati wamefanya kazi miaka yote ktk mazingira magumu zaidi ya haya ya leo kutokana na umaskini. Na nasema tena mimi nitamheshimu mwalimu anayefundisha watoto chini ya mti pasipo madawati kuliko yule anayegoma ili ajengewe nyumba ya kulala kuboresha maisha yake kwanza.

Tuishinikize serikali kwa makosa yake na tusitumie kabisa vigezo vya utawala mbaya ili sote tunufaike na utawala mbovu. Kama tunakubali CCM imeshindwa kuongoza na hatuwataki wabunge wetu zipo njia za UMOJA wetu kuweza kupambana na udhalimu huu. Maandamano ya pamoja nchi nzima kuigomea serikali ni mwanzo mzuri. Anzeni kujipanga kwenda Uwanja wa Uhuru (Mnazi mmoja) kuonyesha Upinzani wa Posho za wabunge na sio kusherehekea madaktari kugoma ili nao wapewe posho..Hamumkomowi JK wala CCM bali mnajikomoa wenyewe.
 
Nguruvi3,
Uzalendo hauanzi kwa mtu yeyote bali ni wajibu wa kila mwananchi - love of country and willingness to sacrifice for it!.. najua inakuuwia vigumu sana kuelewa kwa sababu kama leo hii itatokea vita Tanzania na mkaitwa kwenda kulitumikia taifa wengi wenu wataingia mitini..Hii ndio tofauti ya kimtazamo baina yangu na wewe na wengine wote kwa sababu ubinafsi kwanza. I will register na kwenda front lakini navyojua mimi Wadanganyika wengi watatafuta safari au mgomo maana tayari hata vita ya Uganda na Idd Amin wengi wanailaani. Mapinduzi Zanzibar yanalaaniwa kifupi Wadanganyika kwa asili ni wasanii kama JK na viongozi wengine wote - Maslahi binafsi mbele!
Maneno mengi lakini hakuna Uzalendo.
 
Back
Top Bottom