YALIYOJIRI: Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za CCM - Viwanja vya Jangwani, Dar-es-Salaam

Huyo mkapa namheshimu tu kwa sababu alishawahi kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania. Ila wadau kuna mambo huyo mzee katufanyia chuoni na sina hamu nae tena. Mkapa ndiye mkuu wa chuo kikuu cha dodoma, ila cha kushangaza ameshindwa kutatatua kero za msingi zinazowasibu wanafunzi chuoni kwa maslahi yake binafsi. Nina mengi ila nina moja tu nitakalozungumzia. Wanafunzi chuo kikuu cha dodoma wanalipa sh 100000/= kama hela ya afya. Sh 50400/= kwa ajili ya bina na Sh 49600/= kwa ajili ya usafiri. Cha kushangaza mwaka wa masomo 2014/2015 wanafunzi chuoni tuliondolewa mfuko wa bima pasipo sababu ya msingi. Hela yote imeenda mfuko wa chuo na leo hii mwanafunzi akipata safari ya gafla na akaumwa kwa dharura njiani hana chake tena. Mbali na hapo tumejaribu kuuliza na kuomba kiasi hicho cha hela kipungue lakini mwisho wa siku tumegonga mwamba. Vyuo vingi vya tanzania hasa vya serekali wanafunzi hawalipi hicho kiasi cha hela ila nashangaa kwa nini UDOM? Ndio maana mnasikia wanajisifia wajijenga UDOM kwa mwamvuli wa kusema wanawasaidia watanzania. Mkapa ni mtu mkubwa tena kada ndani ya ccm, leo hii anasimama na kusema ccm ndio chama cha ukombozi. Kuna chama cha ukombozi kinachowafanya watanzania hasa wanyonge mtaji??????
 
Warioba poooole...jamaa(JK) kaanza kumfagilia Samia kuhusu uongozi wa BMK na kufanikisha upatikanaji wa katiba safi(anamaanisha katiba pendekezwa ambayo Warioba aliipinga kwa nguvu zoote)

Warioba ndiyo kashajifunga mdomo jumla hana la kuongea tena kuhusu katiba.
Polepole ndiyo kashadedishwa jumla kuhusu katiba
 
Back
Top Bottom