Mtazamo wangu kuhusu dear Tanzania

martialmtata

New Member
Jul 22, 2023
3
2
Tanzania ni nchi inayodondoshwa na wananchi ni vile tu lawama tumeamua kumpa Rais. Yes katiba imempa mamlaka makubwa sanaa rais lakini nchi haiwezi kuendeshwa wala kujengwa na mtu mmoja labda uwe dikteta. kwa mifumo ya kidemokrasia ni ngumu Sanaa

Wananchi wengi wamekosa accountability. Nenda ofisi nyingi za umma nenda shuleni nenda zahanati na kila seheme, nenda hata mtaani kwa wananchi, wananchi wanashiriki vikao vya mitaani kutunga sheria pia wanahoji matumizi na makusanyo ya pesa za serikali ya mitaa au vijiji.

Wananchi mnafatiria watoto shule wanafundishwa, daftari zao mnakagua unagundua asilimia kubwa hapana, je wananchi mnawajibika kulinda katiba na rasilimali za nchi, wafanya biashara wanalipa Kodi kihalali na kwa wakati au ujanja ujanja mwingi.

Nchi imekosa wazalendo, sasa hivi kaa na mtu yoyote anaetarajia kuajiliwa au ambaye kaajiliwa kwenye sekta za umma uone kipaumbele chake Cha kwanza, watu hawafikrii kujenga nchi akili nyingi wamehamishia katika kujenga familia zao, (Rais ataweza kweli kudeal na watumishi wote Tanzania mmoja baada ya mmoja) kwaio mda mwingi badala ya kufikria Jinsi gani nzuri ya kurahisisha na kubuni njia za kutatua matatizo (efficiency and creativity) mda mwingi watu wanafikria kuhusu kuneemesha familia zao.

Na ni kitu kinaungwa mkono na familia na rafiki, jamii inaamini kufanya kazi ofisi za umma na kuishi maisha ya kawaida ni dhambi " unatakiwa kuwa tajiri". Hii ni perspective inayopelekea watu kuiba, wewe ndo umepewa Rais utajenga vipi nchi na watu wanaofikiria mda wote kufanya hujuma

Wananchi ni waoga na wanafiki, Ni ngumu kujenga nchi na watu ambao wanashindwa kusimamia mitazamo na elimu zao.

Ni watu ambao wanaenda enda ni "autopilot " watu ambao mda wote wamekua wakifata order tu huwezi kuelewa umuhimu wa elimu zao ukisema hichi wanashingilia ukisema vile wanashingilia hawajaeleweka wanataka nini, au wanaamini nini. Kwa kifupi watu wameamua kutokutumia akili zao kwasababu yakutetea mishahara Yao na wengine hata mishahara hawana ili kuwafurahisha watu wachache kwa kutarajia na wao siku wawe kwenye mfumo.

Kwa aina hii ya wananchi kuwa developed country it's a nightmare hata aje Rais kutoka chama gani au nchi gani, Mimi naamini kama mifumo yote kuanzia chini itakua perfect and efficiency hata akija Rais gani nchi haiwezi kutolewa kwenye reli yake na mtu mmoja. Mchukue yule Rais ambae kapuyanga mpeleke Marekani uone kama ataweza kuiyumbisha nchi.

Maendeleo ya nchi ni huduma zinazotolewa na serikali shule elimu maji haki na kila kitu kutolewa kwa wakati na ubora sahihi, hafanyi Rais vyote unafanya wewe mimi na yule, je wewe umefanya katika ubora huo kwaio unagundua sio kitu Cha siku moja kuwabadilisha wananchi na mifumo.

Naamini ukiacha Rais Kuna mtu nyuma ndo alitufikisha hapa huyo ndo anapaswa kulaumiwaa. na mtu mwingine wa kulamumiwa ni mimi mwenyewe nini nimefanya katika nchi.
 
Back
Top Bottom