Yanayotokea Tanzania: Dola inafuata nyayo za Ethiopia!

Kabla uchaguzi wa 2020 lzm nitakuwa nishasepa bongo.

Nionavyo huko mbele, hali itakuwa mbaya sana, napambana niweke maisha mguu sawa nisepe zangu bongoo
 
Mara kwa mara nilikuwa najiuliza kwnn ethiopia vijana weng wanakimbia nch yao?kumbe tatizo ipo kwnye mfumo mbovu wa siasa unaoleta umaskini.
 
Nimeipenda No. 1. Ni kweli hakuna hata mmoja wa upinzani atarudi. Maana huyo Zitto huko ujiji alishalikoroga. Yaani kuna bara bara fulani imejengwa ujiji, yeye Zitto aliwahi kukataa isijengwe ujiji, basi wanamuona ni kimeo cha hali ya juu, na ndiyo maana anatafuta huruma, hahaha, yaani ubunge huyo mnafiki asahau kabisa. Wana ujiji vijana kwa wazee hawataki kabisa kumsikia
Acha unafiki wewe. Kama alimtia mkeo lazima uwe na hasira
 
Ethiopia si ya kuiga. Wahamiaji haramu wanaokamatwa kila uchao wakiwa na njaa ya wiki kadhaa kwenye ma container safarini kuelekea bondeni ni raia wa Ethiopia. Ni hatari sana wananchi katika nchi yao wanapokosa kuwa na furaha na yanayoendelea. Hasa hasa kunapokuwa na mkono wa chuma ni balaa zaidi hayo ndiyo ya Ethiopia na hao wanao kimbia nchi yao in a nutshell.
 
Kila kinachoendelea hakuna jipya ila ni maigizo ya bonge ya movie ya huko Ethiopia.

CCM wangependa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ufanye kazi kwa sharti moja tu uwaimarishe wao vinginevyo nchi ibaki ni ya demokrasia ya vyama vingi kwenye makabrasha tu: In Ethiopia, a Cautionary Tale for Tanzanian Democracy Activists

Ethiopia kabla ya 2005, walijaribu kupanua wigo la demokrasia lakini wakajikuta wanamwagwa na ala zao.

Kilichofuatia demokrasia ikatiwa mfukoni na faulo zilirindima kila kona: mauaji, kesi za kubambikiziwa, NGO kufutwa, vyama vya upinzani mfukoni n.k

Hatua hizi zilikihakikishia chama tawala kushinda viti vyote vya ubunge na udiwani miaka 10 iliyofuata. Siyo kwa kukubalika kwenye boksi la kura bali kwa ubabe tu!

Nionavyo

1) Uchaguzi wa 2020, hakuna mbunge hata mmoja wa upinzani kurudi bungeni.

2) Kutokana na hizi faulo na kauli za Jaji Mkuu tutegemee kama Ethiopia Mahakama kushughulikia na wapinzani.

3) Baada ya 2020, katiba kubadilishwa na kufuta ukomo wa Urais na kuongeza muda wa mihula kutoka 5 hadi 7.

4) Wapinzani wengi aidha kuuawa na wasiojulikana au kutiwa lupango.

5) Fungu la wafadhili kutoweka na kuleta msukumo wa kupandisha na kupanua wigo LA kodi kutafuta pesa ya kuwalinda walaji wachache wasiwageuke.

6). Uchumi kuporomoka na maisha kuwa magumu mno.

7) Kipimo cha ugumu wa maisha ni vijana wengi kukimbia nchi kama Ethiopia na Zimbabwe.

8). Uongozi uliopo wa upinzani kutinduliwa kwa wananchi kukosa imani nao au kuwa jela au makaburini.

9) Ndani ya CCM ya baada ya 2020 kugawanyika kutokana na ugumu wa maisha na mkate kuliwa na wachache.

10) Tegemea kama Ethiopia na Zimbabwe upinzani wa nguvu kuibuka ndani ya CCM siyo upinzani.
SSgt

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom