Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumanne 5 Agosti 2014, Mjadala wa Bunge Maalum la Katiba

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, amani iwe kwenu.

Natumaini kwamba hamjambo na Mungu Muweza amewaafikisha kuiona vema siku ya leo. Kwa wale wagonjwa tuzidi kumuomba Allah awajaalie wapone mapema. Na wale waliotangulia mbele ya haki Mwenyezi Mungu awalaze mahala pema Peponi. Ameen

wadau, baada ya mapumziko ya zaidi ya miezi miwili, Bunge Maalum la Katiba linaendelea tena leo Mjini Dodoma. Jana tarehe 4 Agosti 2014, Kamati ya Uongozi ilikutana kujadiliana masuala kadhaa juu ya bunge hilo. Yapo masuala kadhaa waliyoafikiana kubwa zaidi ni kufanya marekebisho ya baadhi ya kanuni ili kuboresha mfumo wa kuendesha bunge hilo. Kuna kanuni 11 zitafanyiwa maboresho kwa siku ya leo. Nitawatajia hints za mambo mawili tu kutokana na umuhimu wake.

  1. Ili kudhibiti tabia ya baadhi ya wabunge kuchukua posho (Per Diem) na kutohudhuria vikao vya Bunge, maboresho yatafanyika ili wabunge wa aina hiyo wasiwe na haki ya kuchukua posho. Kwa utaratibu wa awali ni kwamba wabunge wote walipewa Perdiem ila kwa wale ambao walikuwa hawahudhurii vikao walikuwa wanakosa posho za vikao tu. Hali hiyo itaokoa fedha nyingi ambazo zilikuwa zinapotea kwa wabunge wasiofanya kazi za Bunge Maalum kutokana na sababu mbalimbali.
  2. Marekebisho mengine yatahusu utaratibu wa mijadala ya Sura za Rasimu. Kwa mujibu wa Kanuni, Bunge linajadili sura mbili mbili. Hata hivyo, marekebisho yatafanyika ili Bunge lijadili sura zote 15 zilizobaki kwa pamoja kwa utaratibu ufuatao;

  • Wabunge watajadili sura zote 15 ndani ya Kamati 12 za Bunge Maalum. Zoezi hilo litafanyika kwa siku 15 kuanzia kesho tarehe 6 Agosti 2014
  • Baada ya mijadala ndani ya kamati kukamilika, Kamati zitapewa siku 3 kuandika taarifa za kamati kwa sura zote 15
  • Baada ya Kamati kukamilisha taarifa za Kamati, Kamati hizo zitawasilisha ndani ya bunge hilo taarifa zake na zoezi hilo linatarajiwa kuchukua siku 5.
  • Baada ya kamati kukamilisha uwasilishaji wa Taarifa, Mijadala juu ya Sura hizo itaanza.
  • Mijadala ikikamilika Bungeni, Kamati ya Uandishi itaandika Sura zote kwa kuzingatia maoni ya taarifa za kamati na mijadala bungeni
  • Kamati ya Uandishi itawajibika Kuwasilisha Bungeni Mpangilio wa sura baada ya maobresho. Wabunge watazipitia tena na kufanya marekebisho stahiki.
  • Baada ya Bunge kukubaliana na kazi ya Kamati ya Uandishi, ndipo zoezi la upigaji kura litafanyika. Kwa hali hiyo, Sura zote zitapigiwa kura kwa pamoja mwisho wa Bunge hilo.

kazi kubwa kwa siku ya leo itakuwa kurekebisha kanuni hizo na inatarajiwa kuwa zoezi hilo litakamilika ndani ya siku moja. Kuanzia kesho, Bunge Maalum litaendelea vikao vyake ndani ya Kamati kwa siku 15. Kama kawaida mimi pamoja na wadau wengine tutawaletea moja kwa moja mijadala ya Bunge Maalum kama itakavyojitokeza Mjini Dodoma. Natarajia ushirikiano kutoka kwa wadau wote ambao tulikuwa nao kuanzia Februari 18 mwaka huu.

Usikae mbali. Stay Connected

[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=175389&d=1407250303
[/JFMP3]
 

Attachments

  • Mwigulu Nchemba.mp3
    3.7 MB · Views: 612
Kwa mliopo eneo la tukio bunge linaanza saa ngapi?

Saa tatu kamili asubuhi

Star TV
 
Rais unachezea pesa zetu bure!hiyo katiba itakua ni ya watu wachache sii ya watanzania
 
Katiba ya Chama Cha Mainterahanwe (CCM). nani apoteze muda kufuatilia? Kwangu itakuwa rahisi kutangaza injili kule kwa boko haram kuliko kufuatilia hawa Mainterahamwe
 
Mchakato huu unaendelea kuutumikia mfumo uliopo kwa kuendekeza uchama kwenye masuala ya katiba ya nchi, unalipeleka taifa katika mgawanyiko zaidi kuliko umoja zaidi, mbaya zaidi bilioni 24 zinateketea kwa kufanya maigizo haya!
 
tupo pamoja ngoja watumwa wa mabepari UKAWA wakae nje wanakula 400,000 kwa siku ili wasaliti, sisi tuwaombee wazalendo waliokwenda kupambana.
Nasubiria kwa hamu siku ya kujadili umilikiji wa ardhi kwa wazawa vijana tutapaza sauti maana kwa hilo hatuna mchezo.
 
Back
Top Bottom